Sitaki, sitaki kuamini kuwa ANNA MAKINDA ndiye anayewaburuza wanaume wa nchi hii. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitaki, sitaki kuamini kuwa ANNA MAKINDA ndiye anayewaburuza wanaume wa nchi hii.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jumakidogo, Dec 7, 2011.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Dec 7, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Sitaki tu, sitaki kuamini kuwa wewe ndiye mwanamke mwenye roho nzuri kuliko wote Tanzania. Sitaki , sitaki kuamini kuwa wewe ndiye kiongozi wa chombo kinachotegemewa kutunga sheria hapa nchini, sitaki kuamini kuwa wewe ndiyo mwanamke unaewaburuza wanaume na akili zao pale bungeni. Sitaki kuamini kuwa mamlaka ya kuongeza posho mara tatu zaidi umetangaza bila kutumwa na mtu mwingine. Sitaki, tena sitaki kuamini kuwa wewe ndiye mwanamke wa kwanza katika historia ya nchi hii kuburuza muswada muhimu wa mchakato wa katiba mpya. Sitaki, sitaki kuamini kuwa, kwa mwendo huo utamaliza muda wa miaka mitano ukiwa spika. Sitaki kuamini kuwa wanawake wenzako wanakuunga mkono kwa misimamo yako isiyo na tija kwa nchi.. Sitaki kuamini kuwa una tofauti na wakabaji wanaotumia nondo mitaani kuwaibia watu. Sitaki kuamini kuwa, mwanao akiomba samaki hutampa, bali utampa nyoka. Sawa kabisa, endelea kubana lakini ipo siku utaachia. Sitaki kuamini kuwa wewe umepingana na kauli ya katibu wako kuhusu kuongeza posho za wabunge huku wafanyakazi wengine mishahara yao ni sawa na kitenda wili kisicho teguka. Sitaki, tena sitaki kuona hata sura yako.
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  KIGUMU Chama Cha Mapinduzi!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...