Sisi wataalam wa Tanzania tumesikitishwa na kauli yako Rais Magufuli

Mtangoo

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
6,167
5,610
Nianze kwa saalam kwako mh. Rais na kukupa pole kwa kuongoza nchi kubwa kama yetu. Nimebahatika kuwa katika uongozi mdogo sana na huko niliona ugumu wa kuongoza wanadamu. Sina shaka una kazi ngumu sana ya kuongoza nchi ambayo ni kubwa kuliko Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi zikiunganishwa.

Nimeisikiliza hotuba yako uliyoitoa wakati unamkaribisha mh. Rais Paul Kagame wa Jamhuri ya Rwanda. Nimeielewa hotuba yako vyema. Lakini pia nikasoma maoni ya Watanzania hasa katika uzi huu wa hapa JF. Baada ya kufuatilia kwa kina, nimeamua kuandika hapa. Kabla sijaenda kwenye hasa ninachotaka kusema naomba niweke vyema vitu kadhaa maana nikiwa mwenyeji wa hapa JF uzi huu hautachelewa kuwa wa kisiasa au hata kujaa matusi.

1. Nimeielewa nia nzuri iliyo katika hotuba yako ya kuleta mambo pamoja. Nakubaliana na tija ambayo System nzima italeta. Ninakuunga mkono asilimia mia moja.

2. Kwa nilivyoielewa hotuba husika, hakuna mahali umeonyesha lengo au nia ya kutudharau wataalamu wako. Infact, umeonyesha malengo ya kutumia e-Government katika kuifanya adhma yako. Kwa hiyo uzi huu si kwa ajili ya kukuhukumu.

3. Uzi huu hauna lengo lolote la kisiasa, au lingine lolote zaidi ya kutoa ya moyoni. Kama kukufikia mh. Rais ingekuwa ni rahisi, nadhani ningeshaleta ushauri mwingi sana huko. Ila sio rahisi hata kidogo, ndio maana nimeamua kuandika hapa, nikijua pengine kama si wewe basi kuna mmoja aliye karibu nawe atakuarifu juu ya hili.

Baada ya kusema hayo naomba niende katika hoja yangu. Mheshimiwa Rais, binafsi sikubaliani na hoja ya kuchukua wataalam Rwanda kwa ajili ya kutengeneza mfumo maalum wa Teknohama kwa ajili ya kuunganisha mfumo wa Serikali (Centralized Government Portal). Hii ni kwa sababu Wataalam tupo na tunaweza kufanya hayo yote. Sioni sababu yoyote ya sisi kwenda kuchukua wataalam Rwanda au nchi nyingine yeyote.

Mh. Rais, nitajitolea mfano, lakini nakuhakikishia wapo wengine pia ninaowafahamu wana uwezo wa kujenga huu mfumo. Pia baadhi ya maelezo nitayaacha kuwa siri kwa kuheshimu mikataba ya watu niliofanya nao kazi. Nalazimika kuweka ushahidi kwa sababu ya masimango, kejeli na kila namna ya mabaya ambayo tumesemewa katika maeneo mbalimbali baada ya kauli yako hii ambayo imeleta mijadala katika mitandao ya kijamii.

1. Kwamba Hatuna Ufahamu wa Kutosha
Kuna waliojenga hoja kwamba hatuna ufahamu wa kutosha. Mh. Rais hili sio kweli. Mimi kama sample space ya kuwakilisha wengine kwa mfano ninafahamu vyema kila kinachohitajika kujenga system ya aina hiyo. Mwaka 2008 au 2009 (sikumbuki exactly ni upi) mimi na vijana wenzangu wawili tuliamua kubadili mfumo wautendaji katika eneo fulani, na kuondoa makaratasi na usumbufu wa kuwaona watu. Kazi zilifanyika hata kama mtu hayupo ofisini. Ni kwa sababu tu tuliaminiwa na mkuu wa idara na Meneja wetu. Kwa miaka iliyofuata nimefanya kazi ya utengenezaji wa programu, uongozaji na ushauri (Consultancy, System Architecture, Leading Developer) katika Taasisi na Kampuni binafsi, ndani na nje ya nchi. Siwezi kuweka wazi projects tulizofanya kwa sababu nilizosema, ila baadhi ya project za nje ya nchi mh. Rais zimefanywa na raia wako japo sifa wanapata wao kwa sababu wao ndio wamiliki.

2. Kwamba hatuna Uzoefu
Kama nilivyokwisha sema hapo juu, kuna Watanzania wengi mh Rais tulio na uzoefu wa ndani na nje ya nchi. Binafsi nimeshafanya kazi ndani na nje ya nchi na nina uzoefu wa kutosha. Lakini pia nawafahamu watu ambao wana uzoefu wa kimataifa kama mimi. Mfano kuna rafiki yangu mmoja hivi karibuni alikuwa nchi moja ya karibu na Afrika kusini akifanya kazi kubwa ya Teknohama, kazi ya serikali ya huko. Kwa hiyo si kweli mheshimiwa Rais kuwa hatuna uzoefu.

3. Kwamba tunapenda 10%
Mh. Rais, Watanzania wenzetu wametusimanga kuwa sisi tunapenda 10%. Kwamba kuna wanaopenda rushwa, hilo lipo kila mahali. Hata Rwanda wapo, na kuna siku nilikuwa naongea na jamaa wa kutoka Bulgaria, pia alinihakikishia kwa mifano kuwa hata ulaya rushwa ipo na wapo wataalam wanakula rushwa.

Kilichonisikitisha mheshimiwa rais, ni kuwa wataalam wa nchi hii wote tumewekwa katika kapu la wala rushwa. ndivyo wao walivyotafsiri kitendo cha wewe kuagiza wataalam toka nje ilhali tupo wenye vigezo. Wakatusimanga kuwa tusingekuwa tunapenda 10%, tungeliaminiwa kupewa kazi. Mh. Rais, tangu nianze kufanya kazi kwa kuajiriwa na baadae kujiajiri, sijawahi kumwomba rushwa mtu, iwe 1% au 20%. Kiukweli ni kuwa wataalamu wako maendeleo yetu ni ya kinyonga kwa sababu hatuko tayai kula rushwa. Tunajisikia vibaya sana pale tunapokuwa waaminifu na kukubali kukosa "maendeleo" ya haraka na bado tukapokea masimango hayo. Hata hivyo kama Biblia inavyotuasa kuwa "tutapata nini kama tukiupata ulimwengu wote na kuukosa uzima wa milele" basi tutandelea kuwa waaminifu lije jua ije mvua. Sio kweli kuwa tunapenda 10%.

3. Kwamba tulipewa tukaharibu
Mh. Rais, wengine wametafsiri kauli yako kuwa eti tulipewa tukaharibu. Katika kazi zote nilizofanya, hakuna hata moja nililalamikiwa iwe kwa kuchelewesha au kwa kuifanya chini ya kiwango. Na mimi ni mmoja nikiwakilisha kundi kubwa la wataalamu wa teknohama Tanzania. Sio kweli tulipewa tukaharibu.

4. HITIMISHO
Mh. Rais, hayo ni machache kati ya matusi na masimango tunayopokea toka kwa rais wenzetu. Kitendo cha kuamua kuchukua wataalam toka Rwanda, ukituacha sisi tulio Tanzania kimetuumiza na kutukatisha tamaa. Hata hivyo kwa kuisikiliza hotuba yako na kuona nia njema iliyo ndani yake, naomba nikueleze kwa nini kama tupo "hatuonekani":

Mh. Rais, tuna utamaduni mbaya wa kutowaamini wataalam Watanzania. Tunajisikia vibaya kwenda nje ya nchi na kutoa suluhu ya matatizo ambayo hapa kwetu yanasumbua. Uwezo tunao ila hatupewi nafasi. Mh. Rais nikupe mfano halisi, mimi binafsi nilipewa ofa ya kufanya kazi nje ya Tanzania mara mbili, ili nikaishi huko kabisa. Walikuwa tayari kuingia gharama ambayo hakuna kampuni hapa Tanzania imewahi kunipa, hata nusu yake. Nilikataa kwa kujua kuwa sikuumbwa Tanzania kimakosa. Huko nako kuna walioumbwa kufanya ya huko. Mimi ni sehemu tu ya wachache waliokataa vyema kwa ajili ya kwao. Wapo wengi walioamua "kuzamia" baada ya kupewa ofa kama hizo. Kama serikali ingeamua kutuamini, naamini tusingekuwa hapa tulipo.

Kwa kuwa kampuni zetu ni changa na hazikubali kutoa 10%, kazi ambazo zingetutambulisha kwa Watanzania au hata kwako mh. Rais "tunazisikia kwenye bomba".

Jambo la pili, mh. Rais, hatupati support ya serikali. Mfano Rwanda, wana Wizara ya vijana na Teknohama. Wizara hii inazunguka kutafuta vipawa na kuvikuza. Si hivyo tu television yao ya taifa, Rwanda Tv ina vipindi ambavyo watu waliogundua vitu anuani katika Teknohama hupewa airtime bure kuonyesha na kuelezea uvumbuzi wao.

Nikuhakikishie mh. Rais, una wataalam wengi ambao hawana pa kutokea. Kama serikali yako ikiamua kuwapa support, unaweza kugeuza Tanzania hub ya ICT kwa muda mfupi sana. Ninawajua watu wenye idea nzuri ambazo hazifanyi vizuri hapa, ila Rwanda kwa mfano au Kenya, wanafanya vizuri sana. Ni kwa sababu ya support ya serikali zao.

La tatu na la mwisho kwa leo ni sheria zetu. Sheria nyingi za majirani zetu zinasaidia kukuza Teknohama. Nitatolea mfano wa Rwanda. Ili kudhibiti kuibiwa na wafanyabiashara wa usafirishaji, Wasimamizi wa kule (RURA) wameamuru magari yote yatumie mifumo ya kielektroniki kutoa tiketi. Kwa kuwa mifumo hii ni self auditing hawapotezi mapato. lakini kuweka ushindani, hawajampa masharti kuwa anayekupa huduma hii lazima awe fulani. Kila Mnyarwanda ana uhuru wa kutengeneza system yake na ikikidhi viwango vya RURA basi anaingia mkataba na mwenye kampuni ya usafirishaji.

Nifikishe tena masikitiko yangu kwa dharau tunazozipokea toka kwa raia wenzetu, na nikuombe ubadilishe uamuzi wa serikali yako wa kuchukua Consultants na Lead developers toka nje ya nchi. Ukifanya hivi utatuvunja moyo wataalam wako ambao tunaweza kufanya kabisa hizi kazi ila tutaziona tu zikipita kwenda kwa wenzetu.

Nikutakie kazi njema za majukumu yako.
Ni mimi,
BH

UPDATE:
Sikupenda kuweka qualifications zangu hapa kwa kuwa si nia ya bandiko hili kuwa tangazo binafsi. Lengo lilikuwa ni kuelezea masikitiko kwa niaba ya wataalam wenzangu ambao wanalalamika kimya kimya. Lengo lilikuwa ni kulisema ambalo wengine hawalisemi. Ila kwa posts nyingi hii ikiwa mfano wake nitaweka links chache kwa wale akina Tomaso kama mpendwa wangu huyu

Mkuu labda hujaelewa point yangu. Sijasema ku-desclose mikataba ya kazi. Point yangu ilikuwa kwamba kwa kusoma bandiko lako kwa mtu ambaye hakujui, hawezi kupata picha......

Pia unaweza kutafuta jina langu google utapata information
 
Wataalam wengi wa Tz mmekaa kiujanja ujanja mnawaza dili badala ya kufanya kazi ya uhakika kwa maendeleo ya watanzania.

Wataalam wazalendo ni wachache sana. Awamu zote kabla ya hii ya tano wenyewe tumeshuhudia uozo wa hao wataalam uchwara.Mashirika ya umma yamekufa,yameshindwa kujiendesha.

Viwanda vimekufa na vingine viko hoi taabani.

Nchi ya Rwanda pamoja na kupata machafuko 1994 lakini imeweza kujikusanya upya na sasa tunabaki kuimezea mate.

Wacha tu wataalam waje tuone kama ATC itanyanyuka upya.
 
Nashindwa kujua kwa nini hatujielewi. Hivi Rwanda si tuligombana nao juzi juzi hapa? iweje leo ni best friend wakati hatujapatana. Ubinafsi umezidi, tunatakiwa tujitambue.
Hawakugombana na sisi waligombana marais na mambo yao...... Tungegombana ubaloz ungefungwa
 
Ipo haja ya kurudisha adhabu ya vifungo kwa wataalamu wetu,waliohadibu au watakaohujumu kazi na miradi ya umma./

Tatizo wapo wachache waliowahi kuharibu na ndio wanaoponza wenzao.

Pia hata tutakapo chukuwa wataalamu kutoka nje pia wa kwetu wataandamana ili kupata au kushare uzoefu.
 
Wa-tz tunaweza pia ila tatizo la baadhi ya wakuu wa idara ni much know. Anataka ampe kazi mtoto wa fulani hata kama hajabobea ktk kazi hiyo.

Warwanda wakipewa wakaharibu tunajua pakufidia maana mashallah wamejaliwa.
 
System nyeti ya serikali mnawapa wageni wawatengenezee system hiyo
...mh. Hebu jirudi unda kikosi kazi hata ukiwashilikisha jwtz wafanye kazi hii...
Hii ni nyeti ya serikali
Halafu kwa kuongezea tu ni kwamba Kagame amebobea ktk masuala ya Espionage, unganisha dots na hao wataalam wake uone tunavyotembezwa uchi kimataifa.
 
