Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Wazo Maridadi: Viongozi ni lazima muwe na misimamo. Misimamo thabiti inaonekana unapokuwa na madaraka. Kwamba madaraka hayakufanyi uje na misimamo ambayo usingekuwa nayo kama usingepata madaraka. Viongozi 'vijana' wanapoonekana wanachukua misimamo kwa ajili ya maslahi ya kisiasa (political expediencies) manake ni kuwa ni rahisi sana kubadilika badilika. Kama ulijikuta unalazimika kuchukua msimamo ambao dhamira yako inapingana nao ulikuwa na wajibu wa kujiuzulu wakati ule ule! Viongozi bila misimamo ni majanga!
Hapa nimewasema viongozi vijana lakini nawalenga viongozi wote ambao wakiwa na madaraka wanaonekana kuwa na misimamo ambayo inakinzana na dhamira zao. Wakikosa madaraka makubwa wanaanza kupata akili kuwa sasa 'wameokoka" na wanaweza kuona vizuri na wanazungumza kana kwamba wana "hekima". Fikiria baadaye Lugola aje na kusema "niliyosema kuhusu CCTV haikuwa msimamo wangu!"
Mojawapo ya vitu ambavyo havina ubishi ni kuwa misimamo ya JPM haijabadilika; hata kabla ya kuwa Rais misimamo yake kuhusu utendaji, viongozi na mambo mengine mengi ilikuwa inajulikana. Na inawezekana wengi walimchagua au kumuunga mkono kwa sababu hiyo na inawezakana akashinda kwa kishindo kikubwa zaidi mwakani kwa sababu hizo hizo.
Tatizo ni viongozi ambao wana misimamo kwa kuweka kidole hewani, kukitemea mate, halafu kukiinua hewani kuangalia upepo wa kisiasa unaenda wapi!
Unaweza kuninukuu!