Sitamani kukutana na mtu yeyote tuliyejuana kupitia mitandao

thA goD

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
1,941
1,843
Hili ni jambo mtambuka sana kwa jinsi mambo yalivyo.
Imefikia hatua sasa humjui nani simba nani swala yani hatutambuani kabisa na hii hupelekewa na hofu kwa yaliyokwishatokea kupitia wapendwa wetu.

Mkasa wa kweli:: Ni wiki inapita Tangu anitafute jamaa mmoja huko Fb akijitambulisha kama(jina kapuni) kwamba yeye anaishi Uganda ila Dada yake anaishi Tanzania akiwa anaendesha miradi yake hapa.

Kupitia maongez na jamaa huyo aliniomba kama sitojali niweze kujiunga na Industry ya dada yake kwa malipo ya $200/week mwanaume nikasema tamaa haiwezi niponza hapa lazima nicheze kama undercover.

Katika kujitafutia uthibitisho kwanza wa location za huyu Dada mtu aliyetaka nikutane nae Dar,maeneo ya Makumbusho nilimuomba anitumie namba yake ili nimpigie na hakika haikuwa kupiga bali kutaka kuipata code namba yake na kuweza kujiridhisha na location anayoitaja(I'm hacker beginner).

Baada ya kupatiwa naomba zake cha kwanza code namba haikuw +255 first discovery, kidume nikajipush video call WhatsApp, mdada hataka kupokea akidai simu haina front camera,nikasema enhee wasiojulikana hawa hapa.

Mnamo tar mbili january hii nikajistosa Makumbusho kwenda kukutana na mlimbwende huyu mwana miradi,kilichotokea Sasa mwenyewe nilijipa ma-credit kwa kucheza kama pelle pale Makumbusho.

Yule aliyejiita mwanadada nakumbuka alitokea majira ya saa sita mchana na gari yake akidai nimfuate niingie garini tukaongee Ofisin kwake,huku hajui namuona apparently katika maeneo niliyojitega. Unataka kufahamu kilichokea baada ya hapo put some much likes to this thread.

Jaman hii dunia ina mengi sana nyuma ya pazia tena kila siku bila sisi kujua. Welcome again.
 
Back
Top Bottom