Sisi watanzania ni wanafiki, kazi yetu ni kupiga domo sana huku wachache wakila nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sisi watanzania ni wanafiki, kazi yetu ni kupiga domo sana huku wachache wakila nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jumakidogo, Jul 12, 2012.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Sisi watanzania ni wanafiki, kazi yetu ni kupiga domo sana huku wachache wakila nchi. Rasilimali za nchi wanafaidi watu wachache. Wakitokea mashujaa wachache kujaribu kuleta mageuzi.
  Tunachochea moto huku tukiwa tumejificha na kuficha nyuso zetu tusionekane. Utaona wanafiki wanashabikia mgomo wa madaktari kwa maneno tu, huku wengine wakificha hata majina yao. Badala ya kujitokeza hadharani kuungana na wagomaji hadi kieleweke.

  Nchi ina hali mbaya! Ardhi inaporwa, madini yanamalizwa, wanyama nao wanahamishwa kila kukicha, mfumuko wa bei, kila kitu kimekaa tenge. Hivi kwa hali hii kuna haja ya kusubiri mpaka uchaguzi 2015? Tuacheni unafiki na woga, waarabu wa misri walionyesha mshikamano na wakaweza. Sisi tunasubiri nini? Mpaka walimu na madaktari wagome huku tunashabikia kwa kuficha nyuso zetu?

  Ukombozi unataka ujasiri...saa ya ukombozi ni sasa.
   
 2. S

  SHIMBONONI Senior Member

  #2
  Jul 12, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Bravo well said comrade!!
   
 3. asrams

  asrams JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 4,011
  Likes Received: 1,381
  Trophy Points: 280
  Naaaam kaka. "that's why we are still behind"
   
Loading...