Sitaki tena Sipendi: Viongozi Vijana Wasio na Misimamo Wakiwa na Madaraka...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,045
2,000
1550608033396.png

Wazo Maridadi: Viongozi ni lazima muwe na misimamo. Misimamo thabiti inaonekana unapokuwa na madaraka. Kwamba madaraka hayakufanyi uje na misimamo ambayo usingekuwa nayo kama usingepata madaraka. Viongozi 'vijana' wanapoonekana wanachukua misimamo kwa ajili ya maslahi ya kisiasa (political expediencies) manake ni kuwa ni rahisi sana kubadilika badilika. Kama ulijikuta unalazimika kuchukua msimamo ambao dhamira yako inapingana nao ulikuwa na wajibu wa kujiuzulu wakati ule ule! Viongozi bila misimamo ni majanga!

Hapa nimewasema viongozi vijana lakini nawalenga viongozi wote ambao wakiwa na madaraka wanaonekana kuwa na misimamo ambayo inakinzana na dhamira zao. Wakikosa madaraka makubwa wanaanza kupata akili kuwa sasa 'wameokoka" na wanaweza kuona vizuri na wanazungumza kana kwamba wana "hekima". Fikiria baadaye Lugola aje na kusema "niliyosema kuhusu CCTV haikuwa msimamo wangu!"

Mojawapo ya vitu ambavyo havina ubishi ni kuwa misimamo ya JPM haijabadilika; hata kabla ya kuwa Rais misimamo yake kuhusu utendaji, viongozi na mambo mengine mengi ilikuwa inajulikana. Na inawezekana wengi walimchagua au kumuunga mkono kwa sababu hiyo na inawezakana akashinda kwa kishindo kikubwa zaidi mwakani kwa sababu hizo hizo.

Tatizo ni viongozi ambao wana misimamo kwa kuweka kidole hewani, kukitemea mate, halafu kukiinua hewani kuangalia upepo wa kisiasa unaenda wapi!

Unaweza kuninukuu!
 
gemmanuel265

JF-Expert Member
Feb 16, 2016
8,500
2,000
View attachment 1026826

Wazo Maridadi: Viongozi ni lazima muwe na misimamo. Misimamo thabiti inaonekana unapokuwa na madaraka. Kwamba madaraka hayakufanyi uje na misimamo ambayo usingekuwa nayo kama usingepata madaraka. Viongozi 'vijana' wanapoonekana wanachukua misimamo kwa ajili ya maslahi ya kisiasa (political expediencies) manake ni kuwa ni rahisi sana kubadilika badilika. Kama ulijikuta unalazimika kuchukua msimamo ambao dhamira yako inapingana nao ulikuwa na wajibu wa kujiuzulu wakati ule ule! Viongozi bila misimamo ni majanga!
Hapa nimewasema viongozi vijana lakini nawalenga viongozi wote ambao wakiwa na madaraka wanaonekana kuwa na misimamo ambayo inakinzana na dhamira zao. Wakikosa madaraka makubwa wanaanza kupata akili kuwa sasa 'wameokoka" na wanaweza kuona vizuri na wanazungumza kana kwamba wana "hekima". Fikiria baadaye Lugola aje na kusema "niliyosema kuhusu CCTV haikuwa msimamo wangu!"
Mojawapo ya vitu ambavyo havina ubishi ni kuwa misimamo ya JPM haijabadilika; hata kabla ya kuwa Rais misimamo yake kuhusu utendaji, viongozi na mambo mengine mengi ilikuwa inajulikana. Na inawezekana wengi walimchagua au kumuunga mkono kwa sababu hiyo na inawezakana akashinda kwa kishindo kikubwa zaidi mwakani kwa sababu hizo hizo. Tatizo ni viongozi ambao wana misimamo kwa kuweka kidole hewani, kukitemea mate, halafu kukiinua hewani kuangalia upepo wa kisiasa unaenda wapi!

Unaweza kuninukuu!
Kipimo cha kukubalika kwa rais hauko kwenye sanduku la kura ambalo halina thamani yoyote kwa wenye mamlaka, hivyo kukubalika kwake haiko kwenye kipimo cha upigaji kura maana tume ya uchaguzi inaweza kufanya inavyotaka

Huko serikalini na chama tawala hakuna wazalendo Ila kuna walafi tu wa mali za umma na kujali matumbo yao binafsi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Automata

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
2,636
2,000
View attachment 1026826

Wazo Maridadi: Viongozi ni lazima muwe na misimamo. Misimamo thabiti inaonekana unapokuwa na madaraka. Kwamba madaraka hayakufanyi uje na misimamo ambayo usingekuwa nayo kama usingepata madaraka. Viongozi 'vijana' wanapoonekana wanachukua misimamo kwa ajili ya maslahi ya kisiasa (political expediencies) manake ni kuwa ni rahisi sana kubadilika badilika. Kama ulijikuta unalazimika kuchukua msimamo ambao dhamira yako inapingana nao ulikuwa na wajibu wa kujiuzulu wakati ule ule! Viongozi bila misimamo ni majanga!
Hapa nimewasema viongozi vijana lakini nawalenga viongozi wote ambao wakiwa na madaraka wanaonekana kuwa na misimamo ambayo inakinzana na dhamira zao. Wakikosa madaraka makubwa wanaanza kupata akili kuwa sasa 'wameokoka" na wanaweza kuona vizuri na wanazungumza kana kwamba wana "hekima". Fikiria baadaye Lugola aje na kusema "niliyosema kuhusu CCTV haikuwa msimamo wangu!"
Mojawapo ya vitu ambavyo havina ubishi ni kuwa misimamo ya JPM haijabadilika; hata kabla ya kuwa Rais misimamo yake kuhusu utendaji, viongozi na mambo mengine mengi ilikuwa inajulikana. Na inawezekana wengi walimchagua au kumuunga mkono kwa sababu hiyo na inawezakana akashinda kwa kishindo kikubwa zaidi mwakani kwa sababu hizo hizo. Tatizo ni viongozi ambao wana misimamo kwa kuweka kidole hewani, kukitemea mate, halafu kukiinua hewani kuangalia upepo wa kisiasa unaenda wapi!

Unaweza kuninukuu!

Ninao waona mimi wa kwanza ni mzee wa kutapatapa Nape Nauye na waziri anayesemekana hajalizika na wizara aliyopewa bwana
January Makamba
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
8,387
2,000
Misimamamo ya JPM haijabadirika?

1. Aliapa kulinda katiba na kutawala kwa mujibu wa sheria
Mabadiriko: Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 aliivunja wazi na akasimamia uvunjaji huo kwa nguvu zote

2. Mwaka 2015 kwenye kampeni alisema kwenye utawala wake hakuna mwanafunzi anayestahili kupata mkopo atakosa mkopo
Mabadiriko: Vijana maelefu wenye ufaulu mzuri tu wa kuingia chuo wanakosa mkopo kila mwaka

3. Mwaka 2016 kwenye zoezi la uhakiki alisema hili zoezi ni la muda mfupi na wafanyakazi wataanza kupata Stahiki zao kwa mujibu wa sheria ya utumishi.

Mabadiriko: Nyongeza za kila mwaka na kupanda madaraja ya wafanyakazi kwa mujibu wa sheria HAKUNA

4. Alisema atapambana na ufisadi
Mabadiriko : -Badala ya kumkamata na kumshitaki DC aliyekamatwa ready handed akila njama za kutoa rushwa kumnunua diwani, yeye akampandisha cheo DC huyo na kuwa RC.

Badala ya kuwashitaki walioingia mikataba mibovu ya madini, na wale walioleta kampuni jinamizi ya IPTL yeye kamkamata Rugemalira na Seti tu vipi watu waliitajwa kwenye maazimio ya bunge?

5. Aliahidi kutawala na kutekeleza Ilani ya CCM
Mabadiriko : amegoma kutekeleza ilani kwa kukacha mchakato wa katiba mpya, hajatoa milioni 50 kila kijiji, na alitangaza kufukuza mabinti watakaopata mimba shuleni kinyume na ilani ya chama chake aliyahidi kuitekeleza!

Kwa hiyo ndugu yangu, JPM anabadirika badirika, akiahidi wakati mwingine hatekelezi au anatekeleza partial partial
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,045
2,000
Hawa walitakiwa waachwe kwanza wakue na wapevuke..wasipewe madaraka yoyote hadi wakue..kama kina mzee mkuchika, mzee muhongo, mzee mwijage, mzee lukuvi, mzee mwakyembe, mzee kabudi na kina mama ndalichako.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hii ilikuwa hoja yangu kwa muda mrefu; hata mtu kama Makonda.. madaraka ya kuongoza Jiji kubwa la Dar ni madaraka makubwa mno...
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,045
2,000
Mbona hata wazee hawana misimamo. Africa mwanasiasa yoyote hatabiriki wako selfish bendera fata upepo

Sent using Jamii Forums mobile app

Kuna ka ukweli hapo. Na hapa hatuzungumzii vitu ambavyo mtu anaweza kubadilisha mawazo kwa sababu ana taarifa bora zaidi kuliko alizokuwa nazo.. kubadili mawazo kunaruhusiwa na hata misimamo ipo inayobadilika. Kubwa ni kuwa misimamo inayoongozwa na kanuni fulani za msingi haipaswi kubadilishwa kirahisi rahisi. Chukulia kwa mfano, Nape angekuwa bado Waziri wa Habari na Michezo angekuwa amebadilisha msimamo wake sasa hivi?
 
KWADWO ABIMBOLA

JF-Expert Member
Jan 8, 2019
763
1,000
Najua walengwa ni Nape Nnauye na January Makamba. Wanaojifanya wameongoka kumbe wana kiu ya mamlaka. Wanatumia gia ya kujifanya wameongoka ili endapo watachinjiliwa mbali basi waende upande wa pili kinafiki kwa kigezo cha kuongoka.

Tatizo la hawa ni wongofu wa nusu nusu. Sauli alipoongoka na kuwa Paulo hakuongoka nusu nusu kama hawa. Hawa wanajifanya kuongoka na kuyakana maovu waliyowatendea watanzania ila wakipewa vyeo watajisahau na kuendeleza uchafu wao dhidi ya watanzania.

Binafsi sijashawishika na uongofu wa sampuli hii. Kama wanajiona waongofu kweli na wameona madhaifu kweli basi na wajikane nafsi zao na vyeo vyao. Waachane na mfumo walimoishi ambao unawapa fedha kidogo huku ukiumiza wananchi walio wengi.

Tuungane tukatae mifumo yote yenye viashiria vya uovu katika nchi ambayo inashabikiwa na wafuasi wa CCM. Tupiganie misingi mipya ya kikatiba imayoleta uhuru, haki, demokrasia ya kweli na maendeleo kwa wananchi wote bila ubaguzi.
 
cariha

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
14,460
2,000
Wanasiasa wengi akiwa na cheo husifia akitenguliwa cheo ndo hujifanya msema ukweli na kuponda sana. Nape angekuwa hajatumbuliwa angekuwa anasifia kila jambo. Ni bora hata kuwa na wanasiasa wenye misimamo na masilahi mapana ya taifa kuliko kushabikia watu au cheo, kitu ambacho ni hatari
Kuna ka ukweli hapo. Na hapa hatuzungumzii vitu ambavyo mtu anaweza kubadilisha mawazo kwa sababu ana taarifa bora zaidi kuliko alizokuwa nazo.. kubadili mawazo kunaruhusiwa na hata misimamo ipo inayobadilika. Kubwa ni kuwa misimamo inayoongozwa na kanuni fulani za msingi haipaswi kubadilishwa kirahisi rahisi. Chukulia kwa mfano, Nape angekuwa bado Waziri wa Habari na Michezo angekuwa amebadilisha msimamo wake sasa hivi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nautico

JF-Expert Member
Jul 28, 2017
258
1,000
View attachment 1026826

Wazo Maridadi: Viongozi ni lazima muwe na misimamo. Misimamo thabiti inaonekana unapokuwa na madaraka. Kwamba madaraka hayakufanyi uje na misimamo ambayo usingekuwa nayo kama usingepata madaraka. Viongozi 'vijana' wanapoonekana wanachukua misimamo kwa ajili ya maslahi ya kisiasa (political expediencies) manake ni kuwa ni rahisi sana kubadilika badilika. Kama ulijikuta unalazimika kuchukua msimamo ambao dhamira yako inapingana nao ulikuwa na wajibu wa kujiuzulu wakati ule ule! Viongozi bila misimamo ni majanga!
Hapa nimewasema viongozi vijana lakini nawalenga viongozi wote ambao wakiwa na madaraka wanaonekana kuwa na misimamo ambayo inakinzana na dhamira zao. Wakikosa madaraka makubwa wanaanza kupata akili kuwa sasa 'wameokoka" na wanaweza kuona vizuri na wanazungumza kana kwamba wana "hekima". Fikiria baadaye Lugola aje na kusema "niliyosema kuhusu CCTV haikuwa msimamo wangu!"
Mojawapo ya vitu ambavyo havina ubishi ni kuwa misimamo ya JPM haijabadilika; hata kabla ya kuwa Rais misimamo yake kuhusu utendaji, viongozi na mambo mengine mengi ilikuwa inajulikana. Na inawezekana wengi walimchagua au kumuunga mkono kwa sababu hiyo na inawezakana akashinda kwa kishindo kikubwa zaidi mwakani kwa sababu hizo hizo. Tatizo ni viongozi ambao wana misimamo kwa kuweka kidole hewani, kukitemea mate, halafu kukiinua hewani kuangalia upepo wa kisiasa unaenda wapi!

Unaweza kuninukuu!
Hata wewe ndio wale wale tu bendera tu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom