Sita Kunaswa na Mtego wa MAFISADI, Uwaziri Utaokolea CCM Sura?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sita Kunaswa na Mtego wa MAFISADI, Uwaziri Utaokolea CCM Sura??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Uwezo Tunao, Nov 23, 2010.

 1. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Sita Kwenye Mtego wa MAFISADI pale CC ya CCM, Je Uwaziri Utakiokoa CCM Kuzama??

  Kumbukumbu kule bunge la Tisa zinaonyesha kwamba SIX alikua ni mwiba mchungu kwenye ngozi ya Kijiwe Cha Walarushwa nchini kwetu.

  Ukweli huu ulisababisha wanakiringe hao kulamba mchanga kwa midomo huku wakichapa kidole kwamba kwa awamu hii mpya katu mpiganaji wa haki za raia hakai tena mbele huku akichochea moto wa kuwatoa jasho jingi washikaji hawa. Katika kutimiza ahadi hizo kuna madai kwamba MAFISADI walilazimika kutumia hadi karibia senti ya mwisho kuhakikisha kiziki hicho cha MPINGO kinaelekezwa viti vya akina yakhe nyuma kabisa bungeni ili hata kwenye kutafutwa Waziri Mkuu sura yake isionekane.

  Sasa baada ya mafanikio hayo ya MAFISADI kuzima ndoto za wananchi kila kona ya demokrasia kunatuletea fundisho gani mpaka hivi sasa??? Je, hili la Mafisadi kufuzu mtihani wa kuhakikisha Six hatoboi ukuta wa CC ya CCM hasa inaleta maana gani kwetu?? Ndio kusema ya kwamba huenda chombo hicho cha juu kikawa kimo mifukoni mwao Mafisadi??
   
 2. s

  skeleton Member

  #2
  Nov 23, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Narudia tena, kwa Mh. Sitta kukubali kubaki CCM, yeye mwenyewe amejimaliza kisiasa. Hii ni kwasababu CCM ni chama cha kifisadi, na yeye sasa atakuwa chini ya amri ya mafisadi haswa atakapopewa uwaziri (kama atapewa kweli)! Na pia sasa hatakuwa hawezi kupinga kitu chochote cha kifisadi kwani kitatakiwa kipitishwe na chama ambacho kimeelemewa na idadi kubwa ya mafisadi.

  Na hii pia ina apply kwa wapinga ufisadi wote walio ndani ya CCM. Ni muda mzuri kwao kutoka katika chama au kukubali kubaki na kumezwa na mafisadi na kuukumbatia ufisadi. Hii ni kwasababu CCM main agenda yake ni ku promote ufisadi na kulinda maslahi ya mafisadi, kwahiyo itakuwa ngumu kupingana na agenda kuu ya chama ukiwa ndani ya CCM. Na utakapopingana nao kuna kipindi utajiona mshindi lakini mwisho wa siku mafisadi watakufanyizia tu. Watu kama kina Mwakyembe wasijione wameshinda, bado dawa yao inachemka hakika!
   
 3. T

  Tanganyika Member

  #3
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sita, Anna Kilango na Mwakyembe nasikia mko kwenye horodha ya kuukwaa uwaziri, angalieni isije ikawa ni mtego wa mafisadi wa kupunguza vita vya kupambana na mafisadi, Mkipata uwaziri msije mkaona ndo mmefika kumbukeni kauli ya mh. Mramba alivyoleweshwa na madaraka hadi kusema ndege ya rais ni lazima hata kama watanzania watakula majani!! Leo mramba pamoja na anazo chapaa yuko wapi?? huu ni mwanzo tu! Uwaziri mnaosubiria kwa hamu inawezekana ikiwa ndo tiketi yenu ya kutoingia mjengoni- Dodoma 2015 angalieni zawadi aliyoipata Mh. Marmo , Masha, Dialo na Mramba au ikawa tiketi ya kuwapeleka Mahakama ya kisutu kwa siku zijazo!!!!! Kumbuka unaweza ukaanza vizuri lakini ukamalizia vibaya. Namshukuru sana Mungu kwani ametufungua watanzania na anatujibu maombi yetu.   
Loading...