Sitagombea tena, hili Bunge langu la mwisho - Sitta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitagombea tena, hili Bunge langu la mwisho - Sitta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sokomoko, Nov 16, 2010.

 1. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Spika wa Tatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel John Tegeza Sitta amesema kuwa utumishi wake bungeni umetosha, hivyo ni wakati wake kustaafu. Amesema anastaafu bunge lakini siyo siasa, hivyo bunge la sasa atalitumia kunoa uwezo wa vijana kabla ya kuachana na siasa za bunge 2015.

  Akizungumza bungeni Jumatano iliyopita, kabla ya Kamati Kuu ya CCM (CC) kuengua jina lake katika mbio za kuwania Uspika, Sitta alisema kuwa hatarajii kustaafu kwa sababu anaweza kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu kwenye chama chake.

  Awali, siku hiyo Sitta alimpongeza Mbunge wa Viti Maalum CCM (Vyama vya Wafanyakazi), Zainab Kawawa kwa ushindi aliopata na kumuahidi kumjenga kiuwezo kabla ya kuachia bunge mwaka 2015.

  “Hongera sana, umerudi tuwajenge ili mwaka 2015 tutakapowaacha, muwe tayari na uzoefu,” alisema Sitta akizungumza na Zainab.

  Baada ya kunasa kauli hiyo, mwandishi wetu alimuuliza Mbunge huyo wa Urambo Mashariki kama hilo ni tamko rasmi au limetoka tu bila kudhamiria ambapo alijibu: “Ni tamko rasmi, sitagombea tena na hili ni bunge langu la mwisho

  Sitta alisema kuwa anafikiri kuwa utumishi wake ndani ya bunge umetosha, kwahiyo anataka kukuza vijana.

  Wakati akizungumza hayo Jumatano asubuhi kwenye viunga wa bunge, jioni ya siku hiyo, CC ilitangaza kumuengua Sitta katika mbio za kuwania uspika na kubakiza majina ya wanawake watatu ambapo mwisho Anna Makinda alishinda.   
 2. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Anastaafi Bunge siyo SIASA, meaning URAIS bado anautaka; pengine kauli kama hizi zitakuwa zimewatisha wenziwe ndio maana wakamweka pembeni kuwania USPIKA
   
 3. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nafikiri anajiandaa kugombea urais 2015!!
   
 4. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,495
  Likes Received: 2,739
  Trophy Points: 280

  Wait 2015, atakuja na ule msemo "Wameniomba hivyo nimekubali"
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Nov 16, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Ahamie CHADEMA 2015, na uspika ataukwaa, hakuna mizengwe, hakuna akina Lowassa ndani ya CHADEMA.
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  by 2015 atakuwa hana mvuto tena
   
 7. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #7
  Nov 16, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kwani sasa hivi Mh. Sitta ana mvuto????
   
 8. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #8
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni wazo lenye busara kama atautekeleza, kwani kusubiri kung`atuliwa kuna punguza heshima kwa hawa wazee.
  Big up sita, washauri na wazee wenzako waweze kukubali kuachia nafasi kwa vijana. Nchi hii sasa hivi inahitaji vijana wenye mawazo ya kileo yaliyo jaa uwazi na mtazamo wa kimaendeleo zaidi .
   
 9. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #9
  Nov 16, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwani Chadema ndio chama pekee? Kama mimi ni Sitta na imenibidi kuhama CCM nitahamia NCCR au chama kisichokuwa na umaarufu.... Sote tunajua matatizo ya vyama vikubwa vya upinzani.
   
 10. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #10
  Nov 16, 2010
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sitta kama anataka urais aondoke CCM tofauti na hilo ampigie kampeni mtu mwingine na kufuatilia nyendo zote za mafisadi.
   
 11. The Spit

  The Spit JF-Expert Member

  #11
  Nov 16, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Haha hulali hupati usingizi sababu ya CHADEMA..Maneno yako hapo juu ushahidi tosha...


  PEOPLE'S.......................................P....................WAAAAAAAA
   
 12. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #12
  Nov 16, 2010
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,541
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  wazo zuri wapishe vijana sasa
   
 13. October

  October JF-Expert Member

  #13
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wajanja watatoa matamko haraka maana wanaona upepo unakokwenda mambo si mazuri kwa CCM. Wamesoma alama za nyakati na wanajua wamechokwa na wananchi.

  Amefanya la maana sana, ameona ni afadhali ajitoe mwenyewe kuliko kuja kuumbuloiwa na wananchi katika sanduku la Kura kama kina Mramba na Chenge n.k.

  Tunasubiri na wengine wajitoe...
   
 14. k

  kambipopote Senior Member

  #14
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 114
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ccm hawawezi kumpa nafasi amekikosti chama hicho, hivyo tunamkaribisha chadema, huku hatuna vinyongo, visasi, majungu, umafia na mengineyo ya gizani. huku tunaangalia uzalendo, uadilifu, uwajibikaji, uwazi na ujasiri, mengine ongezeeni wakuu:israel:
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Nov 16, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Alama za nyakati hizo. Anajua hawezi kupambana na pipozi pawa tena. Ni muongo tu. Aliwadanganya wananchi wake kuwa elimu ya bure haiwezekani wakati binafsi anatoa elimu ya bure kwa watoto 200!!!??&%#@$% Sasa anajua ataulizwa mengi anajiwahi tu kuwaachia Chadema jimbo. Hahahahahahaha
   
 16. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #16
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,986
  Likes Received: 3,735
  Trophy Points: 280
  This (in red) is nice......what an admission from someone draped in yellow and green!!
   
 17. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #17
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,717
  Likes Received: 1,627
  Trophy Points: 280
  sitta kama Ben Nyitanyau au Rais Puttin maana anaachana na kile anaanzisha kipya sasa anamaanisha anautaka Urais, lakini kaisha poteza maana angewawai kabla zengwe hili lisingempata.
   
 18. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #18
  Nov 16, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  hapa hakuna haja ya kumpongeza ,jamani huyu jamaa amekuwa kiongozi tangu Nyerere,Mwisnyi,Mkapa,Kikwete..hawachoki?miaka mitano tena bado kweli atakuwa na nguvu za kuongoza? aende akapumzike bwana...
   
 19. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #19
  Nov 16, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwangu mimi chama hakina nafasi naangalia mtu maana hata kura yangu sijapikia chama kimoja!
   
 20. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #20
  Nov 16, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ni kweli hukupikia chama kimoja lakini ulipigia chama kimoja cha CCM
   
Loading...