Sitamani kufuga kuku tena.

sinajinasasa

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
2,989
4,127
Nilitamani kufuga kuku wa kienyeji ili nivune mazao yao.

Changamoto ninayoipata ni wadudu jamii ya utitiri. Yaani ukienda kuwafungulia banda lao unakumbana na utitiri wa kufa mtu.

Hapa nilipo mwili mzima unawashwa kwa sababu ya kung'atwa na hivi vijidudu, nimevipangusa kutoka mwilini zaidi ya 100. Mwili umevimba kwa kujikuna, sitaki tena hawa kuku wa kienyeji bora niendelee kununua mayai.

Kama kuna mtu anajua dawa/mbinu ya kuwaangamiza hawa wadudu anisaidie.
Naleta na picha ya jinsi nilivyojikuna, hadi nguo zote nimevua

.
1556961269002.jpeg
 
Tumia hiyo dawa aliokushauri hapo juu Chupayamaji,wakiisha endelea tu na ufugaji wako,cha muhimu uwafuatilie ili kujua magonjwa yao na utafute duka la dawa za mifugo karibu na kwako pia uwe na namba yao ya simu itakusaidia kuongeza mazao...
 
Tatizo lako la kwanza wewe ni mchafu by professional kwenye mabanda yako ya kuku na kimsingi usafi ndio tiba kubwa ya kwanza.
Hakikisha mabanda yako unafagia kila Siku lakini pia sehemu ambayo kuku aliatamia mayai mwaga akher powder baada ya kuku kuangua mayai.
Ila kwasasa kwakua tayari umeshazalisha utitiri,safisha banda lako vizuri kisha nyunyiza akher powder banda zima hao utitiri hutawaona.
 
Nenda kwenye dawa za mifugo dawa ipo mbona? Dunia hii huwa hakuna mteremko hivyo pambana mkuu!!
 
Uwe unakata kucha pia
Nilitamani kufuga kuku wa kienyeji ili nivune mazao yao.
Changamoto ninayoipata ni wadudu jamii ya utitiri. Yaani ukienda kuwafungulia banda lao unakumbana na utitiri wa kufa mtu. Hapa nilipo mwili mzima unawashwa kwa sababu ya kung'atwa na hivi vijidudu, nimevipangusa kutoka mwilini zaidi ya 100. Mwili umevimba kwa kujikuna, sitaki tena hawa kuku wa kienyeji bora niendelee kununua mayai.
Kama kuna mtu anajua dawa/mbinu ya kuwaangamiza hawa wadudu anisaidie.
Naleta na picha ya jinsi nilivyojikuna, hadi nguo zote nimevua.View attachment 1087682
 
Sasa hutaki tena kufuga kuku au unataka dawa/mbinu zakutatua tatizo.?
 
Kuna dawa pia inaitwa servin powder vinakufa instantly. Ikiwa Kama una mbwa mbuzi paka kondoo wapake hiyo dawa. Itamaliza viroboto, chawa, na wadudu wote wa mifugo. Kisha zingatia Sana usafi.

Unaponunua mifugo mipya wakague kabla kuwachanganya wanyunyizie hiyo dawa kuua vijidudu ndio uwachanganye.
 
Hakikisha banda la kuku safi, na kavu, kwa kuku wanaotaga/atamia hakikisha cage inakuwa safi. Kama unatumia maranda chini hakikisha unatumia maranda makavu, binafsi huwa naweka chokaa chini halaf maranda ili kuzuia unyevu. Otherwise tumia powder uliyoshauriw hapo juu, mwagia kwa kuku, kwenye mabawa na shingo na mapaja na banda zima.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom