Sitaki tena Sipendi: Viongozi Vijana Wasio na Misimamo Wakiwa na Madaraka...

hakuna mwanasiasa mwenye msimamo
1.Mbowe, Lissu ,Lema na Msigwa ndo walituaminisha kwamba Lowassa ni mwizi na fisadi, baada ya kuhamia kwao hoja wakaanza kuikwepesha kihuni huni eti mbona CCM haijampeleka mahakamani,

2.CCM wote akiwemo mwigulu nchemba waliwahi kusema Dr Slaa hafai kupewa hata ukatibu wa nyumba kumi kumi kisa kaiba Wake za watu kaacha na upadre, lakini siku anapewa ubalozi wao ndo wanasema kweli Slaa jembe alifaa kuwekwa pale,

3.CHADEMA walituaminisha kwamba Zitto kabwe ni nyoka kabisa hapaswi hata kusogelewa maana ni atari sana na akafukuzwa ndani ya chama , lakin leo wamempokea tena kwa aibu

4.CUF walihapa kabisa kutoshirikiana na CHADEMA kipindi cha ngwe ya pili ya Jakaya wakisema kwamba CDM imewatukana kwamba ni CCM B na ni liberal yaan wa mlengo wa kati na wana sapoti ushoga lakin mwaka 2015 wakaunda UKAWA kabisa

5.KABUDI alisema kwamba katiba ya Warioba ndo suluhisho la matatizo lakin muda huu hakuna kitu

hivo siasa ndo zilivyo
 
Nape na January Makamba wameamua kumkiri Mungu wao , wasibughuziwe , wewe endelea na unayoyaamini lakini ni wazi kwamba hautafika kwenye ngazi walizofika huko ccm hata iweje
Mnachotwa akili kama maboya. Sio hawa waliosimamia uporaji wa haki za wagombea wenu (Slaa 2010 na Lowassa 2015) kuingia Ikulu? Mnakuwa kama watoto ambao wakipewa pipi au kuimbiwa wimbo mtamu mnaamini lolote lile. Nape na January bado ni CCM. Na CCM wote ni wale wale.

Jiskie huru kutukana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitakutukana ndugu Chahali , JF haijaruhusu matusi , na nadhani hukunielewa , mimi si mjinga wa kuwaamini Nape na January , nafahamu kila njama waliyoshiriki , bali andiko langu lililenga kumtahadharisha tu mwanachama mpya wa ccm ndugu Mwanakijiji kwamba wengine wanapopandisha maruhani na kuanza kuropoka uchawi walioubeba kwa niaba ya waliowatuma hana haja ya kuumia , kumbuka kwamba andiko la Mzee Mwanakijiji limelenga kuwashutumu vijana wanaoropoka yale waliyoyatenda gizani huko nyuma .

Lingine ni kwamba , kuwa huru tu kuandika hapa jf bila hofu ya kutukanwa , sheria za JF zjnakataza matusi , siwezi kukutukana kisa tu hauko upande wangu , ni hayo tu
 
View attachment 1026826

Wazo Maridadi: Viongozi ni lazima muwe na misimamo. Misimamo thabiti inaonekana unapokuwa na madaraka. Kwamba madaraka hayakufanyi uje na misimamo ambayo usingekuwa nayo kama usingepata madaraka. Viongozi 'vijana' wanapoonekana wanachukua misimamo kwa ajili ya maslahi ya kisiasa (political expediencies) manake ni kuwa ni rahisi sana kubadilika badilika. Kama ulijikuta unalazimika kuchukua msimamo ambao dhamira yako inapingana nao ulikuwa na wajibu wa kujiuzulu wakati ule ule! Viongozi bila misimamo ni majanga!
Hapa nimewasema viongozi vijana lakini nawalenga viongozi wote ambao wakiwa na madaraka wanaonekana kuwa na misimamo ambayo inakinzana na dhamira zao. Wakikosa madaraka makubwa wanaanza kupata akili kuwa sasa 'wameokoka" na wanaweza kuona vizuri na wanazungumza kana kwamba wana "hekima". Fikiria baadaye Lugola aje na kusema "niliyosema kuhusu CCTV haikuwa msimamo wangu!"
Mojawapo ya vitu ambavyo havina ubishi ni kuwa misimamo ya JPM haijabadilika; hata kabla ya kuwa Rais misimamo yake kuhusu utendaji, viongozi na mambo mengine mengi ilikuwa inajulikana. Na inawezekana wengi walimchagua au kumuunga mkono kwa sababu hiyo na inawezakana akashinda kwa kishindo kikubwa zaidi mwakani kwa sababu hizo hizo. Tatizo ni viongozi ambao wana misimamo kwa kuweka kidole hewani, kukitemea mate, halafu kukiinua hewani kuangalia upepo wa kisiasa unaenda wapi!

Unaweza kuninukuu!

Mkuu MM .... mbona hata wewe haujawahi kuwa na misimamo .... toa Kwanza boriti kwenye jicho lako kabla ya kutoa kwenye jicho la mwenzako
 
Kama ulijikuta unalazimika kuchukua msimamo ambao dhamira yako inapingana nao ulikuwa na wajibu wa kujiuzulu wakati ule ule! Viongozi bila misimamo ni majanga!

Leo hii katika nchi yetu hii hawa unaowatafuta utawapata wapi? Na sio vijana tu, na hata nenda vyama vyote vya siasa vilivyopo Tanzania!

Na kama wapo watu wa aina hii unaowazungumzia hapa, sasa hivi hawamo kwenye mambo ya siasa. Wanajifanyia shughuli zao nyingine kwa sababu hawaziamini siasa zilizopo nchini.

Sasa, sijui tufanye nini ili watu hawa tuwahamasishe waingie kwenye siasa zenye misimamo wanayo iamini.

Nadhani jambo la mhimu hapa ni kwa sisi kuchangia mawazo ni jinsi gani tunavyoweza kuziondoa siasa za unafiki zinazotawala wakati huu na kuingiza siasa zinazosimamiwa na watu wenye misimamo ya dhati kwenye mambo wanayoyaamini.

Jaribu siku moja kuleta mjadala kama huo hapa.
 
Kuna ka ukweli hapo. Na hapa hatuzungumzii vitu ambavyo mtu anaweza kubadilisha mawazo kwa sababu ana taarifa bora zaidi kuliko alizokuwa nazo.. kubadili mawazo kunaruhusiwa na hata misimamo ipo inayobadilika. Kubwa ni kuwa misimamo inayoongozwa na kanuni fulani za msingi haipaswi kubadilishwa kirahisi rahisi. Chukulia kwa mfano, Nape angekuwa bado Waziri wa Habari na Michezo angekuwa amebadilisha msimamo wake sasa hivi?
Mbona leo umekuwa hivi, au sijakuelewa vizuri?
 
kingewekwa kipengele kwenye sheria ya vyama kinachokataza mtu aliyehama chama kupewa madaraka ya juu ktk chama kingine hadi baada ya muda wa miaka kadhaa kupita.
Mwanakijiji nadhani umenielewa saaaaana kuhusu hili na sababu zake.
 
Ninao waona mimi wa kwanza ni mzee wa kutapatapa Nape Nauye na waziri anayesemekana hajalizika na wizara aliyopewa bwana January Makamba
WAMEANZA KUFANYA TIMING KUNA WALIO NYUMA YAO UMAARUFU WALIOUPATA AWAMU ILIYOPITA ULIKUWA UJANZA NA DEAL TU

UTENDAJI HAUPIMWI KWA MANENO YA MWAMBAO

Sisi 2035 tutakuwa na JPM
 
Kuna ka ukweli hapo. Na hapa hatuzungumzii vitu ambavyo mtu anaweza kubadilisha mawazo kwa sababu ana taarifa bora zaidi kuliko alizokuwa nazo.. kubadili mawazo kunaruhusiwa na hata misimamo ipo inayobadilika. Kubwa ni kuwa misimamo inayoongozwa na kanuni fulani za msingi haipaswi kubadilishwa kirahisi rahisi. Chukulia kwa mfano, Nape angekuwa bado Waziri wa Habari na Michezo angekuwa amebadilisha msimamo wake sasa hivi?
Huyo njaa imehamia kichwani kila siku anaharisha maneno

Awamu hii ngoja Watanzania halisi wajulikane

Malkia wa Tembo hatimae kalazwa na uniform
 
Pia ifike mahali nyie akina Chahali,na wenzenu wa kule kwa "mwewe" mujiwekee taratibu zenye afya kwa nchi namna ya kuingilia mifumo ya vyama,lengo lisiwe kubomoa chama,bali kubomoa kilicho kibaya ndani ya chama na kusimamisha chenye maslahi ya taifa,na mnaweza kufanya hivyo kwa kuweka watu wenu ndani ya vyama vyote kwa muda mrefu,wakulie ndani ya hivyo vyama,watumike kuhakikisha maslahi ya msingi ya mtanzania yanajengeka,ifike mahali tusiogope kuikabidhi nchi kwa ccm,chadema etc.ifike mahali members individual wa chama lets say CCM wakiona CHADEMA ni hatari kwa maslahi ya CCM,isiwe lazima CCM kama chama kiwe na mtazamo huo,kwa maana ya uwepo wa network yenu kotekote inayofanya regulation ya mambo kotekote.Ifike mahali Rais wa nchi asiogope kumpa kijiti mshindi wa chama chochote kile,kwa vile "wenyewe" mna mizizi kote.Na sio mizizi ya kupandikizwa ghafla tu kwa hama hama,bali iliyokulia humo humo ndani ya vyama husika kwa maslahi ya kitaifa,si maslahi ya chama kingine ndani ya chama kingine,au maslahi ya watu binafsi.Kama ingekuwa hivyo sidhani kama leo kungekuwa na ulazima wa kuanzisha sheria zenye utata kulazimisha regulation ya vyama.Atmosphere ya kisiasa ni lazima ibadilike,tuonekane kuwa na demokrasia,huu udhibiti wa mambo na watu uende underground,unoticed.Sijui nimeeleweka manake najaribu kusema kitu fulani hapa.
 
Mnachotwa akili kama maboya. Sio hawa waliosimamia uporaji wa haki za wagombea wenu (Slaa 2010 na Lowassa 2015) kuingia Ikulu? Mnakuwa kama watoto ambao wakipewa pipi au kuimbiwa wimbo mtamu mnaamini lolote lile. Nape na January bado ni CCM. Na CCM wote ni wale wale.

Jiskie huru kutukana

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni lazima tuwatoe kwenye gumzo lenu la Tundu Lissu..tunaelekea kufunga kitabu cha Tundu Lissu tukimuacha na magongo yake..hivi leo anaingia oparesheni nyingine au nimekosea?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mojawapo ya vitu ambavyo havina ubishi ni kuwa misimamo ya JPM haijabadilika; hata kabla ya kuwa Rais misimamo yake kuhusu utendaji, viongozi na mambo mengine mengi ilikuwa inajulikana
Tafuta kauli zake wakati wa kampeni na leo! Aliyoyaasema na kuahidi wakati wa kampeni ni tofauti kabisa. M/Kijiji Huwezi kufanya reasoned analysis kwa vile u-home boy unakufunika usoni usione.
Vipengele vingine katika andiko lako nakuunga mkono... watu wanafanya vitu tofauti na dhamira zao kwa ajili ya njaa za matumbo yao. Wanaangalia Boss wao aliyewateua anasema nini! Hata wewe akitoka jiwe madarakani, utabadilika kama ulivyobadilika misimamo yako alipoingia Jiwe. Hukuwa hivi kutetea mauaji ezi za Kikwete, NAWE UMEBADILIKA
 
Nimebadilika nini?
 
Back
Top Bottom