Uchaguzi 2020 Sisi Watanzania tunakushukuru sana Tundu Lissu kwa kampeni zako za kiwango cha juu, Tunakutakia kila la heri, Mungu aendelee kukulinda

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,600
218,003
Nikiwa mmoja wa maripota wa Kampeni za Tundu Lissu humu JF na kwingineko kuanzia mwanzo hadi mwisho na kwa kadri ya umri nilionao na uzoefu wangu katika siasa za Tanzania na za kimataifa, Tundu Lissu amefanya kampeni za kiwango cha juu mno, huyu mtu hakuwa tu mgombea wa Urais bali alikuwa Mwalimu wa siasa na haki za Raia.

Elimu kali ya Uraia aliyoitoa kuanzia Zanzibar hadi Tanganyika haijawahi kutolewa na yeyote kuanzia wakoloni wala waliopo leo, amefichua mambo mazito mno yaliyofichwa kwa miaka mingi sana, kwa ujumla ni kwamba kwenye uchaguzi wa mwaka huu wananchi wa Tanzania wamepata faida kubwa mno na nina hakika sasa wananchi wengi sana wameelewa kinaga Ubagha namna nchi yao ilivyojaa makando kando ya aibu yanayolidhalilisha Taifa.

Kwa niaba ya Wananchi wa Tanzania wa ndani na nje ya nchi, natoa shukrani za dhati kwa Tundu Lissu kwa wema wake aliotutendea kwa kuamua kutushirikisha kwenye kila uozo uliofichwa kwa miaka mingi kwenye nchi hii, SPANA zilizopigwa hakuna yeyote katika wanaccm walio hai leo mwenye uwezo wa kujibu , kwa kifupi ni kama wanaccm wote wamevunjwa viuno.

Namuomba Mwenyezi Mungu aendelee kumlinda Lissu kwa ajili ya Uhai wa Nchi yetu
 
Amina🙏🙏

Hakika Tundu Lissu ataendelea kuishi kwenye mioyo ya watz wote hadi umauti utakapomfika....

Tundu Lissu akili nyingi.... Hafai kwenye taifa la kidikteta hasa awamu hii....AWAMU HII ITAPITA

Mungu amjalie afya njema ili apate Urais na kutupeleka nchi ya ndoto yake yenye UHURU, HAKI NA MAENDELEO YA WATU.
 
Dah kweli wakati ukuta. Majigambo yote yale yale safari hii lazima kieleweke, tutaingia barabarani, dunia yote ipo nasisi, mara pompeo, mara kuwadi wa mashoga amstadam, leo hii mnaishia kushukuru bora liende!!!. Nimesikitika sana
Una uwezo mwembamba sana !
 
Amina

Hakika Tundu Lissu ataendelea kuishi kwenye mioyo ya watz wote hadi umauti utakapomfika....

Tundu Lissu akili nyingi.... Hafai kwenye taifa la kidikteta hasa awamu hii....AWAMU HII ITAPITA

Mungu amjalie afya njema ili apate Urais na kutupeleka nchi ya ndoto yake yenye UHURU, HAKI NA MAENDELEO YA WATU.
Survival for the fittest mkuu!! Kungaliko tumaini..kuna siku niliwahi fuatilia maisha ya Mobutu Seseko,Habre of Chad,Nk..wakati ni mwalimu mzuri wa nyakat!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Upuuzi mtupu. Ruzuku hazitoshi kula wote sasa hivi, so kila mtu kivyake. Chama cha Mbowe cha hovyo sana.
 
Basi hongera kwake, lakini Ikulu ya Tanzania haingii NG'O. Tulilisema hilo kabla ya uchaguzi na tunalisema baada ya uchaguzi.
 
Tundu Lissu ni kiboko. Kwa muda mfupi miezi 4 aliyokaa nchini ametusaidia sana wa Tanzania katika mambo mengi. This time CHADEMA walikuwa na mgombea rais bora kabisa ambaye alimpelekesha Jiwe hadi akakonda na kupoteza matumaini. System yote ilichanganyikiwa hadi kufikia kufanya mambo ya aibu kabisa ambao yamemchafua jiwe na utawala wake.

Uchaguzi huu umekuwa uchaguzi muhimu sana na umejenga foundation ya kudai mabadiliko ya msingi ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Wa Tanzania tumeona na dunia imeona. Hatuta fanya uchaguzi tena katika mazingira kama haya. Huu ndo mwisho.

Kwa sasa ni muhimu sana Lissu aondoke nchini ili kupata uwanja salama na huru wa kupaza sauti na kuleta mabadiliko.

Wote wanao mkejeli Lissu siku moja watampigia makofi. Mark my word.
 
Back
Top Bottom