Sisi wanyonge sasa Tumepata Nguvu. Rais Uishi Milele uje ukutane nayo haya

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Napenda kutoa pongezi zangu za "zati' kwa mh mtukufu rais kwa maamuzi aliyoyafanya katika suala la korosho.

Hawa wanunuzi walianza kudhani wana nguvu kuliko serikali.wanataka kununua korosho kwa wakulima maskini kwa bei ya chini kulingana na soko la dunia.wajinga.sisemi wapumbavu.wajinga.

Hizo korosho walipaswa kununua maana rais alishasema zinunuliwe.wao wanabisha.wanambishia rais mwenye jeshi?wao hawana jeshi.wana akili?tena rais asiyetikisika?ni kma mlima kilimanjaro.

Mheshimiwa ukimaliza korosho hamia na kwa wanunuzi wa mahindi nao wananunua kwa bei ya chini sana.wape siku 2 tu wasiponunua yote kwa bei elekezi watume wanajesh wetu waje wasombe yoote.

Hata nyama pia kwa sasa wateja hamna.naona wamefanya mgomo wa kununua nyama...buchan nyama inakaa wiki nzima.hawa nao usiwaache mheshimiwa rais.waandaje wajeshi wetu waje wapakie nyama zote tupewe wananchi bure.

Mimi nina kiduka changu hapa mtaani watu hawanunui sukari.hii yote ni kukwamisha juhudi zako mh.hawa nao wakomeshwe.maana yake wamegoma kutumia sukari ili ionekane maisha magumu wakati si magumu.

Kuna migomo mingi inafanywa na wafanyabiashara hawa.wanakwamisha juhudi zako.sasa ni kutumia tu wajeshi.tena kwenye korosho hawa wajesh walete dar wabangue kwa mikono tu.hata bei yake ishuke.

Mimi napenda sana korosho.lakini naumia bei ya korosho... Wanauza kwa bei ya juu hata inaniumiza.sasa hizi korosho ziletwe dar tuuziwe kwa bei ya karanga.watanzania maskini nasi tule korosho.

Siyo tunasafirisha tu korosho nje na hata ladha yake hatuijui.mtukufu rais pia angalia na wale wafanya biashara wasiotaka kununua nyanya mpaka zinaozea wakulima.wajeshi wetu watumwe wakazisombe.serikali itulipe hiyo pesa maana nyanya zinaoza tu.

Mimi mtanzania mnyonge nmeanzisha kilimo cha mboga mboga... Wanunuzi wanakuja na bei zao ndogo eti uchumi umeyumba.hawa nao wapewe siku chache tu kama vipi utume wajeshi waje kununua.hakuna kuremba.

Hakuna kutikisika, hakuna kuchechemea. Huko ntwara wakisimama mshale,wakikimbia mshale,wakichuchumaa mshale,wakilala mshale. Na hizo korosho. Wasimung'unye, wasiteme, wasimeze wasiziache mdomoni.

Hapa kazi tu.
 
Naunga mkono juhudi za rais kununua mazao toka kwa wakulima kwa bei ya juu kuliko soko. Kweli anawajali wanyonge.
 
Nilikuwa sijayaona magego ya wakuu wengi kitambo sasa.Huu ni wasaa muafaka wa kucheka kwa madaha hadi magego yaonekane na machozi kububujika.
 
Back
Top Bottom