Sisi wafuasi wa Hayati Magufuli tumeumizwa sana na maneno haya ya Rais Samia

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,806
18,786
Sisi wafuasi wa Magufuli tumeumizwa sana na maneno haya ya Samia baada ya kutoka Ulaya, tunauliuza watu hawa walikuwa chama kimoja kweli? Achilia mbali kuwa kwenye ticket moja ya kupigiwa kura.

Tunauliza where is our pride? Maneno haya ni kinyume kabisa na kujiamini alipotupa Magufuli na Kabudi...na wana CCM wengi walivyo wanafiki wanampigia makofi kama walivyopiga kwa Magufuli, ndiyo maana kuna wakati najiuliza CCM ni chama cha siasa au ni genge tu la watu wanaolindwa na mabunduki kujipa madaraka na kula kodi zetu?

Ni chama gani cha siasa kisichokuwa na itikadi? Ukiwaambia hii haifai wataitikia na kushangilia, kesho mwingine anakuambia inafaa wanashangilia tena, hiki ni chama kweli? Tunapata wapi confidence ya kuwakejeli vyama vingine kama chama chetu kipo hivi?


Rais Samia amesema haya, nanukuu

Lakini pia tumeweza kukwamua miradi iliyokuwa imekwama, kama mnavyojua katikati hapa tulichokozana kidogo na umoja wa Ulaya uhusiano ukatetereka miradi ikakwama, Lakini tumeshakwamua fedha mradi mmoja umeshatiliwa na mwingine utatiwa hivi punde, kazi zitaendelea.

Kuna fedha nyingi zimetengwa kwa ajili ya Afrika kama Euro Bilioni 150 ambazo hizo sasa ni kinyanganyiro kwa Afrika. Atakayewahi mwanzo kupeleka miradi ya maana ndiye atakayepata fungu kubwa, kwa hiyo nasi tunajitayarisha tumeanza kupeleka...



 
Mtu alishakufa mnajifanya wafuasi wake kwa hiyo mnaongozwa na mzimu? Nyerere mwenyewe alipokufa aliibuka Kikwete akajiita JK watu wakaaminishwa eti alikuwa mwanafunzi wa Nyerere na mfuasi wa Nyerere Ila alichokuja kufanya anajua mwenyewe.

Same as nyie mnaojifanya wafuasi wa mfu, Magufuli is dead so as his doings, beliefs and legacies.

It's high time for you to come back to your senses and get used to the new system coz things will never be the same again.
 
sisi wafuasi wa magufuli tumeumizwa sana na maneno haya ya Samia baada ya kutoka Ulaya, tunauliuza watu hawa walikuwa chama kimoja kweli? achilia mbali kuwa kwenye ticket moja ya kupigiwa kura
tunauliza where is our pride? maneno haya ni kinyume kabisa na kujiamini alipotupa Magufuli na Kabudi...na wana CCM wengi walivyo wanafiki wanampigia makofi kama walivyopiga kwa Magufuli, ndio maana kuna wakati najiuliza CCM ni chama cha siasa au ni genge tu la watu wanaolindwa na mabunduki kujipa madaraka na kula kodi zetu? ni chama gani cha siasa kisichokuwa na itikadi? ukiwaambia hii haifai wataitikia na kushangilia, kesho mwingine anakuambia inafaa wanashangilia tena, hiki ni chama kweli? tunapata wapi confidence ya kuwakejeli vyama vingine kama chama chetu kipo hivi?

CCM kama chama ni kuanzia kipindi cha Nyerere mpaka wakati wa Mkapa tu! Baada ya hapo, iligeuka kutoka chama na kuwa kikundi cha watu wachache wanaofaidi mema ya nchi, huku wananchi walio wengi wakiishi maisha ya kupigika..
 
Mfuasi wa mwendazake???

Unauliza CCM ni chama gani??

Kwa hiyo ndiyo maana mlianza kuunda CCM Mpya SK Gang ndani ya CCM siyo?

It is revealed, kwamba mlijenga kikundi cha wahujumu nchi kwa nia ya kupambana na CCM.

CCM ni taasisi kongwe, imara, yenye nguvu na isiyoyumbishwa na mtu awaye yeyote hata akiwa jiwe
 
Mtu alishakufa mnajifanya wafuasi wake kwa hiyo mnaongozwa na mzimu? Nyerere mwenyewe alipokufa aliibuka Kikwete akajiita JK watu wakaaminishwa eti alikuwa mwanafunzi wa Nyerere na mfuasi wa Nyerere Ila alichokuja kufanya anajua mwenyewe.

Same as nyie mnaojifanya wafuasi wa mfu, Magufuli is dead so as his doings, beliefs and legacies.

It's high time for you to come back to your senses and get used to the new system coz things will never be the same again.
Mkuu unajua maana ya chama cha siasa? chama cha siasa kipo defined na princiles ambazo zinakiamini ambazo ndizo hutumia kushawishi wananchi na wananchi wakakipa madaraka. Kama Samia na Magufuli walikuwa chama kimoja na tena kweny tiketi moja ya mtu na makamo wake basi imani ya ya kisiasa ilitakiwa kuwa moja, kama sivyo basi mtuamb ia CCM sio chama cha siasa, ni kusanyiko tu la watafuta fursa
 
Well, siku ile tulivyompoteza Magufuli mi binafsi niliumia sana. Nilijua kama nchi tumepata hasara kubwa sana kumpoteza kiongozi wa aina ile. At the same time mi ni mtu wa imani: kufa kwa Musa hakukuwa mwisho wa safari ya kuelekea Kanaani, na kazi aliyoifanya Magufuli ya kujenga imani ya taifa haiwezi kufutwa na mtu mmoja tu pale Magogoni. The man can rest in peace, maana somo lake lilieleweka, hata kama si kwa wale waliokuwa wasaidizi wake wa karibu.
 
Mfuasi wa mwendazake???

Unauliza CCM ni chama gani??

Kwa hiyo ndiyo maana mlianza kuunda CCM Mpya SK Gang ndani ya CCM siyo?

It is revealed, kwamba mlijenga kikundi cha wahujumu nchi kwa nia ya kupambana na CCM.

CCM ni taasisi kongwe, imara, yenye nguvu na isiyoyumbishwa na mtu awaye yeyote hata akiwa jiwe
CCM mbona ilimshangilia hadi ikampitisha kugombea muhula wa pili kwa kishindo na tena kutaka aongezewe muda wa mihula mingine zaidi kwa lazima?
 
Back
Top Bottom