Ng'wanapagi
JF-Expert Member
- Sep 18, 2013
- 9,125
- 8,627
Nimezaliwa na kukulia huko hata nikifa naamini taletwa kuzikwa huko. Huko ndiko ndugu, marafiki na watoto wangu wanaishi.
Naifahamu Bulyanhulu hata kabla ya kuja hao whites, nawakumbuka marafiki zangu waliofukiwa kwenye mashimo wakijificha ili wazungu waliolindwa na polisi wetu chini ya amri ya Mkapa wachukue sehemu hiyo walifukiwa ili kuwapisha wawekezaji hao kutoka mikononi mwa wachimbaji wadogo (wachimaji wadogo waliitwa wachimbaji haramu).
Nakukumbuka Hamisi Mgunga kama mmoja wa rafiki zangu waliofia kwenye hilo sakata. Tangu 1996 hadi leo 2020 hakuna barabara ya lami wala maji ya uhakika. Wana CCM kulisema hili mbele yao utaitwa si mzalendo na huungi mkono juhudi za mtu wa kwetu!
Kule Chato tangu mtu wetu akiwa ujenzi alipapendelea kwa barabara za lami, leo hii kuna taa za barabarani, kuna uwanja mkubwa wa ndege, kuna jengo la mahakama la kisasa kuliko hata lile la mkoa wa Geita, kuna maandalizi ya kujengwa hospital ya rufaa na sasa kuna mbuga ya wanyama (artificial game) wanyama wanahamishwa kupelekwa huko. Kutoka Nyakumbu Geita hadi Kakola (kitovu cha dhahabu) hakuna lami!
Kutoka Kakola hadi Kahama hakuna lami! Naamini hana habari na Bulyanhulu kwa sababu wanaotakiwa kumwambia wanamuogopa na ukimtajia Bulyanhulu moja kwa moja atawawazia mabeberu ACACIA ambao wameshaondoka tayari.
Sent using Jamii Forums mobile app

Inauma ila ipo siku
Sent using Jamii Forums mobile app