Kati ya mambo ambayo yamenichafua roho katika mwezi huu ni haya mambo ya uchaguzi. Awali sikutaka hata kwenda kupiga kura nikiamini kuwa kufanya hivyo ni kupoteza muda wangu, sijui ni roho gani iliniingia ila nilipiga kura bila usumbufu kwani utaratibu wa mwaka huu wa kupiga kura ulikuwa hauna usumbufu kama nilivyodhania, matumaini makubwa yalinijaa moyoni kuwa kama utaratibu huu ndiyo utakuwa mwanzo mwisho basi niliamini kuwa kura yangu itakuwa fimbo na rungu la kuwaponda wagombea nilioamini kuwa hawafai kuniongoza. Sayasi ya kuchakachua ilikuwa kubwa kwani naamini zoezi zima la kuamka mapema na kwenda kupiga kura lilikuwa halina maana kwani nilichoambulia ni kuvunjwa moyo achilia mbali kukatishwa tamaa na mbinu chafu zilizokuwepo kuwapata washindi.
Kwa kuwa tumezoea kuonewa sikuona haja ya kuendelea kulaumu na kujilaumu nikaona nikubali yaishe tugange ya jayo.
Hili la kutafuta spika tokea mzee makamba atangaze kuchukuwa fomu za kugombea nafasi ya spika, mwonekano wake na hamasa yake mzee makamba iliniwezesha kutabiri kuwa lipo jambo lingine linakuja kunivunja moyo. Kwa ufupi kwa mwezi huu na uliopita kwa watu wengi wanaopenda kupigania haki, umekuwa ni mwezi wao. Kukosekana spika kama samweli 6 katika bunge hili lenye sura ngeni na wageni wengi naamini ni tatizo lingine na janga ambalo sijajua mwokozi atakuwa nani.
Inawezekana kweli Sita alikuwa na mapungufu fulani kama binadamu yeyote, lakini namna walivyomuengua sioni kama wamemtendea haki siamini kuwa sita hajafanya lolote la maana kwa nchi hii, isitoshe sita hakuanzia kutumikia taifa hili jana au juzi, ni mkongwe wa siasa za nchi hii toka TANU ya mwalimu nyerere hadi leo, iweje leo hata kwenye tatu bora hayumo? Nionavyo mimi hii ni hatari nyingine kwa chama, huu ni mgawanyiko na huku ni kuanza kupoteana njiani.
Kukosekana kwa mshikamano ndani ya ccm kunaweza kuwagharimu sana maana inavyoelekea sasa hivi kinachoendelea ni kuwa ukimwaga ugali mwingine anamwaga mchuzi, hii ni hatari na ni mwanzo wa mparaganyiko ambao tiba yake inaweza isipatikane. mfano mzuri ni huko mwanza ambako nimesikia kuna viongozi wa chama waliosimamishwa kwa kukihujumu chama. Haya ni matokeo ya kukosa mshikamano na umoja, staili hii ndiyo itaendelea ndani ya chama kwani watu wataanza kutakiana mabaya wenyewe kwa wenyewe, ikifikia hapo huenda ndiyo mwisho kwani dalili ya mwaka huu ya kushindwa ni dalili ya hatari ambayo bila kujirudi na kuwa wamoja pengine wanachama waanze kuweka matanga kwani yaliyotokea nchi jirani kuanguka vyama vilivyokuwa na nguvu yanatujongelea
Nilisikia msemo kuwa "wote tunajenga nyumba yetu kwanini tugombee fito?" msemo huu naona uko katoka nadharia na ukweli wake hauwekwi katika vitendo. Ni kweli wote tunajenga, shida ni pale baadhi ya wachache wanapojimilikisha hiyo nyumba huku wakijua wazi kuwa nyumba hiyo ni yetu wote. hiyo ni sawa na kuchangia kununua unga ila ugali wale wengine.
naamini mzee sita ameghadhibishwa sana, amedhalilishwa sana na amevunjiwa heshima sana ina nataka kwanza ni mpongeze kuwa tulimkubali na kwamba ''vita vya siasa amepigana, haki ameitetea, asivunjike moyo apige vita vizuri vya siasa ili afikie mwisho mwema" mapambano yaendelee