Sisi ni watu wa ajabu! Sukari haitutoshelezi, tunaiuza nchi za nje na kuinunua tena kwa bei kubwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sisi ni watu wa ajabu! Sukari haitutoshelezi, tunaiuza nchi za nje na kuinunua tena kwa bei kubwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkeshaji, Mar 11, 2011.

 1. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wakuu Salaam,
  Nimekuwa nikishangazwa sana na jinsi nchi yetu ilivyoacha mambo mengi yajiendee yenyewe. Vitu vingi tumeviacha vijiendee hasa katika sekta ya uwekezaji, kipekee ile inayomilikiwa na wageni.

  Zao la sukari: Uzalishaji, Usambazaji na Upungufu wake sokoni:
  Kumekuwa na upungufu mkubwa sana wa sukari katika soko la hapa nchini kiasi cha kuwapa upenyo wafanyabiashara kuongeza bei ya zao hilo kwa kiwango cha kutisha.

  Katika hotuba yake rais kikwete aliongelea pia suala hilo. Alitaja sababu za kuongezeka kwa bei ya zao hilo na kutaja kile ambacho serikali imekifanya katika kuhakikisha bei ya sukari inashuka kutoka sh. 2000 ya sasa na kufikia sh 1700, bei ambayo hadi sasa haijashuka tofauti na maagizo ya rais.

  Tukiangalia kiundani zaidi suala hili ni kuwa si kweli sukari inayozalishwa nchini haitoshelezi mahitaji ya ndani kiasi kwamba tunalazimika kuagiza nje ya nchi. Sababu ya kwamba katika msimu wa mvua viwanda vya sukari vinafungwa kwa ajili ya matengenezo ni ya kweli kabisa, lakini si kweli kuwa hiyo ndiyo inayosababisha upungufu wa sukari nchini. Utaratibu wa kufunga viwanda vya sukari kwa ajili ya matengenezo makubwa unahusu viwanda vyote vya sukari dunia nzima si Tanzania pekee. Tena vingine huwa vinafungwa kwa takribani miezi minne hadi sita tofauti na Tanzania ambapo huwa vinafungwa kwa miezi miwili hadi mitatu. Na katika kipindi hicho cha matengenezo, huwa kuna shehena kubwa sana ya sukari ambayo inaweza kutosheleza mahitaji ya ndani hadi hapo msimu wa uzalishaji utakapoanza upya.

  Mojawapo ya sababu zinazosababisha upungufu mkubwa wa sukari hapa nchini ni uuzaji wa sehemu kubwa ya sukari inayozalishwa hapa nchini katika nchi za Ulaya. Kampuni ya sukari Kilombero kwa mfano, ina mkataba tangu mwaka 2006, wa kupeleka tani za sukari zisizopungua 30,000 katika umoja wa nchi za ulaya. Kiwango hiki kilitakiwa kuwa kinaongezeka kwa takribani tani 10,000 kila mwaka baada ya mwaka mwa kwanza. Katika mkataba huo pia wamekubaliana kuwa sukari inayopelekwa ni lazima iwe na kiwango kikubwa sana cha "molasses". Molasses ni kiwango cha utamu kwenye sukari, hivyo kadri molasses inavyokuwa nyingi ndivyo sukari inavyokuwa tamu na uzalishaji wake huchukua muda mrefu zaidi na kuongeza gharama ya uzalishaji. Sukari ikiwa na molasses nyingi zaidi unaweza ukaizalisha tena "reproduce" na ukapata tani nyingi zaidi ya zile za awali. Kwa kila kilo moja ya sukari ya aina hii unaweza ukapata kilo moja na robo hadi kilo moja na nusu ya sukari ya kawaida baada ya ku-reprocess. Na huu ndio ujanja unaotumiwa na nchi za ulaya. Hivyo wakinunua tani 30,000 wana uwezo wa kupata hadi tani 40,000 ambazo baadae wanatuuzia tena kwa bei kubwa zaidi. Na huu ndio utandawazi.

  Swali langu ni moja tu:
  Kama sukari haitoshelezi matumizi yetu ya ndani, kwa nini tunauza sehemu ya sukari yetu tuliyonayo halafu baadaye tunanunua tena kwa hao hao tuliowauzia tena kwa bei kubwa zaidi?
   
 2. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  ...ndani ya sirikali hii ya CCM, who cares!! Syndicate ya kuiba tu!! Honestly,ni nani anayeogopa kauli/maagizo ya JK kwa sasa??? Hawana moral authority hawa jamaa!! Walikopa/saidiwa mabilioni ya shilingi na hao wafanyabiashara sasa wanataka kurejesha pesa zao, so wanafanya kile cha faida kwao na hawa manyang'au hawana moral authority ya kuwaambia nini wafanye!!
  THE WAY FORWARD: LET'S MEET AT OUR OWN TAHRIR SQUARE!!
   
Loading...