Sitaisahau awamu fulani katika nchi ya Kufikirika.

HORSE POWER

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
2,067
1,386
Ni katika nchi ya KUFIKIRIKA.Ni katika awamu hiyo ambapo ilikua 'msimu wa mavuno' kwa manyang'au na mapaka shume wa kila namna.Walikula bila ya kunawa na walisaza bila ya kufuta midomo.WALIRARUA vibaya rasilimali za nchi na kwa makucha ya chuma na KUTAFUNA fedha za umma kwa meno yenye sumu kali inayoua haraka na taratibu.Hapakua na wa kuwahoji wala kuwatisha.Hawakua na huruma wala kujali maskini walio wengi.
Vyombo vya utoaji haki 'vilipigwa' kiharusi na kusalimu amri kwa mtandao huo wa kimafia.
Ni katika awamu hiyo wananchi walishuhudia 'mipasho' mjengoni na mnyukano wa kimakundi badala ya maslahi ya nchi.Nchi ilipoteza uelekeo lakini wananchi walitiwa moyo na wasomi wasaliti kuwa UCHUMI UNAPAA .Na wanasiasa wachovu nao walijiunga kambi ya usaliti na kuitikia 'wimbo' unaoimbwa na watawala wababaishaji kwamba nchi hiyo ni MASKINI katikati ya utajiri mkubwa wa rasimali.
Sijui hali ipoje nchii hiyo kwa sasa maana nasikia wamepata Rais mpya mwenye uthubutu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom