Sisi wananchi tunawaungaje mkono akina zitto?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sisi wananchi tunawaungaje mkono akina zitto??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Apr 21, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,792
  Likes Received: 3,879
  Trophy Points: 280
  Kila mtu ameshuhudia sakata linaloendelea bungeni! Tumeshuhudia uozo wa ajabu kwenye ripoti ya CAG na zile za Zitto, Mrema,na Cheyo! Tumeshuhudia wabunge wetu vijana akina zitto wakiwabana mawziri wajiuzulu na pia ikiandaliwa motion ya kumuondoa waziri mkuu!

  Swali je sisi wananchi tunawasupport vipi hawa wapiganaji wetu nje ya bunge?? Tuendelee kukaa na kuandika tu maoni na kuulizia updates kama mawaziri wamejiuzulu au la??

  Tukumbuke hii nchi ni yetu rais na mawaziri wetu tumewapa tu dhamana kuiongoza,kama hawatendi tunavotaka ni jukumu letu kuwa sweep out! Mimi napendekeza tujadili hapa plan B ya kuwaondoa hawa wanaotafuna nchi bila aibu!

  Tujiandae kuingia barabarani kwa maandmano makubwa kuiondoa serikali hii dokozi au kama hatuwezi tunaogopa tukae kimya tujadili mambo ya akina marehemu kanumba na lulu basi tusitokwe na mishipa na mapovu kama akina Zambi lakini hatutendi lolote!

  Kwa kuanzia tufungue mjadala namna ya kuandaa maandamano makubwa na mbinu zinazofaa tusiwaaachie wapambanaji wetu peke yao wakati nchi ni yetu mimi nipo tayari kuongoza mapambano na kama risasi ya kwanza acha inipate mimi kwanza ili tukomboe nchi yetu kwa vitendo, nakaribisha maoni na mapendekezo!!!
   
Loading...