Sisi tudai Tume mpya ya uchaguzi, If not ....!

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,942
3,819
Nalisema hili isitokee kama wale wanaoshtukizwa na teuzi,tumesikia wakipashana kuwa wale wanaojipanga kwa nafasi ya Uraisi hapo 2025 wasahau !!!

Hili la wanaojipanga kugombea 2025 waache tabia hio mara moja ,sijui mlilisikia na kulichukulia poa ila hilo ni lao ,huku upinzani ni lazima juhudi za makusudi zichukuliwe ili kuanza kudai tume huru au iliyo huru kuhusiana na mambo ya uchaguzi tusisubiri kesho uchaguzi, ndio inakuwa kama tunaotoka kwenye usingizi mzito na kuweweseka kuwa tume sio huru.
Hii tume iliyopo ivunjwe na iundwe tume itakayopewa dhamana ya uchaguzi wa Nchi hii anaeshinda awe ameshinda kwa haki kabisa kama akivurunda au kuvuruga hilo itakuwa hakuna wa kulaumiwa, na wananchi watabeba mzigo wao wenyewe . leo tunaona kila kitu viongozi wanabebeba lawama kuwa hawakuchaguliwa na wananchi ndio maana wanafanya wanavyotaka na hakuna wa kuwalaumu.

Tume huru ndio muamuzi wa maisha ya watanzania na sio genge la wachache ndaniya CCM lilioiteka nchi hii.

Wakuu wa vyama vya upinzani sasa kazi kwenu kuanzisha sekeseke la kudai tume huru ya UCHAGUZI ,serikali ya CCM isipewe muda wa kurilex na kujifaragua ni lazima iendeshwe puta na mchaka mchaka ndivyo upinzani ulivyo,tumechoka na vitendo vyenu vya kuita vyombo vya habari. Imekuwa sasa ndio itikadi yenu.
 
Point!
Haya Mateuzi ni sawa na wafu kuzika wafu wao, sisi tunahitaji katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, bunge lenye nguvu na mahakama iliyohuru!
 
Wakuu wa vyama vya upinzani sasa kazi kwenu kuanzisha sekeseke la kudai tume huru ya UCHAGUZI ,
Hapo ndipo mnapofeli
Yaani uneshindwa kabla ya kuanza, pale tu ulipowaamuru na kuwapa kazi ya kudai Katiba wakuu wa vyama vya upinzani.
Tanzania hakuna upinzani,Kuna waganga njaa ,wakiishiwa wanachukua familia na kukimbilia malisho Bora nje ya nchi
 
Point!
Haya Mateuzi ni sawa na wafu kuzika wafu wao, sisi tunahitaji katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, bunge lenye nguvu na mahakama iliyohuru!
upo sawa kabisa leo akiteuliwa huyu wapinzani nao wamo kushangiria au kuunga mkono au kupongeza ,kuna upinzani hapo ? Huko hata wakichagua na wachina ndani ya wizara zao na serikali yao ni mipango yao, kama wanaunga au wanavunja sheria na katiba ,tufahamu hawakuanza leo ni mila waliyorithi kutoka tawala iliyozopita "HAWAHESHIMU KATIBA" ,sasa unapiga makelele fulani si Mtanzania mwengine anasema ni Mtanzania ,sisi wapinzani itatusaidia ??? Huoni badala ya sisi kuwakeep bize na mambo ya Tume mpya ya uchaguzi na pia katiba ,sasa wao wanatukeep bize na mambo yao ya ndani, wanatuhamisha kwenye reli.

Wajamani hayo ni yao ndani ya Chama chao,wakivuana nguo hata kupinduana ni yao,upinzani hayatuhusu kabisa,nimemshangaa sana Zitto Zuberi Kabwe kulivalina njuga kuwa jamaa ni mkigoma na si mburundi kama ni hivyo advantage kwa upinzani, waachwe wapapatuane wenyewe.

Ni wakati mzuri sasa kwa Vyama vyetu hivi vya upinzani kuwa kitu kimoja katika kuidai Tume huru ndani ya nchi na hata kimataifa ,si wakati wa kushiriki katika mchezo wa teuzi zao na kutufanya sote kama misukule wakichaguana wao sisi tunachakarika na teuzi zao.
Punda ni yuleyule CCM wamebadilisha mpandaji tu.

Tususeme ni mapema kwani muda unaenda kasi sana huyo hapo Magu juzi tu amekuwa Raisi leo hatunae ameondoka kwa speed ya mwendo kasi,

Hivi Mungu akimpenda mtu humuondoa duniani wacheni kumsingizia Mungu ,eti sisi tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi. Uongo mkubwa kuliko yoye hapa duniani ni huo.
 
Hapo ndipo mnapofeli
Yaani uneshindwa kabla ya kuanza, pale tu ulipowaamuru na kuwapa kazi ya kudai Katiba wakuu wa vyama vya upinzani.
Tanzania hakuna upinzani,Kuna waganga njaa ,wakiishiwa wanachukua familia na kukimbilia malisho Bora nje ya nchi
Ni sawa kabisa unayosema,ila ukumbuke sio kila siku ni Ijumaa ,Na hakuna aliekimbia dunia ya leo hakuna pakukimbilia,
Tume ni lazima kudaiwa na kutoa misimamo kama Jogoo la alfajiri.
 
Back
Top Bottom