Sitaki kuamini kuwa vijana waliipigia CCM kura 2015

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Tukisema matokeo hayo yaligeuzwa kuna watu wanakwazika sana,lakini ukweli ndio huo upinzani ulishinda na ni vijana wachache sana wana mapenzi na CCM ila ni michezo michafu ambayo hua tunachezewa.

Nikifikiria vijana walivyokua na hamasa na ari kubwa sana kuichinjia mbali CCM, Vijana walifurika kwenye vituo vyote vya kupigia kura wakiwa na vichinjio vyao mikononi ikiwa ni Mara ya kwanza kufanya maamuzi hayo katika historia ya vyama vingiTanzania.Eti matokeo yanatoka CCM ndio imeshinda, mtu mpaka sasa unajiuliza CCM ilishinda kwa kura za kina nani? Maana wapenzi wa CCM hua ni kina mama na wazee kulinganisha na idadi kubwa ya vijana iliyokuwepo kwenye vituo.


Itoshe tu kusema kua yale ya Yahya Jammeh yana mwisho, michezo michafu ya kisiasa inayochezwa nyakati za uchaguzi itafikia umma utakapoamua.


Uchaguzi wa juzi wa madiwani ilikua kama mkakati wa CCM kutumia mbinu za kila aina kijisafisha kwa aibu ya uchaguzi mkuu 2015, walitumia nguvu nyingi za kila aina mpaka kutumia polisi ili washinde kufumba macho ya watu eti wanapendwa. Hii inaweza kua ndio reflection halisi ya 2020 itakacyokua na tayari wapinzani wameshaligundua hilo na wanalifanyia kazi na wanajiandaa vilivyo.


CCM kwa sasa wanalazimisha wananchi wawapende ili kufuta aibu ya 2015, lakini ukweli utabaki pale pale na mwisho utawafikia tu.


Tume huru ya uchaguzi na katiba mpya vipatikane kwa wakati ili kuepukana na haya.
 
CCM ilishinda kwa kishindoo. Na tutaendelea kuipigia kura na kwa umoja wetu, tutashindaa.
Vijana tuko vizuri na tumejipanga kuhakisha tunapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa serikali za miitaa.
Ushauri wangu kwa wapinzani, njooni na Sera zenye mashiko kwa watu wote na sisi wapiga kura tutawachagua na mtashindaa.
Ni ushauri wanguu tuuu
 
Acha ubwege kijana mambo yote yaliamuliwa kanda ya ziwa ndiyo waliamua rais awe Magufuli sasa nyie kura hamkwenda kupiga mkakesha mnakunywa viroba na bangi
 
CCM ilishinda kwa kishindoo. Na tutaendelea kuipigia kura na kwa umoja wetu, tutashindaa.
Vijana tuko vizuri na tumejipanga kuhakisha tunapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa serikali za miitaa.
Ushauri wangu kwa wapinzani, njooni na Sera zenye mashiko kwa watu wote na sisi wapiga kura tutawachagua na mtashindaa.
Ni ushauri wanguu tuuu

Sera zipi zenye mshiko?Za kukwapua halafu manfukia makaburi??Au zile za kupigia debe hata uvunjaji wa sheria??Zipi sera zenye mshiko?Za kutumia polisi na mahakama??
 
Unapo sema CCM ilishindwa na wakati ndio inayokuongoza kuna haja ya kupimwa uwezo wa kufikiri
 
Back
Top Bottom