Sita: Usivunjike moyo: umepigana kiume, haki umeitetea sasa piga mwendo.

Anold

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,456
612
Kati ya mambo ambayo yamenichafua roho katika mwezi huu ni haya mambo ya uchaguzi. Awali sikutaka hata kwenda kupiga kura nikiamini kuwa kufanya hivyo ni kupoteza muda wangu, sijui ni roho gani iliniingia ila nilipiga kura bila usumbufu kwani utaratibu wa mwaka huu wa kupiga kura ulikuwa hauna usumbufu kama nilivyodhania, matumaini makubwa yalinijaa moyoni kuwa kama utaratibu huu ndiyo utakuwa mwanzo mwisho basi niliamini kuwa kura yangu itakuwa fimbo na rungu la kuwaponda wagombea nilioamini kuwa hawafai kuniongoza. Sayasi ya kuchakachua ilikuwa kubwa kwani naamini zoezi zima la kuamka mapema na kwenda kupiga kura lilikuwa halina maana kwani nilichoambulia ni kuvunjwa moyo achilia mbali kukatishwa tamaa na mbinu chafu zilizokuwepo kuwapata washindi.

Kwa kuwa tumezoea kuonewa sikuona haja ya kuendelea kulaumu na kujilaumu nikaona nikubali yaishe tugange ya jayo.

Hili la kutafuta spika tokea mzee makamba atangaze kuchukuwa fomu za kugombea nafasi ya spika, mwonekano wake na hamasa yake mzee makamba iliniwezesha kutabiri kuwa lipo jambo lingine linakuja kunivunja moyo. Kwa ufupi kwa mwezi huu na uliopita kwa watu wengi wanaopenda kupigania haki, umekuwa ni mwezi wao. Kukosekana spika kama samweli 6 katika bunge hili lenye sura ngeni na wageni wengi naamini ni tatizo lingine na janga ambalo sijajua mwokozi atakuwa nani.

Inawezekana kweli Sita alikuwa na mapungufu fulani kama binadamu yeyote, lakini namna walivyomuengua sioni kama wamemtendea haki siamini kuwa sita hajafanya lolote la maana kwa nchi hii, isitoshe sita hakuanzia kutumikia taifa hili jana au juzi, ni mkongwe wa siasa za nchi hii toka TANU ya mwalimu nyerere hadi leo, iweje leo hata kwenye tatu bora hayumo? Nionavyo mimi hii ni hatari nyingine kwa chama, huu ni mgawanyiko na huku ni kuanza kupoteana njiani.

Kukosekana kwa mshikamano ndani ya ccm kunaweza kuwagharimu sana maana inavyoelekea sasa hivi kinachoendelea ni kuwa ukimwaga ugali mwingine anamwaga mchuzi, hii ni hatari na ni mwanzo wa mparaganyiko ambao tiba yake inaweza isipatikane. mfano mzuri ni huko mwanza ambako nimesikia kuna viongozi wa chama waliosimamishwa kwa kukihujumu chama. Haya ni matokeo ya kukosa mshikamano na umoja, staili hii ndiyo itaendelea ndani ya chama kwani watu wataanza kutakiana mabaya wenyewe kwa wenyewe, ikifikia hapo huenda ndiyo mwisho kwani dalili ya mwaka huu ya kushindwa ni dalili ya hatari ambayo bila kujirudi na kuwa wamoja pengine wanachama waanze kuweka matanga kwani yaliyotokea nchi jirani kuanguka vyama vilivyokuwa na nguvu yanatujongelea

Nilisikia msemo kuwa "wote tunajenga nyumba yetu kwanini tugombee fito?" msemo huu naona uko katoka nadharia na ukweli wake hauwekwi katika vitendo. Ni kweli wote tunajenga, shida ni pale baadhi ya wachache wanapojimilikisha hiyo nyumba huku wakijua wazi kuwa nyumba hiyo ni yetu wote. hiyo ni sawa na kuchangia kununua unga ila ugali wale wengine.

