Sitaki kuamini, Dk Chami, alikuwa Tanzania one, mara mbili?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitaki kuamini, Dk Chami, alikuwa Tanzania one, mara mbili?!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by isotope, May 1, 2012.

 1. i

  isotope JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 2,404
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa inasemekana alikuwa kichwa mbaya shuleni enzi zile, form four alipata A masomo aliyotahiniwa. Form six, A tupu. Mara zote hizo akiibuka Tanzania One. Amepewa wizara akafanya kama Mwanaasha wa Feza girls. Mi nashindwa kuelewa hizo A alizipataje? alikuwa anajilipua (kudesa)? au kazeeka? Wataalam naombeni jibu!
   
 2. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #2
  May 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  Anaonekana mtu makini lakini kanyonyoka nywele labda ndo sababu maana anakila dalili ya kisukari!
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Hata alipoenda UD aliwaburuza mno wenzake!!!kwenye utendaji ni tofauti sana ukizingatia kuna suala la mfumo mzima kuwa corrupt!
   
 4. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  weka uthibitisho hiyo Tz one mwaka gani na shule gan ? We ulitaka amsimamishe kazi Mkurugenzi wa TBS kwan yeye ndo alomteua? Kwann hawakumpa nakala ya report ili afanyie kazi? Acheni kuhukum watu kwa kusomewa taarifa za upande mmoja,weka kosa la waziri Chami lifahamike!
   
 5. m

  manyani Member

  #5
  May 1, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizo A's Haimaaanishi kuwa ni competent always....they are just academics and not necessarily reflect the real thing in the field. wengi ni watalaam wa theory lakini katika hali halisi ni vilaza tuu
   
 6. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #6
  May 1, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kujua vitu is one thing na kutekeleza kile unachokijua ni kitu kingine!Hakuna sehemu yoyote ambako imeshawahi kuonyesha kuwa mtu akiwa amefaulu vizuri basi atakuwa mtawala bora!

  Mytake: Wengine ni Wazuri wa Kumeza(Creaming Capacity) he might be among them!
   
 7. m

  manyani Member

  #7
  May 1, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo red umesema ukweli kabisa... mfano hao TBS hata mara moja hawajawahi kuwa na uongozi competent... hata ukipata CV za wakurugenzi waliopita wote ni ubabaishaji tuuu au la wanashirkiana na wizara kulea uzembe huenda kwa faida yao binafsi. na mara nyingi wamekuwa wakirithishana madaraka kila mmoja anapostaafu.. kwa nn wasilete watalaam wapya kutoka n'je ili kuleta mawazo mapya???/ kuna siri gani hapo?? ni vema kama TBS ikasukwa upya pia vinginevyo tutaendelea kuwa dampo tuuu!
   
 8. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #8
  May 1, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ugonjwa wa upungufu wa cd4 ndio unamsumbua.
   
 9. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #9
  May 1, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,823
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Mambo ya Leadership ni magumu yanataka mtu aliyezaliwa kuongoza sio kila mtu tu anakua na ndio maana mnaona hapa Tz tunapata shida maana viongozi wengi wamepatikana kwa rushwa
   
 10. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #10
  May 1, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Ukweli ni huu first class darasani mtaani(utendaji) mara nyingi huwa zero/poor
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  May 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kama ni darasani Dr Chami ni moto wa kuotea mbali. Alisoma Seminary form I-VI na kufaulu vibaya sana. Hapo UDSM aliwaburuza watu vilivyo. Ni mchumi mzuri sana. Wakati wa ule mgomo (wakati wa Mzee Mwinyi) huyu bwana naye alikumbwa maana alikuwa mmoja wa viongozi - hivyo unaweza kusema alikuwa mpiganaji fulani.

  Wakati wa Mkapa, alikuwa anafanya kazi kitengo cha ushauri wa uchumi (PEPAU) kilichokuwa kinapata support toka UNDP na alifanya vizuri sana. Nadhani ni kipindi hiki ndio alianza kushawishika kuingia kwenye siasa. Lakini kama tujuavyo tatizo tulilo nalo Tanzania sio mtu mmoja mmoja ni mfumo mzima.

  Kwa kifupi karama ya Dr Chami iko kwenye 'think tank' na sio utendaji kwa maana ya kuwa waziri au hata mkurugenzi. Kwa maoni yangu Dr Chami aachane ni siasa za front line, na ajikite kwenye office kama ESRF, IMF, World Bank etc.
   
 12. Kingmairo

  Kingmairo JF-Expert Member

  #12
  May 1, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 4,977
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  Kaka songoro! Nakuunga mkono kabisa siasa ni field chafu sana! Kumchukulia hatua ekelege kwa maneno ya wanasiasa ni kinyume na taratibu. Na pia ni lazima hatua zichukuliwe kukiwa na written evidence na sio tuhuma za maneno. Ila sehemu chami ambapo anabanwa ni katika kusimamia utendaji. Madudu yaliyotokea TBS hawezi kujitoa maana wizara yake ilipaswa kuujua huo udhaifu hata kabla kamati haijaufunua. Kwa hiyo kuna swala la kumuwajibisha mkurugenzi (ambalo mi naona Hawezi kuhukumiwa kwa kushindwa hilo sababu taratibu hazikukamilka kumruhusu kufanya hilo) na la pili ni kushindwa kufuatilia utendaji wa maeneo yanayomhusu hivyo kusababisha hasara. Hili hawezi kilikwepa.
   
 13. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #13
  May 1, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Inabidi muelewe shule kufaulu ni akili zako ila wizarani kuna politics na bureaucracy behind you. Sitetei mtu lakini system ikiwa mbovu hata mtu kama Nyerere asingeweza kuongoza. Kwa hiyo bila kurekebisha system tusitegemee hawa wasomi na hizo PhD zita badilisha chochote.
   
 14. s

  sawabho JF-Expert Member

  #14
  May 1, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Taaluma na siasa ni vitu viwili tofauti. Huyu Dr. alipaswa kuwa think tank wa kushauri maswala ya uchumi na sio mwanasiasa. Kama unataka kuua taaluma yako, ingia kwenye siasa ambayo inasemekana ni mchezo mchafu. Hata hivyo, shuleni alikuwa pekee yake, lakini katika utendaji wa Wizara kuna mambo mengi yanayomzunguka na hawezi kuamua pekee yake na yeye sio Mtendaji hapo Wizarani. Hata ukimchukua Mess au Drogba akamweka kama mchezaji wa Taifa Stars, ataonekana hajui kucheza.
   
 15. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #15
  May 1, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hiyo kwenye bold ndio uwezo wa kufanya nini?
   
 16. S

  Samkyjr JF-Expert Member

  #16
  May 1, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mimi bado naona dr chami bado ni bora kuongoza kwasababu sijaona waziri au naibu anayejibu maswari kwenye bunge hili kama yeye ila nahisi mfumo na mtandao kwenye wizara unawashinda kwenda sambamba.
   
 17. T

  TanzActive JF-Expert Member

  #17
  May 1, 2012
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 350
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Unashangaa nini sana

  Hujawahi kuona Daktari akivuta sigara ?

  hujawahi kuona Civil Engineer akichakuchua vipimo na magorofa kuanguka ?

  huawahi kuona computer scientist , hana antivirus kwenye computer yake ?

  Hujawahi kuona Askofu akiiba pesa za kanisa ?


  hujawahi kuona takukuru wakipokea rushwa ?

  Uadilifu sio Elimu !!!!
  Kuzingatia unachujua na kuamini kwamba ni sahihi ni Uadilifu hata kama wewe au mtu mwingine mtapoteza chochote kile
   
 18. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #18
  May 1, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  wazuri hawapendwi!
   
 19. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #19
  May 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  mkuu hapo kwenye RED ndio sehemu yenyewe, huyu jamaa mie nimemfahamu tangu zamani akisoma seminari, ni mtu mzuri sana ila kawaida ukiwekwa sehemu iliyo corrupt then inakusumbua na usipokuwa makini unajikuta umeingia humo, tabu sana inabidi kubadili mfummo mzima, swala la kubadilisha mawaziri bado sio suluhisho
   
 20. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #20
  May 1, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  isotope Mh Chami amekabidhiwa wizara ikiwa na watendaji wanaofanyakazi kama walivyozoea na yeye akawa sehemu ya mazoea
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...