Sisi vijana wa Kusini mwa jangwa la Sahara tuwe na nidhamu (self discipline) kwenye maisha

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
4,042
10,463
Kwa utafiti ambao sio rasmi unaonyesha vijana wa kusini mwa jangwa la Sahara wanaongoza kuishi maisha yasiyo ya ndoto zao binafsi naunga mkono hoja hiyo nikiwa Mimi na marafiki zangu Kama mifano halisi.

Katika maisha yangu nilitamani siku moja kuwa mhandisi wa mitambo lakini sasa ni mlinzi, mume na baba wa watoto wanne nikiwa sijatimiza hata robo ya kile nilichokuwa natamani Kufanya katika hii dunia inasikitisha ila ndo hali halisi wanayopitia na vijana wengine wengi.

Ukweli mchungu Mimi Baba Morgan na asilimia kubwa ya vijana tunaoishi kusini mwa jangwa la Sahara hususani Tanzania hatuna nidhamu katika maisha yetu na sio ile nidhamu ya kumuamkia baba na mama asubuhi bali ni nidhamu ya aina ya maisha tunayoishi.

Mifano ya maisha yasiyo na nidhamu
1. Hatutaki kujibidiisha kwenye kazi tunasahau kuwa no pain no gain.

2. Hatujali afya zetu kwa kuwa na lifestyle isiyofaa kama kunywa pombe kupitiliza, madawa ya kulevya na kushiriki ngono zembe

3. Ni wepesi wa kulizika tunasahau kuwa tunahitaji kuboresha maisha yetu Kila siku.

4. Kuchukia wale waliofanikiwa wakati walipaswa tuwachukulie Kama watu wa kutupa amasa.

5. Kushindwa Kufanya maamuzi kitu kinachopelekea kuamliwa Cha Kufanya na wanao tuzunguka hususani wazazi.

6. Kukata tamaa hata kabla ya kujaribu

7. Kukosa mwendelezo hii utokea haswa Wana michezo Kama wachezaji leo amekuwa bora next day anaboronga

Mwisho nipende kujisihi na kuwasihi vijana wenzangu tuwe nidhamu.

From northern part of Tanzania.
 
Wa kwenye taasisi moja kubwa na maarufu huku mikoa ya kaskazini
East Africa Community, najaribu kuotea tuu, na kama ndivyo kulingana na hadhi na kiasi cha mishahara ya taasisi ile sishangai kwako kuzipotezea ndoto na mipango yako na kutujumuisha vijana wa kaskazini mwa jangwa la sahara kuwa hatuna adabu na nidhamu katika maisha na eti ndio sababu hupotea kwenye barabara ya ndoto zetu.
 
East Africa Community, najaribu kuotea tuu, na kama ndivyo kulingana na hadhi na kiasi cha mishahara ya taasisi ile sishangai kwako kuzipotezea ndoto na mipango yako na kutujumuisha vijana wa kaskazini mwa jangwa la sahara kuwa hatuna adabu na nidhamu katika maisha na eti ndio sababu hupotea kwenye barabara ya ndoto zetu.
You're wrong Mimi ni hungry fire ukubwa na umaarufu wa kampuni haina maana kuwa nakunja fungu kubwa bado naisoma namba tena kwa kirumi.
 
Back
Top Bottom