naamini mzee sita ameghadhibishwa sana, amedhalilishwa sana na amevunjiwa heshima sana ina nataka kwanza ni mpongeze kuwa tulimkubali na kwamba ''vita vya siasa amepigana, haki ameitetea, asivunjike moyo apige vita vizuri vya siasa ili afikie mwisho mwema" mapambano yaendelee
 
wakusoma

JF-Expert Member
Feb 25, 2008
1,081
1,034
ni bora tukaongozwa na kuku kuliko serikali ya ccm.uwezo wa mzee makamba kupambamabnua mambo ni sawa a mtoto wa pre form one tena wa shule ya kata.maana hata pre form one wa saint marry anamzidi.nimechukia kuliko maelezo kumtoa mzee sitta.kwangu mimi huyu ni zaidi ya kiongozi.
 
Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,518
6,090
unajua Sitta anachukulia mambo very traditional.anasahau kuwa ametengeneza maadui wengi sana wakati wa mambo ya richmond sasa anakuja na mbinu za zamani wakati watu wamemkamia lazima upigwe chini.....hivi hakuwa na kamati ya kuchakachua matokeo..teh teh mzee sitta pole bana nakumbuka ulivo msimamisha Zitto pili nakumbuka siku umemfukuza Cheyo bungeni kwa jazba...hahaaa na wewe zamu yako inakuja uwe unachangia sasa
 
Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,518
6,090
ni bora tukaongozwa na kuku kuliko serikali ya ccm.uwezo wa mzee makamba kupambamabnua mambo ni sawa a mtoto wa pre form one tena wa shule ya kata.maana hata pre form one wa saint marry anamzidi.nimechukia kuliko maelezo kumtoa mzee sitta.kwangu mimi huyu ni zaidi ya kiongozi.

simpendi Sitta kwa kuwa alikuwa na ubabe hasa inapokuja watu wa opposition wanaongea...mwache aende zake bana
 
PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,208
8,683
simpendi Sitta kwa kuwa alikuwa na ubabe hasa inapokuja watu wa opposition wanaongea...mwache aende zake bana
Alikuwa na pande 2 kama binadamu yeyote!
Upande wa 2 mbona huuongelei?
Be fair broda, hukumu tu haifai, hata marehemu anasifiwa!
 
Double X

Senior Member
Nov 4, 2010
184
3
Sitta nilikuwa namkubali sana lakini tokea alipoufunga mjadala wa richmond KIHUNI namna ile nilianza kumwona hafai.halafu huyu bw sio mzalendo na hana uchungu na watz, anawezaje akaacha wabunge akiwemo yeye mwenyewe walipwe posho ya mafuta kwa bei ya tsh 2500 kwa lita??hata elfu 2 mafuta hayajafika, bado posho kubwakubwa wanazopewa, safi tu alivyopigwa chini, aanze na yeye kunyoosha kidole kuchangia.
 
ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,161
1,427
Apige mwendo kwenda wapi wakati kashafungwa speed Governor miguuni?
 
Saharavoice

JF-Expert Member
Aug 30, 2007
3,515
1,812
Sitta nilikuwa namkubali sana lakini tokea alipoufunga mjadala wa richmond KIHUNI namna ile nilianza kumwona hafai.halafu huyu bw sio mzalendo na hana uchungu na watz, anawezaje akaacha wabunge akiwemo yeye mwenyewe walipwe posho ya mafuta kwa bei ya tsh 2500 kwa lita??hata elfu 2 mafuta hayajafika, bado posho kubwakubwa wanazopewa, safi tu alivyopigwa chini, aanze na yeye kunyoosha kidole kuchangia.

