Sisi tuwe kizazi cha mwisho kufa kwa malaria

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,847
2,669
Ni kauli ya JK katika kampeni dhidi ya malaria. Najiuliza kizazi ni nini na kinaanzia na kumalizikia wapi. Kama ni vile ninavyofikiri, basi itatuchukua karne 4 kwa malaria kuisha, la sivyo, kauli ya rais ibadilishwe. Kizazi kinaanza pale mtoto anapozaliwa siku ya kwanza. Hadi akue na kufa ni miaka mingapi? Hadi hicho kizazi kitoweke ndio malaria itakuwa simulizi. Tueleweshane juu ya kauli ya rais
 
Jana niliisikia hiyo kauli nikajiuliza....! Kwahiyo JK amekubali sisi kufa kwa malaria? Kuna haja ya kulikubali hilo? Yaani kwa maneno rahisi it is ok kizazi hiki kufa kwa malaria!!!! Jamani hizi kauli mbiu nyingine huwa zinafikiriwa jukwaani au!!! Huyo ndio Rais wetu bwana! Tulimchagua kwa kura kedekede! Tz zaidi ya uijuavyo
 
Anashaurikaa kirahisii...Kauli ilinishangaza hata kama alitaka kumaanisha kuanzia sasa kusiwe na kizazi kitakachokufa kutokana na malaria..ingeelewekaa kidogoo lengo ni nn.

Kwa Mh Raisi hizo ni kauli tata na zisizofaa kutoka kinywani mwake..Inahuzunishaa washauri wake kuna wachambuzi hata wa lugha na mantiki zake.
 
Nyauba, wakati mwingine tunawabebesha washauri wa Rais mizigo isiyokuwa yao. Rais ni msomi hata kama anaandikiwa hotuba inabidi naye aipitie kwa makini na kuisahihisha ipasavyo kabla ya kuitoa. Hata kama anatoa hotuba off the cuff lazima awe amejitayarisha mentally kujua atasema nini. Si tunahusudu sana mambo ya Marekani? Basi Rais wetu angalau angejifunza kutoka kwa 'mwenziwe' Obama ambaye mara nyingi hasomi hotoba kutoka kwenye makaratasi ila zinatoka kichwani kwa mtiririko murua usio na maswali!
 
Za obama huwa hazitoki kichwani moja kwa moja. Kuna teknolojia hutumika. Ila obama ni kichwa. Kwa JK tatizo yuko bize sana kiasi cha kumfanya mambo mengine ameze na kuyatoa kama yalivyo
 
Za obama huwa hazitoki kichwani moja kwa moja. Kuna teknolojia hutumika. Ila obama ni kichwa. Kwa JK tatizo yuko bize sana kiasi cha kumfanya mambo mengine ameze na kuyatoa kama yalivyo
Jk hayuko busy kama Obama ila sio mtu wa kusoma na kufuatilia utendaji wa serikali kwa umakiniiii..

Ni tabia yake kama binadamu asiyependa kusoma na kujishughulisha kama kiongoziii...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom