Sisi Waafrika na extremes!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Huwa mara nyingi tunachelewa sana kujua mambo ukilinganisha na Dunia nje ya Afrika yetu ya Kusini mwa sahara lkn sasa tukishajua basi huenda extreme klk hata wale waliotufundisha!

Mifano iko mingi, kwenye lugha hakuna binadamu ambaye kwake lugha ya Kiingereza au Kifaransa, Kiarabu au Kireno inategemea na Mkoloni wake inapewa umuhimu kama Muafrika hili utaliona ukiongea na Mzungu hata kama ukifanya kosa kwenye lugha yake siyo ishu lkn Mwafrika anaweza hata kunywa sumu!

Hata ushoga unaruhusiwa sehemu nyingi Duniani lkn siku ukija kuruhisiwa kwetu Afrika Dunia itaomba pooo!


Ukija kwenye Dini hapo sasa ndiyo mwisho utafikiri Uislamu au Ukristo ulianzia kwetu, sisi ndiyo wajuaji wa Uislamu/Ukristo namba moja Duniani wkt Dunia nje ya Afrika washaanza kuzipotezea hizi Dini huku kwetu Kanisa Katoliki/Ukristo na Uislamu ndiyo dini zinazokuwa kwa kasi klk sehemu yoyote ile Duniani na watu wako tayari kufa kama vile Nigeria na Boko haramu!

Hata tu kwenye social media hizo instagrams na facebook utafikiri Zuckerberg alizaliwa Kisiju kwa jinsi tulivyozikumbatia!

Na sasa hivi tumejua maneno demokrasia, dikteta, fashist Mungu wangu, hapo sasa ndiyo kohozi limepata mkohoaji utakuta mtu ambaye hata familia yake tu hatoi haki kwa mke wala watoto wake lkn kwenye hili mtamalizana kwa utafikiri akina Plato ndiyo wamezaliwa jana Rufiji na wakatufundisha hili neno Waafrika tunakwenda extreme na hili klk hata Wagiriki wenyewe...
 
Back
Top Bottom