Kulikuwa na outside pressure kubwa ktk Richmond, alihitaji ujasiri mkubwa kukwepa kuufunga, unfortunately alishindwa.

kwa asilimia kubwa alifanya vizuri kuliko alivyofanya vibaya. Uwepo wake kama Spika kulifanya upinzani kusikika sana na matunda yake tumeyaona kupitia Dr. Slaa. Hofu ni je, ajaye atawapa nafasi ya kutamba kama ilivyokuwa bunge lililopita?
 
Tata

JF-Expert Member
Dec 3, 2009
5,800
2,713
Kati ya mambo ambayo yamenichafua roho katika mwezi huu ni haya mambo ya uchaguzi. Awali sikutaka hata kwenda kupiga kura nikiamini kuwa kufanya hivyo ni kupoteza muda wangu, sijui ni roho gani iliniingia ila nilipiga kura bila usumbufu kwani utaratibu wa mwaka huu wa kupiga kura ulikuwa hauna usumbufu kama nilivyodhania, matumaini makubwa yalinijaa moyoni kuwa kama utaratibu huu ndiyo utakuwa mwanzo mwisho basi niliamini kuwa kura yangu itakuwa fimbo na rungu la kuwaponda wagombea nilioamini kuwa hawafai kuniongoza. Sayasi ya kuchakachua ilikuwa kubwa kwani naamini zoezi zima la kuamka mapema na kwenda kupiga kura lilikuwa halina maana kwani nilichoambulia ni kuvunjwa moyo achilia mbali kukatishwa tamaa na mbinu chafu zilizokuwepo kuwapata washindi.

Kwa kuwa tumezoea kuonewa sikuona haja ya kuendelea kulaumu na kujilaumu nikaona nikubali yaishe tugange ya jayo.

Hili la kutafuta spika tokea mzee makamba atangaze kuchukuwa fomu za kugombea nafasi ya spika, mwonekano wake na hamasa yake mzee makamba iliniwezesha kutabiri kuwa lipo jambo lingine linakuja kunivunja moyo. Kwa ufupi kwa mwezi huu na uliopita kwa watu wengi wanaopenda kupigania haki, umekuwa ni mwezi wao. Kukosekana spika kama samweli 6 katika bunge hili lenye sura ngeni na wageni wengi naamini ni tatizo lingine na janga ambalo sijajua mwokozi atakuwa nani.

Inawezekana kweli Sita alikuwa na mapungufu fulani kama binadamu yeyote, lakini namna walivyomuengua sioni kama wamemtendea haki siamini kuwa sita hajafanya lolote la maana kwa nchi hii, isitoshe sita hakuanzia kutumikia taifa hili jana au juzi, ni mkongwe wa siasa za nchi hii toka TANU ya mwalimu nyerere hadi leo, iweje leo hata kwenye tatu bora hayumo? Nionavyo mimi hii ni hatari nyingine kwa chama, huu ni mgawanyiko na huku ni kuanza kupoteana njiani.

Kukosekana kwa mshikamano ndani ya ccm kunaweza kuwagharimu sana maana inavyoelekea sasa hivi kinachoendelea ni kuwa ukimwaga ugali mwingine anamwaga mchuzi, hii ni hatari na ni mwanzo wa mparaganyiko ambao tiba yake inaweza isipatikane. mfano mzuri ni huko mwanza ambako nimesikia kuna viongozi wa chama waliosimamishwa kwa kukihujumu chama. Haya ni matokeo ya kukosa mshikamano na umoja, staili hii ndiyo itaendelea ndani ya chama kwani watu wataanza kutakiana mabaya wenyewe kwa wenyewe, ikifikia hapo huenda ndiyo mwisho kwani dalili ya mwaka huu ya kushindwa ni dalili ya hatari ambayo bila kujirudi na kuwa wamoja pengine wanachama waanze kuweka matanga kwani yaliyotokea nchi jirani kuanguka vyama vilivyokuwa na nguvu yanatujongelea

