Sisi ni wapambanaji kweli au wasindikizaji - amua mwenyewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sisi ni wapambanaji kweli au wasindikizaji - amua mwenyewe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 24, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Sijui kama kweli tunataka mabadiliko au tunaombea mabadiliko yatokee. Sijui kama tunafanya ili kusababisha mabadiliko au tunasubiri wengine wafanye ili tufurahie mabadiliko; Sijui hata kama tunajua vizuri ni mabadiliko gani hasa tunayataka na kama tunataka ni juhudi gani tumezifanya kushiriki kwenye mchakato wa kuleta mabadiliko hayo.

  Tunaweza kubishana vijiweni na kwenye mitandao na kujaribu kubadilishana mawazo mchana kutwa na usiku kucha lakini mabadiliko hayaji kwa kusema. Mabadiliko hayaji kwa kupigiwa magoti au kwa kukemea giza usiku. Mabadiliko husababishwa na kutekelezwa.

  Tukijifunza kwenye kampeni ya Obama utaona kuwa Wamarekani hawakuombea tu kuwa kiongozi mzuri au wamtakaye aje na alipojitokeza hawakukaa pembeni kuombea kuwa afanye vizuri ili hatimaye "alete mabadiliko" wanayoyataka. Wamarekani walishirikishwa katika kampeni kuanzia kuchangia fedha, muda wao, vipaji vyao n.k


  Je kwanini tunafikiri sisi Tanzania tutapata mabadiliko kwa kubishana vijiweni na kwenye mitandao na kuoneshana nani anajua nini na anahusika na nini? Mabadiliko ndugu zangu hayaji kwa kunuia au kuwa "kusudio zuri" au kwa kujua ufisadi ulivyo mbaya na fisadi ni nani!!

  Mabadiliko huletwa na watu waliokusudia kuleta mabadiliko hayo.

  Nisikilize:

  [mp3]http://mwanakijiji.podomatic.com/enclosure/2009-08-23T18_12_10-07_00.mp3[/mp3]
   
  Last edited: Aug 25, 2009
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135


  Simple answer is that most people can talk the talk but can't walk the walk. Ni sawa sawa na baadhi ya viongozi ambao wana pinga ufisadi kwa maneno lakini hawafanyi chochote cha maana kuudhibiti. Watanzania tumezidi sana kupay lip service kutoka kwa viongozi mpaka wananchi wa kawaida. Kudebate is a starting point but what we do after our debates here on JF or else where is what really matters and counts. Ni sawa sawa na upige kelele kiongozi fulani hafai lakini ikija siku ya kupiga kura hauendi kumpinga kwa vitendo unaishia kulala mika tu kwa nini kashinda tena.
   
 3. S

  Shamu JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watu washapiga hizo kura na matokeo ya kabadilishwa. CCM na Serikali yake, na hao viongozi hawawezi kuondoka kwa njia ya KURA. Viongozi (Mafisadi) wetu wako tayari kufanya jambo lolote ili imradi wakae madarakani. WTZ hatuna mtu kama Martin Luther King au Gandhi. Kitu kilichobakia ni kupandikiza watu ndani ya CCM in order kuleta mabadiliko.
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,555
  Likes Received: 18,247
  Trophy Points: 280
  MMKJJ,Huu ndio utamaduni wetu Watanzania, we just sit and watch as the movie unfold, mambo yanapokwenda ndivyo sivyo, tunaishia kulalamika.Mfano mzuri ni kinachoendelea sasa kati ya CCM na Spika, no one has a daring guts za kufanya chochote zaidi ya to sit and watch.Hata miongoni mwa ile first 11 yake ya Mwakiembe etc, none of them has the gut to act on anything zaidi ya to sit and watch.CCM inahodhiwa na mafisadi tena wana nguvu za kikweli kweli. Kuna uwezekano 2010 Siitta na first 11 yake hawatasimamishwa kugombea kwa tiketi ya CCM, utashudia jinsi baadhi yao watakavyo just sit and watch kwa sababu kwao siasa ni oportunities na sio leadership streghths.Hata CCM iwe imeoza vipi, oportunists watavumilia uvundo kwa sababu they can't risk loosing the oportunities, they better sit and wait mpaka wakikumbukwa tena.Watanzania tu wapenda amani na utulivu, sitting and watching ndio order of the day na inapobidi silaha yetu kubwa ni kuzungumza na haswa kulalamika.Mungu ibariki Tanzania.
   
 5. Lighondi

  Lighondi JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 585
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  You are absolutely correct. I second you!!!!!

  Hii kitu nimeifikiria siku nyingi sana. Nadhani ile falsafa ya jino kwa jino tunaweza kuitumia vizuri hapa. Kama pande hii ya GREEN inapandikiza kule kwa rangi nyingine, kwa nini na wale wa rangi zingine wasipandikize huku kwa Green??

  Njia ni ndigo tu, unajifanya unarudi kundini then unafanya mambo na mwisho wa siku 3 bila.
  Kwisha habari yake!!!

  Wazee mmesahau ule ujumbe wa wahenga kuwa ukishindwa kupambana nao (kutoka nje) basi ungana nao (fight from within)
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Aug 24, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mzee Mwanakijiji,
  Mkuu wangu nitakueleza zaidi uzembe wa mwafrika... na hasa Mtanzania. Ni jana tu nilikuwa nimekaa barazani na mshikaji wangu tukipiga domo tukisubiri muda wa futar, unajua tena wengine ndio tupo ktk funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhan..naomba unisiome vizuri mkasa huu maanake una shadidi zake..
  Mbele yetu tulipokaa kuna njia panda ya njia nne, yaani makutano ya barabara mbili..na hakuna traffic lights ila stop sign pande zote nne za barabara..

  Basi tulikaa kwa muda mrefu sana tukizungumza mambo mengi ya dunia wakati huo huo tukitupia chapuo jinsi jamaa wenzetu (wazungu)walivyokuwa wakiachiana nafasi ya kupita bila kuwepo kwa askari wala mtu kuwaongoza...isipokuwa sheria ya udereva inayosema -First at the junction, has the right of!..
  Mara kadhaa magari yalijikusanya wakashindwa kupishana kwa dakika chache kutokana na kwamba pembeni ya makutano hayo kuna sehemu kubwa ya kuegesha magari (Parking Garage), hivyo kuna magari yaliyokuwa yakiingia ku park, menginew kutoka na bado kuna njia panda sehemu hiyo hiyo.. lakini hata hivyo mara zote waliweza kuachiana nafasi tena bila kutumia horn wala mtu kubwatuka kwa hasira na traffic ikaendelea bila tatizo kubwa...

  Mara mshikaji wangu akanidokeza na kuuliza what if hali hiyo ingekuwa Bongo... pale pale nika shift akili yangu na kufikiria sehemu kama hizi tanzania huwa vipi?..Nafikiri jibu unalo wala sina haja ya kusimulia maanake magari yetu ktk sehemu kama hiyo yangefunga kila kona na asiondoke mtu kwa sababu ya kuchomekea.. Kila mtu hutaka yeye kuwa wa kwanza kuondoka na mara nyingi sana utagundua kwamba traffic kubwa Tanzania sii swala la kuwa na barabara ndogo au magari mengi wakati wa rush hours isipokuwa uendeshaji wa magari Tanzania ni kinyume cha taratibu, ustaarabu na mara zote tunakwama kwa sababu kila mtu ni mjuaji zaidi ya mwingine. Hivyo mara zote tunapokwama ktk traffic na hasa njia panda sii kwamba watu hawa hawajua wanapotaka kwenda isipokuwa huwekeana kizuizi sisi wenyewe na hatuwezi kuondoka hadi traffic aje kuongoza magari moja baada ya jingine hadi njia itakapo funguka..

  Sasa nini mahusiano ya kile tulichokiona jana na mada hii tunayozungumzia maswala ya kubishaa na kadhalika..
  Mkuu wangu mara nyingi ni rahisi sana kumwona mtu mwingine mbishi na mbovu wa kufikiri ikiwa tu wewe mwenyewe utaweza kutazama vituko hivyo ukiwa pembeni kaa tulivyokuwa tumekaa sisi pale barazani tukitazama magari..Lakini mara zote wale wanaohusika ktk vituko hivyo, yaani wale wanaoendesha magari na kujikuta wamekwama ktk junction wakichomekeana magari kila mmoja wao humwona mwingine ndiye mkosefu na kibaya zaidi kwa kila inchi ya ardhi inayoachwa wazi mtu mwingine husogeza gari lake..Matokeo yake traffic hukwama pande zote wakashindwa wote kwenda wanakotaka kwenda ktk wakati waliokusudia..

  Hii ndio hulka ya Mtanzania hata katika maisha yetu iwe Uchumi, maisha ya kawaida ktk kuparamia daladala kulima kula na kadhalika yaani kila kitu tunachofanya ni vituko vitupu hakuna maarifa, busara wala hekima. Tunapuyanga tu na tunapokwama mara zote hatuwezi kutatua matatizo yetu hadi atokee mtaalam toka nje kutusawazisha Huyo (Traffic Polisi)..
  Muda tunaochukua kuparamia daladala kama tukipanda kwa utaratibu watu watakao ondoka ni hesabu ile ile, kuparamia hakuongezi hesabu ya watu, ukubwa wa bus wala kuharakisha safari, isipokuwa kuchelewesha, kukaribisha wizi, (ufisadi) na kuchosha wasafiri maanake ukisha ingia ndani ya dalaldala energy yote imekwisha....

  Ukitazama hata Kula chakula, Mdanganyika huwezi kupima tonge lake ..yaani anafukanya utadhani kachangia na mtu sahani yake, tonge tatu tu kafuta sahani nzima within minutes mkuu anatafuta maji.. Lakini ukifikiria kwa makini, mtu akila matonge kumi au matatu hakuna tofauti yoyote ktk kuzidisha au kupunguzxa kipimo, nutrition au muda wa digestion..ya chalula alichokula. Pengine utafikiria ni muda labda anaharakisha apate kurudi kazini haraka, utaambiwa hapana.. Mtanzania lazima apate a nap kila anapomaliza kula chakula cha mchana - at least half hour!..

  Kwa hiyo baabu kujaribu kufikiria maswala ya mstkabali wa tanzania ni kazi ambayo inategemea wewe unaendesha gari lako wapi (Mazingira) na kuna WATU gani nyuma ya Usukani wa magari mengineyo..
  Ni imani yangu kwamba hadi siku tutakapojifunza discipline, tukaheshimu sheria na taratibu zote.. tukatumia akili zetu kuelewa umuhimu wa ubunifu na matumizi ya elimu ktk utendaji kazi wetu..ndipo tunaweza kutegemea mabadiliko ya aina yoyote ile lakini kama tutaendelea kufikiria kwamba tunaweza kubadilisha maisha yetu kwa kuendelea kuchomekeana ktk njia panda... hakuna mtu atakayetoka..
   
  Last edited: Aug 24, 2009
 7. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2009
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,498
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Mkandara;
  Sjui pengne labda mimi akili yangu iko kwenye low level sana. Yaani leo kabisa umekuja kubomoa mada. for the first time nimeshindwa kukuelewa. Anyway pengine leo umeamka vibaya hujaweza kutumia busara yako ya siku zote, maana siku zote huwa hazilingani. Mwenzio kaanzisha mada kwa point na kwa nia njema kabisa, wewe unaleta mchango wako uliojikita kuwasagia watanzania wenzako wanaohangaika. Sijwahai kuona Mwanakijiji anatoa michango kama uliyotoa wewe hapa. Anyway I respect you ila nisingefurahi sana kuona mchango mwingine wa aina hii kutoka kwako. Watch your words! Unless uniambie uko SUPERIOR au INFERIOR, then nitakuelea na kuanza kukutafutia msimamo mpya nikuweeke wapi. Goodday
   
 8. E

  Engineer JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji,

  Unajisumbua bure kwamba wana JF watafanya mabadiliko kwa kumuunga mtu mpya ambaye hawamfahamu.