Hii kwa kweli haijakaa vizuri..Tuna wataalamu wengi sana hapa nchini wangeweza kufanya hiyo kazi. Rwanda wamechukua system nyingi zilizotengenezwa hapa kwetu na wanazitumia. Iweje leo eti wao ndo waje watutengenezee system ambayo tuna uwezo wa kuitengeneza. Serikali imesomesha wataalamu wengi nnje ya nchi ambao wana uwezo wa kutengeneza hiyo IT Acct system. Hii ni dharau kwa nchi yetu na hata wanyarwanda wanatuona sisi mabogas
 
Nanukuu;-
hon.john p magufuri.
"wataalamu wa tanzania jiandaeni kufanya kazi RWANDA,pia wataalamu wa rwanda karibuni kufanya kazi Tanzania"
--->>what's wrong...?
in facts mh.rais HAKUFEDHEHESHA WATAALAMU WETU WATANZANIA.
-->>ILI INSIST KATIKA TECHS EXCHANGES...
{{{{--->>ANAJIULIZA RWANDA WALIWEZAJE?...MPAKA SISI TUKASHINDWA JAPO TUNADAI TUNA WATAALAMU WABOBEZI....}}}}
****PLS WHY WE DAILY CRIES...
~~SOMETIMES TUSIPENDE KULALAMA AU MLITAKA NAYE NAYE ASEME "SIJUI KWANINI TANZANIA NI MASIKINI?"...
...WE MUST LOOKS FORWARD--->>....
•••RAIS WETU SONGA MBELE...
 
Wataalam wengi wa Tz mmekaa kiujanja ujanja mnawaza dili badala ya kufanya kazi ya uhakika kwa maendeleo ya watanzania.

Wataalam wazalendo ni wachache sana. Awamu zote kabla ya hii ya tano wenyewe tumeshuhudia uozo wa hao wataalam uchwara.Mashirika ya umma yamekufa,yameshindwa kujiendesha.

Viwanda vimekufa na vingine viko hoi taabani.

Nchi ya Rwanda pamoja na kupata machafuko 1994 lakini imeweza kujikusanya upya na sasa tunabaki kuimezea mate.

Wacha tu wataalam waje tuone kama ATC itanyanyuka upya.

mwanamwana nisikilize mimi baba yako, Mwana Mtoka Pabaya. Unafiki si jambo jema na ni dhambi iletayo mauti.

Wataalam wengi wa Tanzania wamekaa ... si kauli njema. Unajumuisha watu huku ukichanganya tabia binafsi na taaluma. Hapa unaihukumu taaluma kwa kosa la jamii nzima. Wewe uonavyo, wataalamu ni wezi sababu ya utaalam wao au ni wezi sababu ya kutokea kwenye jamii inayoendekeza wizi?

Kufa kwa viwanda na vingine kubakia hoi ni kosa la wataalam au kosa la wasimamizi wa nchi yetu? Mbona tangu mimi nazaliwa Kiwanda cha CocaCola hakijafa? Kikifa kiwanda cha serikali, analaumiwa mtaalamu au serikali?

Kama mtazamo wako ni kuwa Watanzania hawawezi wapewe Wanyarwanda, basi haya na tuanze kuagiza wacheza soka, madiwani, wakuu wa mikoa na wengineo kutoka Rwanda.
 
uzalendo ni sifuri na tatzo ni 10%. tena unakiri kabisa kuwa "mh. rais hilo la 10% lipo kila mahali sio sisi tu" hahaha
 
mwanamwana nisikilize mimi baba yako, Mwana Mtoka Pabaya. Unafiki si jambo jema na ni dhambi iletayo mauti.

Wataalam wengi wa Tanzania wamekaa ... si kauli njema. Unajumuisha watu huku ukichanganya tabia binafsi na taaluma. Hapa unaihukumu taaluma kwa kosa la jamii nzima. Wewe uonavyo, wataalamu ni wezi sababu ya utaalam wao au ni wezi sababu ya kutokea kwenye jamii inayoendekeza wizi?

Kufa kwa viwanda na vingine kubakia hoi ni kosa la wataalam au kosa la wasimamizi wa nchi yetu? Mbona tangu mimi nazaliwa Kiwanda cha CocaCola hakijafa? Kikifa kiwanda cha serikali, analaumiwa mtaalamu au serikali?

Kama mtazamo wako ni kuwa Watanzania hawawezi wapewe Wanyarwanda, basi haya na tuanze kuagiza wacheza soka, madiwani, wakuu wa mikoa na wengineo kutoka Rwanda.
***
DONT PANIC....
"ONLY TECHS EXPERT"NA SI KILA UTUMBO.
 
Back
Top Bottom