Sitaki tena Sipendi: Viongozi Vijana Wasio na Misimamo Wakiwa na Madaraka...

Kipimo cha kukubalika kwa rais hauko kwenye sanduku la kura ambalo halina thamani yoyote kwa wenye mamlaka, hivyo kukubalika kwake haiko kwenye kipimo cha upigaji kura maana tume ya uchaguzi inaweza kufanya inavyotaka

Huko serikalini na chama tawala hakuna wazalendo Ila kuna walafi tu wa mali za umma na kujali matumbo yao binafsi

Sent using Jamii Forums mobile app
Inashangaza sana kua wapo watu wenye akili timamu wanao amini kua magufuli/ccm ati wanashinda kwa kutegemea sanduku la kura.

Au eti magufuli atashinda kwa kishindo kwa sababu ya misimamo yake.

KIfupi nae hana misimamo yoyete nje ya madaraka aliyonayo ni sawa na hao akina nape na makamba.
 
Mbona hata wewe Mzee mwanakijiji baada ya baba yako wa kisiasa Dr Slaa kuhama umebadilika na kukosa msimamo. Mmekuwa mkilamba matapishi yenu kwa kuyakana maneno yeny.
#Mayallaaaaaaa #Njaaaaaaaaaaaa
daktari slaa aliaamini kabisa kua magufuli alistahili kua jela kwa madudu aliyo yafanya.ila leo magufuli ni boss wa daktari slaa.

siasa itabaki kua ni siasa tuu.
 
Cheo ni dhamana, wengi hawalielewi hili na pindi wanapopata kazi kubwa hubadilika ghafla na kufanya mambo kwa kujionyesha kuwa "ana uwezo wa kufanya lolote
Tunayaona haya katika nchi za Africa tu ambapo mtu hata akiwa amekosea bado atakuambia nyamaza au "muweke ndani huyo"
Hii kauli wanaitumia wengi sana hata mtu akiwa kadhulumiwa haki yake na anaidai na kufungua kesi utasikia "uhamiaji mchunguzeni uraia wake"

Ni jambo la ajabu sana hili ambalo kwa hakika hata wao ancestor wao wametoka Zambia au babu zao wamezikwa Maputo.



Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Kuna ka ukweli hapo. Na hapa hatuzungumzii vitu ambavyo mtu anaweza kubadilisha mawazo kwa sababu ana taarifa bora zaidi kuliko alizokuwa nazo.. kubadili mawazo kunaruhusiwa na hata misimamo ipo inayobadilika. Kubwa ni kuwa misimamo inayoongozwa na kanuni fulani za msingi haipaswi kubadilishwa kirahisi rahisi. Chukulia kwa mfano, Nape angekuwa bado Waziri wa Habari na Michezo angekuwa amebadilisha msimamo wake sasa hivi?
Ni kama vile ambapo dr slaa angekua bado yuko upinzani angewashangaa sana watu wanao jiuzuru nafasi zao na kuunga mkono juhudi.

mzee mwanakijiji katika hilo kundi vijana wanafuata mkumbo kwa wazee wao,kwamba leo hiii waweza simamia jambo fulani na kesho ukakana misimamo yako na maisha yakaendelea.

dawa ili kua ni moja tuuu kukomesha huu ulaghai nayo ni kua na mifumo huru ya uchaguzi ambayo kura ya mwananchi kweli inaheshimiwa.huu ujinga ungeisha.
 
Hawa walitakiwa waachwe kwanza wakue na wapevuke..wasipewe madaraka yoyote hadi wakue..kama kina mzee mkuchika, mzee muhongo, mzee mwijage, mzee lukuvi, mzee mwakyembe, mzee kabudi na kina mama ndalichako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona Mwakyembe alibadilika akakana ile article yake! Huko ccm hamna cha mzee wala kijana wote ni matapeli ya kisiasa. Wanabadilika kutokana na upepo wa kisiasa pamoja na maslahi yao binafsi. Wote ni walafi tu
 
