Sita na mustakabali wake kisiasa

Paul S.S

JF-Expert Member
Aug 27, 2009
6,402
3,242
Baada ya aliyekuwa spika wa bunge lililopita Mh Sita kukwaa kisiki katika mchakato wa kuwania tena nafasi ya kuliongoza bunge kwa kipindi kingine, mengi yamekuwa yanasemwa juu ya jambo hili.
Ni ukweli usio fichika kuwa Sita pamoja na kuweka maslahi ya chama chake mbele wakati wa uongozi wake, lakini alijitahidi sana kujaribu kuwa fair kwa kuacha bunge uwe uwanja huru kwa watu kutoa michango yao licha ya shinikizo kubwa kutoka chama chake kumtaka awabane vilivyo wapinzani bungeni,

Sote tunakumbuka jinsi alivyotaka kupokwa kadi ya uanachama na kusababisha kuundwa tume ya usuluhisho chini ya mzee Mwinyi.

Ni chini ya uongozi wa sita kama spika ccm ilipitia katika kipindi kigumu cha mpasuko wa chama kati ya wabunge waliojipambanua kuwa wapinganaji wakiongozwa na sita mwenyewe pamoja na wale walio tuhumiwa ufisadi wakiongozwa na lowasa na rostam.

Ni chini ya spika sita tuliona mawaziri wakipelekeshwa na spika kwakutakiwa kutoa maelezo au majibu ya kuridhisha kwa maswali waliyo ulizwa,na wakati mwingine hata alikuwa anamuomba Rais awe mkali kidogo, kitendo ambacho hakikutegemewa wala kufanywa na maspika waliopita,

Ni chini ya spika sita, ililazimu waziri mkuu kujiuzulu kwa kuruhusu mjadala kuendelea na kuunda tume na kusababishwa kuvunjwa kwa baraza la mawaziri,

Mambo hayo kwa ujumla yamenjengea maadui wengi ndani ya chama na serikali, na mbaya zaidi amejanga chuki na watu wanaosadikiwa kuwa ndio wenye nguvu zaidi ndani ya chama,watu anao jua wanatahatarisha nafasi yake ktk chama,watu walio jitahidi kuhakikisha hapiti hata ktk kura za maoni

Nimengi sana aliyoyafanya sita kama spika yalioonekana kama utendaji mzuri mbele ya jamii lakini yakawa usaliti mkubwa mbele ya chama chake, wakati wa uongozi wake wapinzani walilalamika kuonewa lakini sasa wana regret kuwa hakuna spika kama sita kwa sasa, tumeona kauli mbalimbali za viongozi wa upinzani zinazo ashiria kuwa sita alikuwa spika pora kabisa kutokea nchi hii,

baada ya maamuzi ya chama kuwa watagombea wanawake tu Tanzania nzima ilizizima, kuonyesha ni jinsi gani sita alivyokubalika mbele ya jamii, na wote tulitaka arudi kuliongeza bunge hili jipya.

Ukiangalia kwa makini niliyo yaandika hapo juu, utagundua kuwa Sita alitambua kabisa kuwa nafasi yake ya kurudi Bungeni kama spika ilikuwa finyu kama ngamia kupenya kwenye tundu la sindano, hata hivyo kwa kujua hali ya upepo wa kisiasa ilivyo hivi sasa ukizingatia baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu, Sita alijitosa kugombea nafasi hiyo ili hali akijua kuwa hata kama atashindwa nafasi hiyo basi lazima atapata nafasi hata ya uwaziri ili kuwapoza wananchi wanao amini kuwa sita ni mchapakazi maridadi na hastaili kuachwa bila wadhifa wowote.

Baada ya vurugu zote hizo Sita ametangaza kutogombea tena ubunge kipindi kijacho, je kauli hiyo ya Sita ya kutogombea tena ubunge inamaanisha nini,

Tukumbuke wengi tumetabiri kuwa hili ni anguko la kisiasa la Sita, wengi tunaona kuwa kumpa sita uwaziri wa Afrika mashariki ni kumshusha hadhi, wengi tumefika mbali na kumtaka akatae uteuzi huo.

