Sita Kuanguka Kwenye Mtego wa MAFISADI pale CC ya CCM INAMAANA GANI????


U

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2010
Messages
6,947
Likes
13
Points
0
U

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2010
6,947 13 0
Sita Kuanguka Kwenye Mtego wa MAFISADI pale CC ya CCM INAMAANA GANI????

Kumbukumbu kule bunge la Tisa zinaonyesha kwamba SIX alikua ni mwiba mchungu kwenye ngozi ya Kijiwe Cha Walarushwa nchini kwetu.

Ukweli huu ulisababisha wanakiringe hao kulamba mchanga kwa midomo huku wakichapa kidole kwamba kwa awamu hii mpya katu mpiganaji wa haki za raia hakai tena mbele huku akichochea moto wa kuwatoa jasho jingi washikaji hawa. Katika kutimiza ahadi hizo kuna madai kwamba MAFISADI walilazimika kutumia hadi karibia senti ya mwisho kuhakikisha kiziki hicho cha MPINGO kinaelekezwa viti vya akina yakhe nyuma kabisa bungeni ili hata kwenye kutafutwa Waziri Mkuu sura yake isionekane.

Sasa baada ya mafanikio hayo ya MAFISADI kuzima ndoto za wananchi kila kona ya demokrasia kunatuletea fundisho gani mpaka hivi sasa??? Je, hili la Mafisadi kufuzu mtihani wa kuhakikisha Six hatoboi ukuta wa CC ya CCM hasa inaleta maana gani kwetu?? Ndio kusema ya kwamba huenda chombo hicho cha juu kikawa kimo mifukoni mwao Mafisadi??
 
Msanii

Msanii

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2007
Messages
6,446
Likes
393
Points
180
Msanii

Msanii

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2007
6,446 393 180
naona unatoa maelezo ya jibu hapo.
unaulizia cc inavyoweza kudhibiti mambo wakati unaona kabisa inafanya hivyo kwa ufanisi mkubwa.
kudumu chama cha wahuni
 

Forum statistics

Threads 1,237,684
Members 475,675
Posts 29,297,361