  Tumezidishiwa ubinafsi na wivu katika mambo yetu yote na hicho ndio kilema kikuu cha sisi Watanzania.

  Huku vijijini mtu akifanya jambo lolote la maana watu wataweka majungu tu. Badala ya kuiga na wenyewe wakafanya makubwa zaidi ya hayo wao ni majungu na wivu tu.

  Hata hapa JF tumeona siku za karibuni jinsi wana JF hawa hawa walivyoamua kuwabomoa baadhi ya wana JF wenzao kwa kutumia majungu.

  Sisi kazi zetu ni kuimba nyimbo zile ambazo tayari zipo. Kama Dr. Salaa kajitengenezea jina lake basi sisi tutaanza kuimba wimbo huo huo. Akitokea kijana mdogo kama Zitto anataka kumpinga basi hapo kutakuwa na maneno kibao na kila sababu ya visingizio.

  Amkeni na nendeni kufanya mabadiliko kwenye sehemu zenu badala ya kukaa hapa tu na kuandika mbovu mbovu.

  Kumbukeni Obama hakuwa na jina kubwa kabla ya kuanza kugombea. Watu waliona ana uwezo lakini hakuwa tested kabla ya hapo na bado walimwunga mkono na kuwaacha wenye majina. Mabadili hayaji kwa kufuata mambo yale yale.
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  Aug 25, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  tatizo hao 'wapiganaji' wakereketwa wengi wako ughaibuni. sasa ni kama kitendo cha mtu kutupa mawe gizani. mje bongo muonekane kama wanasiasa na wataalam wengine. kutumia remote control si jambo la msingi
   
 10. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #10
  Aug 25, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mkuu pole sana kwa maandishi haya ya uchungu, ila utambue kuwa katika safari ya mamba..... ndiyo maana japo unaona kama ze comedy , bado tunao na tutakuwa nao baadhi ya watu kama MKJJ, invisible n.k,,,,


  Kuna wakati nimekuwa hata nikianzisha maada za uchokozi ili nione mwitikio na mawazo ya watu, sijafanya hivi kwa nia mbaya ila nijue sisi kama JF wengi wetu tunawakilisha jamii kubwa ya watanzania.tulivyo hapa ndio walivyo wasio na access za internet.

  1. Mwanakijiji amepiga msumari ambao inabidi baadhi ya watu kujiangalia tena kama vita hii ni ya watu fulani, kila mtu au kupotozeana muda.

  acha nitoe matatizo yetu watanzania wengi.

  1. Ubinafsi

  2.kutaka kujionyesha,kujikomba

  3.kutokujali na kuona tatizo fulani ni la watu fulani tu na si yeye,mathalani, jamii kubwa ya graduates hawana mpango na siasa, wakinunua magari ya mkopo na kupanga sinza wameshamaliza kila kitu.

  4. Idadi kubwa ya wanawake ndiio kabisa , ktk serikali nzima wanamjua JK tu!

  5.Inaonekana kuna upofu wa raha za muda Tz, tunasema tuna amani, chakula, n,k hatujafika level ya shida kiasi cha kumfanya kila mtu ashtuke na kuwa serious kuchagua kiongozi atakayetatua matatizo na sio 'bora liende'

  6.Hatuna elimu ya ukombozi wala ya kufikiri, hatuna masomo ya mazingira na uongozi tangu utotoni, HATUNA CULTURE

  7.tuna hesima ya woga, hatuna tabia ya wazi na maamuzi huru katika maisha ya kila kitu, hii inapelekea kuwa wanafiki katika vitu vingi sana kuanzia dini,uongozi na mahusiano yetu na wengine.

