Sitamani kukutana na mtu yeyote tuliyejuana kupitia mitandao

Watu wenye matatizo ya akili kama Trump wako wengi siku hizi humu JF....hivi walifukuzwa Instagram na Fesibuku?
 
ILIPOISHIA...

Yule aliyejiita mwanadadaa nakumbuka alitokea majira ya saa sita mchana na gari yake akidai nimfuate niingie garini tukaongee ofisini kwake,huku hajui namuona apparently katika maeneo niliyojitega.

SASA ENDELEA...

Nikiwa nipo juu nje ya kighorofa flani wanauza nguo nikaanza kumdodosa huyu aliyejiita mwanadada,kumbuka hapo ni text tu tena kwa kutumia WhatsApp, lakini hataki kupokea call wala text za kawaida.

Nikiwa napretend kwa kujivisha uhusika wa jamaa mmoja ninayemuona kwa chini anachoma mahindi,basi nikamtext yule mwanadada kwamba "mimi nipo hapa kwa huyu muuza mahindi na nimekaa hapa nakula mhindi,nieleze gari yako ipoje ili nikufate twende huko ofisini kwako?" Yule dada akaanza kunielekeza.

Cha ajabu maeneo aliyokuwa akinielekeza hapakuwa na parking lots, maelekezo yake kwakweli hayakuwa wazi sana akili yangu iki-click kuwa huyu naye anataka kuni-survey kabla ya kukutana nae kabisa ili tu ajidhatiti mapema kwamba anaenda kukutana na MTU wa aina gani(kama atam-mudu au la hasha).

Nikampa mtego mdogo,nikamwambia hivii,pokea video call yangu uonyeshe maeneo yanayokuzungua hapo itakuwa rahisi mimi kupajua na kukuona kiurahisi maana hapa makumbusho ni mitaa yangu ya kujidai sana. Ndipo alipokubali nami nikamrukia kwa hewa, mtandao ulipounga fresh video ikasoma poa sana basi akaizungusha kamera yake kuonyesha maeneo aliyokuwepo hapo makumbusho,lakini chinichini naskia sauti za mijitu kama ya miraba minne ikizungumza huku ikikohoa kwa mbaali kana kwamba inavuta sigara na kupaliwa kwa moshi wake.

Sasa katika kujiridhisha zaidi nikamuuliza mwanadada umesema upo peke yako? Akajibu ndio kwani vipi? Niakamuuliza tena, Upo sahihi na maneno yako? mbona kama navunjika moyo na uaminifu wako? Ndipo yule dada akatoka ndani ya gari huku nikiskia kabisa akifungua mlango,ebanae akanidanganya ni watu wa kupita njia mimi mbona nipo alone tena garini ndani.

Lakini muda wote huo hakutaka sura yake ionekane japo kweli sauti ilikuwa ya kike mwenye kujiamini sana. Katika kuongea ongea huku nikifanya movement za hapa na pale( kumbuka bado nipo ghorofani) na nimefanya kwa makusudi ili huyu mdada aamini namfuata huko aliponiita.

Ebwanae mungu akiwa na nia ya dhati juu yako lazima akuletee ishara zote,yule Dada ndio aliponyoka na kuonyesha uso wake kwa bahati mbaya ghafla nilichoweza kuona ni kiji-maiki kidogo kimetoka kwenye sikio lake hadi mdomoni akikitumia kuongea na kuniskilizia sura akiwa amekomaa flank,somewhat age.

ITAENDELEA....

JAMANI NAJAWA NA HOFU HATA HAPA NILIPO BADO SINA AMANI YA KWELI,TUKIO BADO BICHI SANA NAOMBA SUBIRA ZENU NITAWEKA KILA KITU HAPA ILA AKILI YANGU INAHITAJI SANA KUTULIA MAANA NI KAMA NIMETOKA KWENYE MDOMO WA MAMBA KIMASOMASO.

CC:Zuleykha na mengine wore.
Sawa mkuu tunasubiria
 
Back
Top Bottom