Nilisikia msemo kuwa "wote tunajenga nyumba yetu kwanini tugombee fito?" msemo huu naona uko katoka nadharia na ukweli wake hauwekwi katika vitendo. Ni kweli wote tunajenga, shida ni pale baadhi ya wachache wanapojimilikisha hiyo nyumba huku wakijua wazi kuwa nyumba hiyo ni yetu wote. hiyo ni sawa na kuchangia kununua unga ila ugali wale wengine.

naamini mzee sita ameghadhibishwa sana, amedhalilishwa sana na amevunjiwa heshima sana ina nataka kwanza ni mpongeze kuwa tulimkubali na kwamba ''vita vya siasa amepigana, haki ameitetea, asivunjike moyo apige vita vizuri vya siasa ili afikie mwisho mwema" mapambano yaendelee

Tatizo lako sasa ni nini hasa?
Je ni Sitta kuondolewa kwenye uchaguzi wa uspika?
Je ni chama cha mapinduzi kuelekea kusambaratika?
Je ni kukosekana mshikamano na umoja ndani ya chama cha mapinduzi?

Hivi watanzania ni lini tutajua kuwa tatizo letu siyo mtu mmoja mmoja bali ni mfumo wa kifisadi ulioasisiwa na kulelewa na CCM? CCM hii ya leo siyo ile iliyoasisiwa na Mwl. Nyerere ya siasa ya ujamaa na kujitegemea.

Chama cha CCM cha Nyerere kililenga kupindua hali ya maisha ya wananchi kuwa nzuri zaidi na kiliainisha maadui kinachopambana nao yaani ujinga, maradhi na umaskini. Hiki ni chama cha kupindua ukweli kuwa uongo. Hakina dira wala mwelekeo kwa sababu kilishayatosa mawazo ya muasisi wa chama. Kwa sasa kinaishi kama kinyonga na kinasubiri dira na mwelekeo kutoka kwa mashirika ya kibeberu ya nchi za magharibi yaani (IMF na World Bank) na nchi wafadhili. Hakiamini tena katika kujitegema bali katika kuhemea vibaba nje ya nchi.

Sitta alikengeuka kwa kudhani kuwa anaweza kubadili mfumo akiwa ndani. Hili kwa ufupi haliwezekani kwa CCM kwani kinaendeshwa na genge la mafisadi ambao kwao kitu chenye maana zaidi ni maslahi binafsi. Watanzania tuamke sasa tufungue macho hii CCM ya sasa imeshachakachuliwa na wajanja siyo ile tuliyokuwa tunaifahamu siku zote hii .
 
The Good One

Member
Oct 31, 2010
12
0
'SAMWEL SITTA OUT' :tape:! HII NI ISHARA 'CHAMA CHA ZAMANI' KINAELEKEA KWENYE ANGUKO KUU :rip:! TUMWOMBE MUNGU ATUPE MABADILIKO YA KWELI 2015 TUONDOKANE NA VIONGOZI WANAOWEKANA , KUJILIMBIKIZIA MALI, USULTAN WA KURITHISHANA MADARAKA, WANAOLINDANA, WABINAFISI, WASIO NA CHEMBE YA HURUMA KWA MASIKINI WA NCHI HII, WENYE TAMAA YA MADARAKA, WANAOUZA KILA WANACHOWEZA KWAAJILI YA MASLAHI BINAFSI. EEH MWENYEZI MUNGU TUNAOMBA UWAFUMBUE MACHO MASIKINI WA NCHI AMBAO HAWANA UMASIKINI WA MALI BALI ULE UMASIKINI HATARI WA FIKRA WAWAKATAE WATU HAWA 2015! CHAMA CHA ZAMANI KITAANGUKA KAMA MNARA WA BABELI! CHANGES ARE INEVITABLE, LETS JOIN OUR FORCES AND MAKE THE TRUE CHANGES IN 2015. :smile-big::smile:
 
Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
47,178
60,683
kati ya mambo ambayo yamenichafua roho katika mwezi huu ni haya mambo ya uchaguzi. Awali sikutaka hata kwenda kupiga kura nikiamini kuwa kufanya hivyo ni kupoteza muda wangu, sijui ni roho gani iliniingia ila nilipiga kura bila usumbufu kwani utaratibu wa mwaka huu wa kupiga kura ulikuwa hauna usumbufu kama nilivyodhania, matumaini makubwa yalinijaa moyoni kuwa kama utaratibu huu ndiyo utakuwa mwanzo mwisho basi niliamini kuwa kura yangu itakuwa fimbo na rungu la kuwaponda wagombea nilioamini kuwa hawafai kuniongoza. Sayasi ya kuchakachua ilikuwa kubwa kwani naamini zoezi zima la kuamka mapema na kwenda kupiga kura lilikuwa halina maana kwani nilichoambulia ni kuvunjwa moyo achilia mbali kukatishwa tamaa na mbinu chafu zilizokuwepo kuwapata washindi.

Kwa kuwa tumezoea kuonewa sikuona haja ya kuendelea kulaumu na kujilaumu nikaona nikubali yaishe tugange ya jayo.

Hili la kutafuta spika tokea mzee makamba atangaze kuchukuwa fomu za kugombea nafasi ya spika, mwonekano wake na hamasa yake mzee makamba iliniwezesha kutabiri kuwa lipo jambo lingine linakuja kunivunja moyo. Kwa ufupi kwa mwezi huu na uliopita kwa watu wengi wanaopenda kupigania haki, umekuwa ni mwezi wao. Kukosekana spika kama samweli 6 katika bunge hili lenye sura ngeni na wageni wengi naamini ni tatizo lingine na janga ambalo sijajua mwokozi atakuwa nani.

Inawezekana kweli sita alikuwa na mapungufu fulani kama binadamu yeyote, lakini namna walivyomuengua sioni kama wamemtendea haki siamini kuwa sita hajafanya lolote la maana kwa nchi hii, isitoshe sita hakuanzia kutumikia taifa hili jana au juzi, ni mkongwe wa siasa za nchi hii toka tanu ya mwalimu nyerere hadi leo, iweje leo hata kwenye tatu bora hayumo? Nionavyo mimi hii ni hatari nyingine kwa chama, huu ni mgawanyiko na huku ni kuanza kupoteana njiani.

Kukosekana kwa mshikamano ndani ya ccm kunaweza kuwagharimu sana maana inavyoelekea sasa hivi kinachoendelea ni kuwa ukimwaga ugali mwingine anamwaga mchuzi, hii ni hatari na ni mwanzo wa mparaganyiko ambao tiba yake inaweza isipatikane. Mfano mzuri ni huko mwanza ambako nimesikia kuna viongozi wa chama waliosimamishwa kwa kukihujumu chama. Haya ni matokeo ya kukosa mshikamano na umoja, staili hii ndiyo itaendelea ndani ya chama kwani watu wataanza kutakiana mabaya wenyewe kwa wenyewe, ikifikia hapo huenda ndiyo mwisho kwani dalili ya mwaka huu ya kushindwa ni dalili ya hatari ambayo bila kujirudi na kuwa wamoja pengine wanachama waanze kuweka matanga kwani yaliyotokea nchi jirani kuanguka vyama vilivyokuwa na nguvu yanatujongelea

nilisikia msemo kuwa "wote tunajenga nyumba yetu kwanini tugombee fito?" msemo huu naona uko katoka nadharia na ukweli wake hauwekwi katika vitendo. Ni kweli wote tunajenga, shida ni pale baadhi ya wachache wanapojimilikisha hiyo nyumba huku wakijua wazi kuwa nyumba hiyo ni yetu wote. Hiyo ni sawa na kuchangia kununua unga ila ugali wale wengine.

Naamini mzee sita ameghadhibishwa sana, amedhalilishwa sana na amevunjiwa heshima sana ina nataka kwanza ni mpongeze kuwa tulimkubali na kwamba ''vita vya siasa amepigana, haki ameitetea, asivunjike moyo apige vita vizuri vya siasa ili afikie mwisho mwema" mapambano yaendelee
labda wadau mimi sina kumbukumbu, kwani si ni huyu ndio aliyetaka kufanya mdahalo na genuin phd holder dr slaa!!? Wakati dr anataka kukomboa nchi na kutoa elimu bure si nin huyuhuyu alisema elimu bure haiwezekani!!?? Sitaki kuona watu wanaomlilia sita hapa, mwenye uchungu nae aende pale lumumba makamba yupo atawapa kadi. Mtu yeyote anaeitakia mema nchi hii, awezi kubaki ccm mpaka leo. Huyo atakuwa analinda maslahi yake tu. Hongera kamati kuu ya ccm, sasa ndio watajuwa mioyo yetu huwa inaumia kiasi gani. Wacha tushehe maumivu.
 
Kumbukumbu zako ni nzuri sana mheshimiwa. Ni huyu bwana aliyedhani kuwa kwa kumshambulia Dr. Slaa angeweza kusafisha jina machoni pa mafisadi wenzake. Kumbuka alijenga ofisi ya gharama kubwa ya mbunge pale Urambo Mashariki akidai kuwa inatakiwa kuwa na hadhi ya uspika wake. Alisahau msimamo wa chama chao wa mwaka 47 kuwa cheo ni dhamana na siyo mali binafsi ya mwenyenacho.
 
Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,151
199
labda wadau mimi sina kumbukumbu, kwani si ni huyu ndio aliyetaka kufanya mdahalo na genuin phd holder dr slaa!!? wakati dr anataka kukomboa nchi na kutoa elimu bure si nin huyuhuyu alisema elimu bure haiwezekani!!?? Sitaki kuona watu wanaomlilia sita hapa, mwenye uchungu nae aende pale lumumba makamba yupo atawapa kadi. Mtu yeyote anaeitakia mema nchi hii, awezi kubaki ccm mpaka leo. Huyo atakuwa analinda maslahi yake tu. Hongera kamati kuu ya ccm, sasa ndio watajuwa mioyo yetu huwa inaumia kiasi gani. Wacha tushehe maumivu.

huo ndio ulikuwa msimao wa chama chake. Ccm wanamtuhumu sitta kwa sababu ya kuwalea na kuwakuza wapinzania kama akina dr slaa mpaka wakakubalika mbele ya macho ya watanzania. Kama hujui hilo inaonekana umeanza kufuatilia siasa za tz kipindi cha uchaguzi.
Samwel sitta ni shujaa alitumia nafasi yake ya uspika kuwaanika mafisadi vilivyo, isipokuwa watanzania ndio tulimwangusha kwa kutokufanya maandamano ya kumuunga mkono na kuipinga ccm na mafisadi wakati ccm ilipokuwa inamshughulikia sita na wabunge wapamabanaji na uifisadi. Hiyo ingeleta hisia kuwa watanzania wapo tayari kukabiliana na mafisadi kwa wingi wao. Kama tutaendelea kuwaachia wabunge mapambano dhidi ya ufisadi tutegemea kuwaona akina sitta wengi zaid wakishughulikiwa.

kwa kifupi sisi watanzania ndio tunawangusha wabunge kwa kutoshiriki katika kupinga vitendo vya ufisadi kwa vitendoa badala yake tunavipinga kwa maneno tu hapa jf kama unavyofanya wewe na magazetini. Sitta alichokuwa anakifanya ni kutumia ibara ya 63 ya katiba inayotama madaraka ya wabunge ni kuisimamia na kiushauri serikali. Sasa kama watanzania wenyewe hawachukui hatua zozote wanapoona wabunge wao wanashughulikiwa ulitaka yeye kama sitta afanye nini cha ziada kama sio kuufunga huo mjadala?

