Sisiem na hili la uchaguzi wa umeya arusha mnatia kichechefu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sisiem na hili la uchaguzi wa umeya arusha mnatia kichechefu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by YanguHaki, Dec 21, 2010.

 1. YanguHaki

  YanguHaki Senior Member

  #1
  Dec 21, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani mbona SISIEM inatupeleka pabaya! Kweli tuna sheria za kipuuzi za namna
  hii zinazoweza kuruhusu mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga aitwye Mary Chitanda kushiriki uchaguzi wa umeya Arusha mjini unaofanywa na madiwani wa kule? Sijui kwa kuwa ni katibu wa SISIEM wa Wilaya Arusha? Tuite ni ulevi wa madaraka au kujisahau au ni nini hiki? Naona kila dalili ya kutaka kuvuruga amani ya nchi kwa uchu wa kutaka kupata kila nafasi ya uongozi nchini. Maslahi ya SISIEM yapo mbele ya WANANCHI wa taifa lake. Siku mambo yakiharibika hapa nchini hii lawama mtaikwepa vipi? Wako wapi wazee wa chama au nao ndo wamepofuka? Hawaoni? Ila tahadhari tuendako huko wengi mtaishia The Hague msipoangalia.
   
 2. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2010
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mimi nina swali kwa mwenye kujua anisaidie. Nalo ni je chaguzi zinazoendelea za wenyeviti wa halmashauri za wilaya na mameya wa miji na manispaa zinasimamiwa na ofisi gani??? Tume ya uchaguzi (NEC)??? au ofisi gani??? Nauliza hivyo kwa sababu pamoja na matatizo yote yaliyotokea Mwanza, Arusha, na sehemu nyingine, sijasikia maelezo yoyote toka ofisi inayohusika na chaguzi hizi. Suala la Mary Chitanda, linatakiwa kutolewa ufafanuzi wa kina na hiyo ofisi, lakini SIJASIKIA KITU na ndio maana Mambo yanajiendea tu kama yalivyo.
   
Loading...