Sita ametangaza kuachana na ubunge na amekubali uteuzi wa uwaziri kwa maana kubwa kwake na hatima yake kisiasa, inasemekana mwanzo alikataa kabisa uteuzi wowote,baada ya kumshawishi sana waka mpa wizara fulani akakataa na nimoja ya sababu za kuchelewa kutangaza baraza (kama ilivyokuwa kwa mizengo aliyekataa kabla ya kukubali)lakini baada ya kubadilishiwa na kutafakari sana alikubali.
Anacholenga Sita kwa sasa ni upepo ukikubali agombee urais au astaafu siasa baada ya muhula huu kuisha

Kwanini urais, Matokeo ya uchaguzi huu yameipa funzo kubwa sana CCM ,kura za maoni na uteuzi wa wagombea umeicost sana CCM, mambo ya kulazimisha kusimamisha wagombea wasio kubalika yamempa moyo Sita
Katika siasa chochote chaweza tokea,nani alitegemea jk ataporomoka kiasi hiki, miaka 5 ni mingi na sioni jk atafanyanya nini kuuridhisha umma huu unaoonyesha kila dalili ya kumchoka, hivyo CCM itahitaji mtu makini na anaye kubalika na jamii kusimama kama mgombea wao ktk nafasi ya urais, na unapotaja walau watu wanaotia moyo kidogo CCM kwasasa huwezi kuto mtaja Sita, Magufuli, mwakyembe na wengine ambao hawana nguvu sana ndani ya chama, watu kama akina Membe wanatajwa lakini hawana mvuto ktk jamii ukizingatia kwa wakati huo naamini upinzani utakuwa strong zaidi ku compete nafasi ya uraisi na najua CCM haiwezi kufanya jipya kurudisha imani ya wananchi

Na amekubali nafasi hiyo ya uwaziri kwa maana ya kuwa karibu zaidi na system, na pia ni nafasi yake kuonyesha utendaji wake makini wa kazi, swala la kupewa wizara isiyo na umuhimu kwa mtazamo wa wengi haina mantiki,wakati mwingine kupewa wizara ngumu zinaweza kukusababishia ukaonekana hufai bure kama ilvyo kuwa kwa magufuli (zilpouzwa nyumba ikaonekana kama ni wazo lake binafsi kumbe ni order toka juu)
Hata hivyo wizara hiyo bado inachangamoto nyingi sana na ninafasi yake kuonyesha umakini wake kuongeza imani kwa wananchi waamini kweli ni mchapakazi.

Lengo lake la pili ni iwapo upepo wa kisiasa utakataa pengine ashindwe kugombea urais kwa sababu yoyote ile, basi ili kuonyesha ukomavu wa kisiasa anastaafu rasmi siasa na nadhani atabaki katika mambo ya chama na si siasa za majukwaani kama ilivyo kuwa kwa Sumaye na si kama mzee malechela,

Naamini kabisa mtu kama sita bado anahitajika sana katika uongozi wa nchi yetu kwa sasa ukilinganisha na viongozi wengi tu waliopo CCM,pamoja na madhaifu yake kama kama binadamu bado naamini kuwa Sita anayo nafasi kubwa ya kugombea urais iwapo litatokea hitaji hilo na iwapo wabaya wake watakapo tambua kuwa hakuna namna yoyote ya kufanya zaidi ya kumsimamisha sita kukinusuru chama, vinginevyo hali ni ngumu kwake na option ya kustaafu siasa ni muafaka kwake

Mwisho, Sita tupo wengi nyuma yako tunao kuunga mkono, tunakuomba uturekebishie hayo makubaliano ya jumuia yawe na manufaa kwa watanzania

Paulss
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom