Sisi wenye GPA chini ya < 2.8 tunatumia njia gani kupata scholarships za nje ya nchi

kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
2,030
2,929
Habarini ndugu zangu, mwenye kujua au mwenye ushuhuda wa uwezekano wa kupata scholarships kusoma nje ya nchi kwa sisi wenye GPA chini ya 2.8, mfano mimi nina GPA ya 2.6 level ya degree, je nawezaje kupata scholarships niweze kusoma Postgraduate degree (Masters).

KARIBUNI KWA MSAADA
 
Mko wangapi? It means mmefeli na hivyo mnatakiwa kuurudia mtihani ili mpate alama za ufaulu.

Hakuna namna. Vinginevyo unataka mtafutiwe alama za michongo kama PhD za You-Do-M? Because, nasikia huko Bongo hakuna kinachoshindikana--they say, wewe tu na pesa zako!
 
Mko wangapi? It means mmefeli na hivyo mnatakiwa kuurudia mtihani ili mpate alama za ufaulu.

Hakuna namna. Vinginevyo unataka mtafutiwe alama za michongo kama PhD za You-Do-M? Because, nasikia huko Bongo hakuna kinachoshindikana--they say, wewe tu na pesa zako!
Mtu kagraduate unamwambia arudie mtihani, we unashida ase
 
Huwa nasoma kwenye kwenye wavuti za vyuo vyetu kufanya master kama haukidhi vigezo vya GPA 3+ lazima uwe umefanya kazi eneo husika zaidi ya miaka 5.
Taratibu nyingi zinafanana duniani inaweza ikawa hivyo huko nje.
Jambo la pili uwe umefanya tafiti na kuzichapisha, vile vile unaweza omba post graduate diploma kisha uunge master.
Pole mkuu kwa kukosa hio GPA pambania ndoto yako kwa njia zote, hakuna kinachoshindikana chini ya jua.
 
Kwa sasa kigezo cha kusoma masters ni GPA kuanzia 2.7 degree kwa hapa Tanzania sijajua uko nje
 
Kupata scholarship unaweza kupata, mfano wa gpa uliyopata kwa mfumo wa UK unaangukia kwenye daraja linaitwa 2:2 ambapo kwetu ni lower second class. Na baadhi ya vyuo kwa scholarship za chevening, commonwealth na erasmus mundus wanapokea. LAKINI LAZIMA UONGEZE KITU KIPYA
-Machapisho (jornals za kitaaluma)
-Postgraduate degrer (masters au PGD)
-Muda wa kazi zaidi (miaka isiyopungua miwili)
Na motivational letter yako ijielezee ikaeleweka hapo unakuwa umemaliza kabisa
-Lakini pia usiombe vyuo vyenye rank za juu sana

Kwa za USA na barani Asia wataongezea wengine lakini kwa kidogo navyojua scholarship nyingi za Asia (China (mofcom) na Korea kusini (KOICA na KGS)) hawa wanaangalia sana wafanyakazi wa utumishi wa umma hata kama gpa ikiwa chini ukaweza kuwashawishi uwezo wako wa kiuongozi basi unapata japo kwa gpa hiyo sijaona bado ila gpa ya 3.2 nimeona na 3.4.
 
Back
Top Bottom