View attachment 1026826

Wazo Maridadi: Viongozi ni lazima muwe na misimamo. Misimamo thabiti inaonekana unapokuwa na madaraka. Kwamba madaraka hayakufanyi uje na misimamo ambayo usingekuwa nayo kama usingepata madaraka. Viongozi 'vijana' wanapoonekana wanachukua misimamo kwa ajili ya maslahi ya kisiasa (political expediencies) manake ni kuwa ni rahisi sana kubadilika badilika. Kama ulijikuta unalazimika kuchukua msimamo ambao dhamira yako inapingana nao ulikuwa na wajibu wa kujiuzulu wakati ule ule! Viongozi bila misimamo ni majanga!
Hapa nimewasema viongozi vijana lakini nawalenga viongozi wote ambao wakiwa na madaraka wanaonekana kuwa na misimamo ambayo inakinzana na dhamira zao. Wakikosa madaraka makubwa wanaanza kupata akili kuwa sasa 'wameokoka" na wanaweza kuona vizuri na wanazungumza kana kwamba wana "hekima". Fikiria baadaye Lugola aje na kusema "niliyosema kuhusu CCTV haikuwa msimamo wangu!"
Mojawapo ya vitu ambavyo havina ubishi ni kuwa misimamo ya JPM haijabadilika; hata kabla ya kuwa Rais misimamo yake kuhusu utendaji, viongozi na mambo mengine mengi ilikuwa inajulikana. Na inawezekana wengi walimchagua au kumuunga mkono kwa sababu hiyo na inawezakana akashinda kwa kishindo kikubwa zaidi mwakani kwa sababu hizo hizo. Tatizo ni viongozi ambao wana misimamo kwa kuweka kidole hewani, kukitemea mate, halafu kukiinua hewani kuangalia upepo wa kisiasa unaenda wapi!

Unaweza kuninukuu!
kama msimamo pekee humfanya mtu ajiuzulu mbona magufuli hakujiuzulu kwen
View attachment 1026826

Wazo Maridadi: Viongozi ni lazima muwe na misimamo. Misimamo thabiti inaonekana unapokuwa na madaraka. Kwamba madaraka hayakufanyi uje na misimamo ambayo usingekuwa nayo kama usingepata madaraka. Viongozi 'vijana' wanapoonekana wanachukua misimamo kwa ajili ya maslahi ya kisiasa (political expediencies) manake ni kuwa ni rahisi sana kubadilika badilika. Kama ulijikuta unalazimika kuchukua msimamo ambao dhamira yako inapingana nao ulikuwa na wajibu wa kujiuzulu wakati ule ule! Viongozi bila misimamo ni majanga!

Hapa nimewasema viongozi vijana lakini nawalenga viongozi wote ambao wakiwa na madaraka wanaonekana kuwa na misimamo ambayo inakinzana na dhamira zao. Wakikosa madaraka makubwa wanaanza kupata akili kuwa sasa 'wameokoka" na wanaweza kuona vizuri na wanazungumza kana kwamba wana "hekima". Fikiria baadaye Lugola aje na kusema "niliyosema kuhusu CCTV haikuwa msimamo wangu!"

Mojawapo ya vitu ambavyo havina ubishi ni kuwa misimamo ya JPM haijabadilika; hata kabla ya kuwa Rais misimamo yake kuhusu utendaji, viongozi na mambo mengine mengi ilikuwa inajulikana. Na inawezekana wengi walimchagua au kumuunga mkono kwa sababu hiyo na inawezakana akashinda kwa kishindo kikubwa zaidi mwakani kwa sababu hizo hizo.

Tatizo ni viongozi ambao wana misimamo kwa kuweka kidole hewani, kukitemea mate, halafu kukiinua hewani kuangalia upepo wa kisiasa unaenda wapi!

Unaweza kuninukuu!
msimamo wa magufuli upo wapi mkuu!
nyumba za umma zilipouzwa 1990s alikuwa wazir wa nyumba alisimama wapi?
msimamo wake juu ya kukataa magar yenye uzito mkubwa ulipopigwa chini na kina JK alosimama wapi?
msimamo wake juu ya wakazi wa kigamboni kupiga mbizi ulipovunjwa alisimama wapi?
msimamo wake juu ya bomoabomoa kule kanda ya ziwa ulipostopishwa na jakaya yye alisimia lipi?
wanasiasa wa kiafrika sio wa wa USA
 
kingewekwa kipengele kwenye sheria ya vyama kinachokataza mtu aliyehama chama kupewa madaraka ya juu ktk chama kingine hadi baada ya muda wa miaka kadhaa kupita.
Mwanakijiji nadhani umenielewa saaaaana kuhusu hili na sababu zake.
Kwa tukio la leo la EL kurudi CCM nadhani mnazidi kuelewa maana ya hiyo post yangu hapo juu.
 
Back
Top Bottom