Sitaingilia uhuru wa mahakama-kikwete

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
kwa kuwa JK alitupiga wananchi kijembe kwamba ni wasahaulifu sana,basi ni vyema tukajikumbusha waraka huu na kulinganisha na mwenendo wa kesi mbalimbali za ubunge nchini.

SITAINGILIA UHURU WA MAHAKAMA-KIKWETE· Aahidi kuongeza idadi ya majaji wa mahakama ya rufaa

Na Mwandishi Maalum

14/2/2006
Ikulu


Rais Jakaya Kikwete amesisitiza kwamba, serikali ya awamu ya nne itajitahidi kuheshimu utawala wa sheria na kutoingilia uhuru wa mahakama. Ametoa ahadi hiyo jana (Jumatatu) wakati alipokuwa akizungumza na uongozi wa mahakama ya Tanzania, katika mfululizo wake wa kuzitembelea wizara na idara mbalimbali za serikali. “Narudia tena, kama nilivyozungumza wakati nalihutubia Bunge, serikali ya awamu ya nne itajitahidi kuheshimu utawala wa sheria na kutoingilia uhuru wa mahakama, mimi sitafanya hivyo na nitahakikisha kuwa na wenzagu hawafanyi hiyo”. Akasema Rais. Akakitaka chombo hicho kinachosimamia utoaji wa haki, kuwa huru kabisa katika kutimiza majukumu yake. Na kuongeza kuwa uhuru huo lazima uhakikishe kuwa raia wanapata haki zao kwa wakati na kwa usawa. Hata hivyo Rais alisema kuwa pamoja na kuwa mahakama iko huru katika utekelezaji wa majukumu yake, lakini uwezeshaji uko ndani ya serikali. “Ninachoweza kuwaahidi ni kwamba tutatimiza wajibu wetu ili muweze kutekekeleza wajibu wenu. Na katika uwezeshaji huo ni pamoja na uteuzi wa majaji wa mahakama ya rufaa mapema iwezekanavyo”, akasema Rais. Akasema kuwa serikali pia itajitahidi kuongeza bajeti ya mahakama pale hali ya mapato ikatakaporidhisha. Ikiwa ni pamoja na kuongeza watumishi wa idara nyingine, majengo na vitendea kazi vya kisasa. Rais akatumia nafasi hiyo kuipongeza mahakam ya Tanzania kwakufanya kazi nzuri licha ya mazingira magumu ya kufanyia kazi. Akimkaribisha Rais kuzungumza na uongozi wa mahakama ya Tanzania, Jaji Mkuu, Mhe. Jaji Samatta alisema kuwa baadhi ya changamoto zinazoikabili mahakama ni pamoja na upungufu wa majaji wa mahakama ya rufaa. Akasema kuwa hivi sasa wapo majaji tisa tu katika mahakama hiyo ya rufaa ambayo ndiyo chombo cha juu kabisa. Idadi ya majaji inayotakiwa ili waweze kukabiliana na wingi wa kesi za rufa zinazofunguliwa katika mahakama hiyo ni 15. Jaji Mkuu alisema kuwa hivi sasa majaji hao tisa wa mahakama ya rufaa waliopo wanashughulikia kesi kati ya 400 na 500 na kwamba kalenda ya usikilizaji wa kesi hizo imejaa hadi mwezi Agosti hali inayopelekea kesi mpya kupangiwa mwezi Septemba na kuendelea. Akielezea zaidi kuhusu upungufu wa watendaji katika mahakama ya Tanzania, Jaji Mkuu alisema, majaji wa mahakama kuu wapo 37 wakati idadi halisi inayotakiwa na 60. Mahakimu wakazi wapo 198 wanaotakiwa ni 398 na mahakimu wa mahakama za mwanzo wapo 698 wanaotakiwa ni 1105. Aidha Jaji Mkuu alibainisha kuwa bajeti halisi inayotakiwa kukidhi mahitaji ya mahakama ya Tanzania ni shilingi bilioni 62 kwa mwaka. Hivi sasa idara hiyo inapata shilingi bilioni 30.9 Kuhusu vita dhidi ya rushwa miongoni mwa watumishi, Jaji Mkuu alisema kuwa vita dhidi ya rushwa ndani ya mahakama ya Tanzania imekuwa ni ya kudumu. Akaeleza kuwa Tume ya Utumishi wa Mhakama zimeendelea kuwastaafisha kazi mahakimu wote walioonekana kwamba walijihusisha na vitendo vya rushwa hata kama waliachiwa mahakamani kwa kukosekana ushahidi katika viwango vya kisheria. Katika mwaka 2004/2005 mahakimu wa walaya watano na mahakimu wa mahakama za mwanzo nane walistaafishwa kazi kwa makosa ya kinidhamu na kujihusisha na vitendo vya rushwa. Katika mazungumzo hayo, uongozi huo wa mahakama uliomba serikali kuangalia uwezekano wa kudhamini vipindi vya elimu ya uraia vinavyohusu kazi za mahakama ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kuzifahamu vema haki zao na namna ya kuzitafuta. Uongozi huo ulisema kuwa wananchi walio wengi hawana ufahamu na shughuli za mahakama, hali inayowafanya washindwe kutafuta haki zao. Aidha walipendekeza kuwa vianzishwe vipindi katika shule za msingi na sekondari ili kupanua uelewa wa wanafunzi katika masuala yanayohusu mahakama. Mwisho.
 
Back
Top Bottom