  8.Kujidharau na kutukuza wazungu na kila kitokacho nje,

  Tumebinafsisha kila kitu ikiwemo utamaduni, akili, uhuru, mali asili, elimu, mpaka huduma za jamii, ili hali mtanzania halisi mwenye uwezo mkubwa kufanya kila kitu haonekani!


  Hayo hapo juu kwa namna moja ama nyingine inapelekea katika nyakati kama hizi, wachache sana walio serious katika vita hii ya ufisadi kumbuka.

  1. kutokana na ubinasfi wengi wanaangalia maisha yao.
  2,kuotkana na kutoguswa direct na shida za wengine hii inawafanya watu wajisahau sana.
  3.umbea, majungu, unafiki, na kutokusaka majawabu ya matatizo .


  Hii inaweza kuonwa katika.

  1.viongozi kuwaza kununua magari ya kifahari mno, wakati jamii kubwa ni maskini. haiingii akilini!
  2.harusi za mamilioni ya shilingi, kwa watanzania wengi ili hali jamii bado ni maskini na tungeweza kutumia fedha hizi katika mambo ya maana kama elimu, matibabu , kupanda miti n.k
  3.kuishi maisha ya kifahari DSM wakati kijijini kwenu biharamulo kwa madale wanateketea kwa shida.
  4 we are not using our own researchers and other professionals to solve our own problems!

  Hili hapa JF tunaliona kwa.

  1. Kuchangia maada juujuu bila kufikiri.(kutowaza)

  2, Kudharau mawazo ya wengine(kujiinua)

  3.kuchagua nani kaanzisha thread then mtu achangie, kama hufahamiki ....pole

  4.kutoangalia mambo in 3 Dimensions, kutochukuliana na kutaka kumuelewa mwenzako ana maanisha nini.

  5.Kutoa mawazo ya kufungamana na ufisadi kwa namna yeyote ile, kutokuwa WAKALI NA ufisadi.

  6.Kugeuza forum kama kijiwe na si sehemu ya kutoa ufumbuzi,

  7.kutoangalia mzizi wa tatizo,JF time is up to talk about individuals ufisadi uko kila kona kuanzia nyumba tulizopanga, owners wengi ni mafisadi MAPINDUZI YAANZIE MITAANI, KIJIJINI, KATA, WILAYANI, TAIFANI, kumsema Rostam mwizi mkubwa aliyeua watu 1000 (indirectly) ni sawa kabisa na kumsema mwizi wa dawa aliyeua watu 5 kijijini kule kabale vita ya ufisadi iwe kama unapuliza dawa ya kuua wadudu ndani hujui na itamuua! nchi ilishajisahau thats why was not hard for Chenge kwenda kuweka bilioni ulaya!

  8. Kutoa mawazo ya kichovu, kama tusubiri kuwaondoa kwa kura (huku tume ya uchaguzi yao)

  9. Kuchekacheka na mafisadi na kuwaita baadhi ya wana CCM wasafi, kana kwamba ufisadi nikuchafuka na vumbi au kutoa ushuzi bahati mbaya

  10. Kutokutilia mkazo katika thread zote zenye lengo la kutukomboa, bila kujali nani kaanzisha HII INATOA PICHA 'PEOPLE ARE SERIOUS AT WORK' wala sio kijiwe kuwa kama fulani asipokuwepo basi JF haipo!

  11. Any sense ya kubaguana humu kwa namna yeyote inatoa picha kuwa
  a. ni tatizo la jamii kwa rais (viongozi) wa nchi kuchagua washkaji wake au ndugu
  b. Ni tatizo la jamii kwa rais (viongozi) kutotilia mkazo mabo yote, kwa upeo, uzito sawa na kujali misingi muhimu ya maendeleo
  c.Nitatizo la jamii kubagua na kutosikia mawazo ya watu wengine hasa wasiofahamika!


  Tiba jumlisho:

  1. Tulinde utamaduni, utakaopelekea sisi kutambulika kama taifa na sio watu tu walijikusanya kwenye sehemu moja inayoitwa Tz, hawana katiba,utamaduni na taratibu walizojiwekea.

  2. Kwa akina baba, walimu, doctors, engineer in fields, waandishi wa habari ,polisi n.k ongeeni na watu wenu wa chini athari za ufisadi, umuhimu wa kuwa honesty na faida za kulinda mali asili za sasa na vizazi vijavyo

  3. Let us have sense that Tz is family rather than country , angalia nchi kama kama USA yenye watu milioni 300 see how they love their country,proud of etc

  4. Tuongee na wake zetu (waume) kuhusu siasa , cha ajabu kuwa wengi wa wake zetu they are not aware of whats going on, hawa ndio rahisi wakipewa kanga, kofia na mchele basi , hawaangalii in big picture, TUONGEE NA watoto wetu, kwenye sherehe this point is special for family level

  5. Tuangalie na kuweka strategy katika safari yeyote ya mapinduzi ni kichekesho mwakani kwa vyama vya siasa na wananchi kuingia kwenye uchaguzi

  1. Wakati katiba hajabadilishwa, nchi inatakiwa iwe na serikali ya pamoja yenye kushirikisha vyama vyote NCHI HII SI YA CCM.

  2.Kuwa tume ya uchaguzi iwe huru isiwe na upendeleo wa chama chochote

  3.Tukishaweka misingi muhimu ya kitaifa na si ya CCM au dini fulani, tukishaweka dira na ya kila ajaye hata miaka 1000 ijayo then this will be a country, KATIBA HAIGUSWI kiholela, wala haijadiliki pasi grouds muhimu (kadhi saga)

  SIONI SABABU KUINGIA KWENYE UCHAGUZI ili hali ukijua utashindwa.


  6,Vita ya ufisadi si ya kuchekeana wala eti kusema tutapigana ndani ya CCM, kama kuna CCM wasafi na mnatamani jina hilo undeni CCM B, hakuna usafi ndani ya mafisadi HAKUNA!

  7. Tusipoteze muda kuwaza na kuwasema individuals tuwaseme, lakini focus yetu iwe kwenye kutatua tatizo, mawazo ya wana JF wengi na umbea tu na sio kumaliza tatizo HAKUNA SULUHISHO LINALOISHI LA VITA YA UFISADI BILA KUMGUSA RAIS AU KUMPATA RAIS SERIOUS. UFISADI NI DHAMBI IJULIKANE HIVYO KWA KILA MTU, NA SIO KWA MIAKA 4 JK ANACHEKA NAYO, WE ARE NOT SERIOUS. WENGI MAFISADI WANAJIFICHA NYUMA YA ROSTAM NA LOWASSA MAANA NDIO TUNAOWASEMA KILA SIKU HUMU, ILI HALI WENGI WANAOLIPELEKA TAIFA PABAYA WAKO KULE HAWAJULIKANI

  8. If any possibe solution is not working then , iwe kama tunapigania uhuru, tuungane kwenye maandamano n,k JAMII FULANI LAZIMA ITESEKE ILI VIZAZI VIJAVYO VINEEMEKE NA VIWE PROUD ZAIDI NA NCHI YAO.kama taifa halikupatikana kwa nguvu, na kujitoa kwa mababu HAKUNA MWENYE UCHUNGU NALO, INAKUWA KAMA MALI YA URITHI NDIO TUNACHOONA SASA! Mkwawa aliweza karne ya 18!


  Kama kweli tunachukia ufisadi na tuna misimamo ni ngumu sana kuamini kuwa kuna wasafi ndani ya CCM, NA ITAKUWA VIGUMU KUAMINI KUWA SI MATUMBO YANAYOWAFANYA WAKE HUMO,. na sitaamini kuwa hawawezi wakafanya kitu kipya!

  Pamoja na tabia zetu za asili tusizozipenda tulizo nazo bado tutabaki watanzania wenye chellenge nyingi zilizo mbele yetu, tunahitaji viongozi wa kuielewa halii hii, wakatubadilisha kwa vitendo na kutupeleka katiika level mpya ambayo bado tutakuwa watanzania walio badilika kifikra,kimatendo watanzania wanaowaza kutunza mazingira,kulinda mali asili na kuwaza kila kitu kwa faida ya watanzania wote , uwezo huo hupo kamwe hatutakuwa wazungu wala wachina , wala si rahisi taifa libadilishwe jina, wala hatutaota tena tuchukuliwe utumwa, wanatutawala kwa mbali, wala tusiote watoto wetu kwenda ulaya kuishi THEY WILL BE SECOND HAND CITIZEN AND THIS HURTS!

  Tunaweza sasa do something !
   
 11. W

  WildCard JF-Expert Member

  #11
  Aug 25, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  MABADILIKO MAZURI na ya KUDUMU ni yale yanayokuja YENYEWE bila ya SHINIKIZO, CHAGIZO au KULAZIMISHWA. Kwa Tanzania mabadiliko haya hayako MBALI ili mradi tumeanza kuona wapi tulikuwa, tulipo na tunakojaribu kwenda. Tuvute subira tu na kutakiana HERI na AMANI. Bahati nzuri mabadiliko ya kuja yenyewe yanawaumiza wachache ambao wanajaribu kukinzana nayo.
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Aug 25, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Historia inaionyesha mapinduzi huja baada ya watu kuamua wanataka kuona mabadiliko. Hata hivyo lazima tujue there is a space between stimulus and response.

  Watu wengi zaidi wakiamua mabadiliko ndivyo inavyokuwa rahisi kutokea.Ninavyoiona jamii ya watanzania, taratibu wameanza kuzinduka kutoka kwenye usingizi mnene ambao tumepitia.Kwa wale walioko mstari wa mbele inaweza ikawa kama inakatisha tamaa kuona mambo hayaendi vile inavyotegemewa.

  Tukumbuke, sisi tulio wengi hata elimu ya kusoma na kuandika bado ni tatizo, na wakati wa uchaguzi sisi tulio na elimu ndogo tuna sehemu kubwa ya kufanya.

  Effect ya hii mijadala inayoendelea ni kubwa sana.Inawafanya watu kuanza kujua namna gani Taifa letu linatakiwa liwe. Badala ya kuchora mstari kwa sasa,tuongeze nguvu tukiamini kuwa mafanikio yapo tena hayako mbali.

  By the way, dukuduku hizi naona zimezagaa karibu Afrika nzima. sidhani kama viongozi wataendelea kukataa haja ya kufanya mabadiliko.
   
 13. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #13
  Aug 25, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Wengi wetu ni watazamaji na sana sana tunashabikia tu mambo yanavyokwenda.
   
 14. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #14
  Aug 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mabadilko yanawezwa yakaongozwa toka ughaibuni kama vile tulivyoshuhudia kule Iran na Ayatolah Khomeni.. Alifukuzwa na Shah na kwa kipindi kirefu harakati zake zilikuwa ughaibuni mpaka Shah Reva Parlavi akatimuliwa mwaka 1979. Ferdinand Marcos na utajiri wake akufua dafu kwa wimbi lililochochewa kwa kiasi kikubwa na marehemu Aquino (mme wake Corason Aquino) akiwa Ughaibuni huko USA.

  Ukiacha mabadliko ya kijeshi na yale ya vita vya msituni mabadilko ya kiraia yanahitaji vitu viwili muhimu.

  1) Uongozi wenye kuona mbali (visionary leadership) na ujasiri mkubwa (courage)

  2) Raia walio tayari kwa mabadiliko yenyewe (state of readiness)

  Hili la pili ni muhimu sana. Kule Ufaransa kwenye karne ya 18 wakulima walifanya mabadilko (French Revolution) wakashika dola kutoka kwa mabwenyenye lakini mabadiliko hayo yalidumu muda mfupi sana kwa vile wananchi hawakuwa tayari kuyalinda ili yadumu vile vile uongozi dhaifu ukachangia kuanguka kwa mabadilko hayo.