Ccm na mafisadi wamegundua kuwa watanzania hupata elimu ya uraia bungeni ndio maana wameelekeza nguvu zao zote kuzima kasi ya wabunge wa upinzani.

hivyo kabla ya kumnyooshea sitta kidole jiulize binafsi umechangia nini katika mapamano dhidi ya ufisadi? Kwa ujumla wetu tumeshindwa hata kuandamana kuipinga takukuru kwa kumsafisha chenge. Sasa kama wananchi tuko hivyo kwa maana ya kutoonyesha nguvu ya umma; ni kwanini hata hao wabunge wetu wasinyamazishwe huko bungeni?
 
Ndachuwa

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
6,272
4,539
Sitta sasa aungane na kina Kingunge kuchapa usingizi mjengoni kwa muda wa miaka mitano yake ya mwisho maana joto alilopata mweziwe Jumaane Malecela kitamtokea 2015 kama atadiriki kuchua fomu ya kugombe cheo chochote kuanzia udiwani
 
Nyumbu-

JF-Expert Member
May 26, 2009
988
348
huo ndio ulikuwa msimao wa chama chake. Ccm wanamtuhumu sitta kwa sababu ya kuwalea na kuwakuza wapinzania kama akina dr slaa mpaka wakakubalika mbele ya macho ya watanzania. Kama hujui hilo inaonekana umeanza kufuatilia siasa za tz kipindi cha uchaguzi.
Samwel sitta ni shujaa alitumia nafasi yake ya uspika kuwaanika mafisadi vilivyo, isipokuwa watanzania ndio tulimwangusha kwa kutokufanya maandamano ya kumuunga mkono na kuipinga ccm na mafisadi wakati ccm ilipokuwa inamshughulikia sita na wabunge wapamabanaji na uifisadi. Hiyo ingeleta hisia kuwa watanzania wapo tayari kukabiliana na mafisadi kwa wingi wao. Kama tutaendelea kuwaachia wabunge mapambano dhidi ya ufisadi tutegemea kuwaona akina sitta wengi zaid wakishughulikiwa.

kwa kifupi sisi watanzania ndio tunawangusha wabunge kwa kutoshiriki katika kupinga vitendo vya ufisadi kwa vitendoa badala yake tunavipinga kwa maneno tu hapa jf kama unavyofanya wewe na magazetini. Sitta alichokuwa anakifanya ni kutumia ibara ya 63 ya katiba inayotama madaraka ya wabunge ni kuisimamia na kiushauri serikali. Sasa kama watanzania wenyewe hawachukui hatua zozote wanapoona wabunge wao wanashughulikiwa ulitaka yeye kama sitta afanye nini cha ziada kama sio kuufunga huo mjadala?

Ccm na mafisadi wamegundua kuwa watanzania hupata elimu ya uraia bungeni ndio maana wameelekeza nguvu zao zote kuzima kasi ya wabunge wa upinzani.

hivyo kabla ya kumnyooshea sitta kidole jiulize binafsi umechangia nini katika mapamano dhidi ya ufisadi? Kwa ujumla wetu tumeshindwa hata kuandamana kuipinga takukuru kwa kumsafisha chenge. Sasa kama wananchi tuko hivyo kwa maana ya kutoonyesha nguvu ya umma; ni kwanini hata hao wabunge wetu wasinyamazishwe huko bungeni?

You have said it. Nilitaka nikupe thanks 2 lakini ziko limited!
 
Avanti

JF-Expert Member
Aug 24, 2010
1,209
239
anajuta kwa nini alizima ule mjadala wa richmond

Sitta was buying own popularity. Bora abgeenda CCJ aliyoiasisi. Sasa amechelewa, Chenge ana akili sana, kanifurahisha, na najua nia yake haikuwa Uspika hata!
 
bojuka

Senior Member
Sep 9, 2010
128
1
ccm wanajipalia makaa kwa sasa wanapanda lkn watavuna 2015 na ndio utakuwa mwisho wao.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom