Sitakagi ujinga: Hata miguu ni chombo cha usafiri, wavuka kwa miguu wapewe driving license class 'P'

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,063
40,724
Mtu asiruhusiwe kuvuka zebra au mataa bila kuwa na leseni ya udereva ya walau class P (pedestrian), atakayekiuka apigwe faini/ notification ya 30,000/= kama magari, asipolipa ndani ya siku saba apigwe penalty ya 25% kama gari, na zifungwe kamera za 'facial recognition' kwenye mataa ili kuwabaini watakao kwepa kulipa kama ilivyo kwa kamera za kukamata magari. Yaani unakuta mijitu inavuka kama nyumbu mtoni hovyo hovyo na kuhatarisha usalama wa waendesha vyombo vya moto vya usafiri, wengine wanakatiza hovyo kwenye bustani za barabarani kama vichaa. Nao wapigwe faini kama magari, na waonyeshe vyeti vya udereva wa miguu kutoka vyuo vinavyotambulika kabla ya kupewa leseni. Sitakagi ujinga.
 
Mimi nadhani ungetafuta tafsiri ya neno "Chombo" kwanza ndipo uhoji kuhusu uhalali wa Mwanadamu kuwa na leseni kwa ajili ya ruhusu ya kuvuka nayo barabara (Alama ya pundamlia).

Unaposema "tusivuke kwenye Zebra crossing","Yaani unakuta mijitu inavuka kama nyumbu mtoni hovyo hovyo na kuhatarisha usalama wa waendesha vyombo vya moto vya usafiri",Hujui kwamba dereva ndiye anapaswa kuwapisha waenda kwa miguu pindi anapokaribia popote penye alama hiyo (Zebra crossing)?.Na kutokufanya hivyo ni kinyume na utaratibu/Sheria za barabarani?.

Unakuta waenda kwa miguu wamesimama wengi pembezoni mwa barabara sehemu penye Zebra crossing lakini madereva wetu ndio kwanza hawataki kuwapisha waenda kwa miguu na kupita kwa spidi isiyo ya kawaida,Huwa najiuliza hizi shule za Driving wanafundishwa nini?.

Wewe Francis Da Don,Unapaswa ufahamu kuwa ni Dereva wa gari anayepaswa kusimama na kuwapisha waenda kwa miguu popote penye alama ya pundamlia na siyo waenda kwa miguu kusubiri.
 
Dahafrazeril,
Haswaaa.., wavuka kwa miguu wengi huvuka sehemu zisizo na zebra, tena kama wimbi la nyumbu. Nasisitiza waende shule za udereva wa miguu na wapewe leseni
 
Kuna wanaovuka wakati taa za kijani wameruhusu magari.... walipishwe tu

Kuna wanaovuka kwenye round about.... walipishwe tu

Kuna wanaovuka kwa kufuata mkumbo ... walioishwe tu

Kuna wanaovuka huku wapo busy na simu....walipishwe tu

Nitarudi
 
Back
Top Bottom