  Kuna wakati hapa kwetu kulikuwa na mazingira fulani ambayo pengine yangepelekea kuwa na mabadiliko kwa kiasi fulani. Mtakumbuka miaka ya mwanzo ya 1990 Mchungaji Mtikila alijitokeza na kuleta changamoto fulani na kusema kweli kidogo wananchi walizinduka. Kilichokosekana pale ni uongozi wenye vision madhubuti na matokeo yake wote tunayaona. Mtikila wa sasa sio yule wa zamani. Tulipoteza nafasi hii adimu.

  Nani asiyemkumba Augustine Mrema mwaka 1994/95 alivyoichachafya CCM. Unaambiwa na wazee wa CCM kwamba kama sio mvuto binafsi wa Nyerere na Mrema mwenyewe kukosa “vision”, mzee wa Kiraracha alikuwa anachukua nchi mwaka 1995. Pamoja na kwamba (with hind sight) nchi ilipona balaa fulani lakini wananchi walikuwa tayari kusema CCM sasa basi!

  Hivyo basi utona kwamba uongozi, tena wa mtu mmoja mmjoa ni muhimu sana. Mabadiliko yoyote hapa duniani lazima yawe na “kinara” kuanzia kwa Yesu Kristu na Mtume Mohamad (SAW). Kule Urusi Lenin alikuwa kinara wa kuondoa Ufalme kwa kimwinyi na tumemwona Gorbachev alivyobadirisha nchi hiyo tena. Mifano ni mingi mno hapa duniani.

  Anachokifanya Mwanakijiji na wengine sio kwamba tunapiga domo kwenye janvi na vijiweni. Kinachofanyika ni kutayarisha umma pole pole uzinduke usingizini ili ikitokea uongozi wa kuchochea mabadailko hayo basi wananchi wawe tayari kuyalinda na kuyatetea bila hivyo mabadilko hayo hayatadumu. Kule Burma (Mynamar) yule mama si alishinda uchaguzi lakini majenerali wakakataa kumpa nchi na raia wakafyata mkia mpaka leo anasota kifungoni? Nasi inaweza ikatokea hivyo.

  Hivyo MNKJJ kazi inayofanyika sasa hivi sio bure. Pole pole iko siku patatokea kiongozi hapa kwetu atakayewasha “cheche” ya mabadiliko na hatutarudi nyuma wala kuyumba. It is just a matter of time.   
 15. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #15
  Aug 25, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  And there is no a quick fix to the problems we currently face.Uvumilivu ni lazima uwepo, na juhudi za makusudi za kuelimishana maana bila elimu ya kujua nini tunataka, kazi ipo!!
   
 16. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #16
  Aug 25, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mzee Mwanakijiji,
  Shikamoo.

  Mabadiliko yoyote yanahitaji KIONGOZI ambaye anaweza kuwaunganisha wapambanaji na kuwaongoza hadi kufikia mafanikio ya vita vyenyewe. Akiwepo Kiongozi madhubuti wasindikizaji wote watamfuata nyuma na kumsikiliza. Katika kumsikiliza kunaweza kuundawa Kamati Kuu ambayo itasaidia kuratibu mikakati, kuwahabarisha wafuasi/wasindikizaji nini cha kufanya ili lengo la mabadiliko liweze kutimia. Ni kweli watu wanabishana sana kwenye mitandao, vijiwe etc etc lakini hakuna matokeo yoyote ya maana. Anatakiwa KIONGOZI atakayekuwa tayari kupaza sauti kwa uhakika kabisa kwamba mabadiliko yanahitajika na kutamka wazi kwamba yeye yuko tayari kuongoza mapambano hayo na anahitaji wafuasi.
   
 17. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #17
  Aug 25, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Umesema kweli, inabidi tujiulize nini kifanyike ili kuleta mabadiliko ambayo tunayaota na kuwafantasize kwenye keyboard zetu.
   
Loading...