Sisiyemu, sisiyemu! Zama za watawala wa kikerewe zimekwisha.

isotope

JF-Expert Member
Apr 4, 2012
2,392
816
Salaamu wanajamvi,
naomba niwasimulie habari za watawala wa Kikerewe.
Kabila la wakerewe ni miongoni mwa makabila yaliyokuwa yakitawaliwa kifalme. Wafalme hawa walikuwa dhalimu sana. Mtu yeyote alitisha maslahi ya mfalme aliuwawa. Aina ya kifo ilitegemea na aina ya kosa la mtuhumiwa husika. Hivyo kuna waliouwa kwa kukatwa na shoka, wengine waliuwawa kwa kuchomwa na vitu vyenye ncha kali kwenye masaburi yao hadi vitokezee utosini.
Baada ya tukio hilo la mauaji, ndugu wa marehemu walilazimika kuchagua ng’ombe aliyenona na kumpelekea mfalme. Tukio la kukabidhi zawadi liliambatana na maeneno ambayo yanaweza kutafsiriwa hivi: TUNAKUTOLEA ZAWADI HII EE MFALME ILI KUKUPONGEZA KWA KUONDOA KIZUIZI KWENYE NJIA YAKO. Bila kufanya hivo mfalme angeweza kufuta ukoo mzima.
Nchi yetu imeshuhudia vifo vingi yenye utata ambayo nimekuwa vikihisiswa ni kuondo vizuizi kwenye njia za watu flani.Orodha inahusisha viongozi wa kitaifa hadi wa mtaa (m/kiti wa CDM Usa river) hata raia wa kawaida; mfano mauaji ya Igunga , Arusha nk. Kuna vilivyoshindikana, mfano ajali ya mwakyembe (ripoti iko kwa IGP). Watawala wanachelea kufanya uchunguzi wa vifo hivyo. Mbona tuliona tume ikiundwa kuchunguza vifo vya wafanyabiashara wa madini? Kama sisiyemu haifaidiki na vifo hivyo mbona haiagizi serikali yake ifanye uchunguzi? Wananchi tunatendewa kama kondoo wa kuchingwa.
Kama vile watawala wa kikerewe, sisiyemu walitegemea JoSHUA achague ng’ombe aliyenona akawape zawadi kwa kumumua kamanda wake? Joshua, kwangu mimi kauli yako ni ya kukomesha uaji wa kisiasa nchini mwetu. Kama sisiyemu wanabisha wauwe mtu tena waone kama issue haitawageuka. Kijana tupu pamoja wakati huu unapopitia upepo wa kisiasa. Ile shilingi elfu mbili nilikuchangia kwenye kampeni zako naona unaitendea haki. Umefanya kitu ambacho hata Mbowe au Slaa hawajafanya. Watu wanakufa wao wanamtumia kiongozi wa ngazi ya chini kutoa tamko. Kitu gani bora zaidi ya uhai wa binadamu? Hakuna kitendo cha kiungwana cha kumfanyia muuaji kuliko kuamua kuaka mbali naye.
 
Back
Top Bottom