Sitakunyima hata unikere vipi kwa sababu ni dhambi.

Tamati

JF-Expert Member
May 15, 2017
1,085
1,957
Jana nikiwa naperuzi humu jukwaani nikakutana na uzi wa mdau akidai kuwa amemlisha mke wake chakula bila mboga sababu ya tabia ya mke wake kutompokea pindi anaporudi kutoka kwenye mihangaiko akiwa na mzigo wowote hatimaye jirani yake kampokea na kumpa nyama aliyokuwa amenunua.

Baada ya hapo niliamua nimshirikishe mpenzi wangu ambaye ndio mke wangu mtarajiwa Mungu akipenda kuhusu huo ujumbe wa mdau. Nilipiga screen shots nikamtumia WhatsApp maana yeye hayupo hapa(hana ID) JF.

Lengo la kufanya hivyo ilikuwa ni kumpima juu ya uelewa na mtazamo wake kuhusu haki ya mume kwa mke wake, akadai kitendo alichofanya mke wa jamaa sio kizuri na ni tabia mbaya. Akasema mke anatakiwa amheshimu mume wake ikiwemo kumpokea kila anaporudi kutoka kuhemea awe na mzigo au asiwe na mzigo na kuingia ndani kwa pamoja endapo mke alikuwa nje kwa muda huo, ili aweze kumfariji na uchovu pamoja na kumjulia hali kwa ujumla.

Kuhusu kitendo cha jamaa kunyimwa haki yake ya ndoa, alisema hivi kama inavyosomeka kwenye picha.

Wanawake jitahidini kutambua haki za waume zenu hata kama mtakuwa mumekwaruzana sio vizuri kutowatendea waume zenu haki zao maana mnapata dhambi kwa kitendo hicho. Pia wanaume mjitajidi kufanya hivyo hivyo, hasira zenu/zetu zisisababishe kunyimana haki za kindoa.

IMG_20190315_183356.JPG
IMG_20190315_183428.JPG
 
Mapenzi Ni tendo lenyewe haya mengine sijui kupokelewa Ni uvivu TU sio lazima.acha uvivu kwani Ni ujinga
 
mwanzoni wote hua hivyo, mkishaoana na kuish kwa mda mrefu wengi hujisahau. Anaweza kwambia chakula kipo mezani jihudumie mwenyewe na kusahau hata kukupakulia
Kama mnapendana kwa dhati hamuwezi kuchokana, mtavumiliana kwa kila jambo na kufurahia ndoa yenu vizuri bila kujali status zenu
 
Back
Top Bottom