Sisi ni wajamaa, kwetu ujamaa au ujamaa na kujitegemea ni imani

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Na Humphrey Polepole

Tunapoanza Mwaka Mpya wa 2019 nimeona ni vema tukaanza kukumbushana Misingi ya Taifa letu na hapa kwa umahususi nikizungumzia Itikadi yetu na namna inatupa mwongozo na hamasa ya kuwaletea maendeleo wananchi tukihudumu kama Chama na Serikali.

Mfumo wa Jamii

Tunaishi katika jamii ambayo tumejiwekea utaratibu ambao tunaufuata na kuuishi, tumesema katika nchi yetu tutajiundia Mamlaka ya Nchi, humo ndani tukaweka Serikali, Bunge na Mahakama. Lakini tukaenda mbele tukasema nani na nani watahudumu katika Mamlaka ya Nchi. Tukasema Katika Serikali tuweke viongozi watakaotoa uongozi kwa watumishi wa Serikali, viongozi hawa tutawachagua kutoka miongoni mwetu katika mchakato tutakaouita uchaguzi.

Tukasema tena katika Mchakato wa Uchaguzi tutaweka utaratibu kwamba kuwepo taasisi ambazo zitashindanisha Sera zao na Watu wao dhidi ya taasisi nyingine kisha wananchi watachagua taasisi mojawapo na watu wake ili kutoa uongozi. Taasisi hizi tumeziita vyama vya siasa na ndani yake kuna makundi kama matatu ya watu; kwanza kuna wanachama, pili kuna viongozi ndani ya vyama hivi na tatu kuna viongozi wa vyama hivi wanaohudumu katika Mamlaka za Nchi yaani ama Serikalini au Bungeni. Kundi hili la Pili na la Tatu kwa pamoja wanafanya kazi ya Siasa na huitwa wanasiasa.

Siasa na Wanasiasa

Siasa huwa ni utaratibu tuliojiwekea kufanya maamuzi au kufikia maamuzi kama jamii ya watu na katika namna ambayo kila mhusika kwa namna fulani hupata fursa ya kutoa mchango wake katika jambo tunalolifanyia uamuzi. Kimsingi siasa yaweza kufanyika katika wigo wa rasmi katika utaratibu tuliojiwekea au yaweza fanyika hata nje ya utaratibu rasmi, kulingana na ukubwa jambo lenyewe.

Siasa katika mfumo rasmi inaweza kuwa wakati tunaamua wapi ijengwe Hospitali ya Wilaya au Kituo cha Afya cha Kata, hakika tutakuwa na mjadala utakaohusisha Malengo, Shabaha, Mahitaji, Jiografia na kadharika, na hakika mjadala huu utajengwa kwa hoja na sababu zenye mashiko, hiyo ni siasa kubwa na wanaoshiriki ni wanasiasa.

Siasa yaweza pia kuwa katika ngazi ya mtu mmoja au watu kadhaa lakini si katika mfumo rasmi tuliojiwekea wa maamuzi. Mtu anapotaka kuposa mke kwa hakika itampasa kufanya mambo kadhaa, ukiacha kutathimini lengo la msingi kwanini apose mke, sharti atafakari malengo ya muda mrefu na mfupi, aweke shabaha katika jitihada yake, kisha atafute mposwaji (si zoezi jepesi), kisha atashirikisha nduguze na marafiki. Mpaka shughuli imekamilika imehusisha watu kadhaa na maamuzi kadhaa yamefanyika na yamezingatia ushiriki wa watu, malengo, shabaha na matokeo, hiyo ni siasa kubwa sana.

Watu wengi wanafahamu na katiba za vyama vya siasa zinathibitisha kwamba lengo kuu la vyama vya siasa na wanasiasa ni kushika dola au Mamlaka ya Nchi. Hili halina ubishi hata kidogo, ila aghalabu hatujatenga muda kutafakari nini huwa motisha, hamasa ama msukumo wa vyama vya siasa na wanasiasa kuutafuta uongozi wa Mamlaka ya Nchi. Jibu la swali hili muhimu, nini hamasa, motisha na msukumo wa wanasiasa wema kutafuta uongozi wa Mamlaka ya nchi ndio hutupeleka katika fikra zao, mawazo yao, tafakuri zao, Imani zao na namna zinawaelekeza kitabia na namna ya kutenda au kufanya uamuzi wakati wote ama wakiwa madarakani au nje ya madaraka (siasa) au kuutufuta uongozi wa Mamlaka ya Nchi.

Kumbe Itikadi ni nini?

Itikadi ya kisiasa ni ujumla wa mawazo, fikra, tafakuri, maono, misingi fulani, mafunzo fulani yatokanayo na uzoefu unaopimwa kwa wakati na vitendo yanayotaarifu na kuelekeza namna jamii ya watu, Chama cha Siasa, Serikali na mtu mmoja mmoja utendaji wake, mienendo yake, tabia zake na namna masuala yahusuyo ustawi wetu (maendeleo) yanavyoamuliwa na kufanyiwa kazi kwa maslahi mapana ya wote.

Kwa maneno mengine itikadi ya Chama cha Siasa inaelekeza na kutaarifu namna ambavyo Chama cha siasa kitaielekeza Serikali yake kufanya uamuzi juu ya jambo fulani. Itikadi ya kisiasa inaelekeza na kutaarifu namna ya kuenenda, hulka na tabia za viongozi (wanasiasa) katika Chama na Serikali. Itikadi ya Kisiasa ndio inataarifu umma namna ya kufikia malengo yao ya pamoja na kuupa umma hamasa ya mshikamano na ushirikiano katika kufikia malengo yao.

Hapa Tanzania Itikadi hujumuisha nini?

Hapa Tanzania tofauti na nchi nyingi, tunayo Itikadi ya Kisiasa ya Taifa na inatambulika na Katiba ya Nchi na iyo hiyo ndio Itikadi ya Kisiasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Ili tuwe na uelewa wa pamoja ni vema nikaeleza chimbuko la Itikadi ya Kisiasa ya Ujamaa na Kujitegemea ambayo Taifa la Tanzania na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaiamini na kuifuata tangu mwanzo, hata sasa na nina hakika miaka mingine mingi ijayo.

Watu wengi wamejaribu kuielezea Itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea lakini kwa hakika Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Awamu ya Kwanza, Rais Mstaafu wa Awamu ya Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenye heshima ya Baba wa Taifa amefanya kazi kubwa katika ujenzi wa Itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea.

Alikuwa mtu wa mwanzo kuweka bayana kwamba neno Ujamaa sio tafsiri ya moja kwa moja ya neno la kiingereza "Socialism". Ukisoma maandiko ya Mwalimu utagundua neno la Kiswahili la "Socialism" ni Usoshalisti na sio moja kwa moja ujamaa, lakini akaendelea kusisitiza kuna mfanano wa kutosha wa kimisingi kati ya Itikadi ya Ujamaa na Itikadi ya Usoshalisti. Nina hakika kwa mfanano huu ndio Mwalimu katika kutusaidia kuuelewa Ujamaa akasema kwa lugha ya Kiingereza "Ujamaa is Tanzanian Socialism" kwa maana ya Ujamaa ni Usoshalisti wa Kitanzania" [Tafsiri ni yangu].

Ujamaa wa Tanzania na asili ya neno lenyewe ujamaa linasadifu asili yake, udugu, familia, kaya au mahusiano ya karibu ya kindugu na kwamba jina hili lilichaguliwa ili kujenga fikra za watu wetu juu ya aina ya Sera zetu na zenye uasili wa Afrika ambazo tumeamua kuzifuata na zinazojengwa katika misingi ya ushiriki, kushirikiana, mshikamano na umoja kama ilivyo kidesturi katika familia au kaya zetu za Kitanzania na Kiafrika.

Je ni ipi misingi ya Usoshalisti (Socialism)?

Usoshalisti kama zilivyo itikadi nyingine inayo misingi yake na kwa kumrejea Mwalimu Nyerere nitaifafanua kama ifuatavyo;

Jamii yoyote inayoamini katika usoshalisti jambo kubwa ni lazima iamini kwamba shughuli zozote za kijamii zinamlenga Binadamu (Mtu). Na kwamba neno binadamu linamaana ya Binadamu, mtu mume na mtu mke, bila kujali hali yake ya uchumi, rangi yake, Imani yake, wakati wote itambulike binadamu wote ni sawa. Zaidi ya yote lazima ifahamike kwamba shughuli yoyote ile ni lazima kusudio lake liwe mtu, Mwalimu Nyerere anasema hakuna faida ya kuzalisha, kuutukuza utaifa wetu bila kwanza kutambua kuwa lengo letu ni ustawi wa mtu (Binadamu).

Usawa wa binadamu ni msingi mwingine wa usoshalisti, na kwamba mtu yeyote anayeamini katika usawa wa binadamu huyo ni Msoshalisti. Jamii yoyote ni lazima katika mifumo yake, taasisi zake ihakikishe ya kwamba kuna usawa wa binadamu na wakati wote wanajitahidi kuondoa unyanyasaji wa aina yoyote baina ya mtu na mtu.

Msingi mwingine wa usoshalisti ni utu wa binadamu, jamii yoyote ya kisoshalisti ni lazima ilenge kukuza utu wa binadamu. Utu wa binadamu ndio unatutofautisha binadamu na wanyama, ndio unafanya tunavaa nguo, kukaa kwenye nyumba, kuandaa chakula na kadharika. Utu wa binadamu ndio unafanya tunasaidiana na kuinuana kila inapobidi, utu wa binadamu unakuwezesha na kukuhamasisha kusaidia hata watu wasio wa jamaa yako.

Demokrasia ni msingi mwingine wa jamii ya kisoshalisti, Mwalimu anasema lazima taasisi za kisiasa zizingatie usawa wa binadamu na kwamba Serikali katika jamii ya kijamaa lazima itokane na watu na ishirikishe watu. Katika jamii ya kisoshalisti Mamlaka yote ya nchi itatokana na wananchi na kwamba utawekwa utaratibu ambao utawezesha wananchi kufanya uamuzi juu ya nani atawaongoza.

Katika jamii ya soshalisti demokrasia haimaanishi tu uchaguzi bali wananchi kuwa na uhuru wa kuchagua viongozi wao na viongozi wao kuwezeshwa kushika hatamu ya uongozi katika taasisi na sekta mbalimbali. Ifahamike pia uongozi wa kitaasisi, kisekta na kijamii ni lazima ulenge kuhakikisha wakati wote kuna usawa wa binadamu, hiyo ndio demokrasia ya jamii ya kisoshalisti.

Jamii ya kisoshalisti lazima iwe na watu wanaofanya kazi na wanaotambua kazi ni kipimo cha utu. Katika jamii hii ni lazima mali na utajiri unaozalishwa na jamii lazima uwe na mchango wa kila mmojawapo ya wanajamii wenye uwezo wa kufanya kazi. Katika jamii ya kisoshalisti ambao wanaopata msamaha wa kutokushiriki katika kufanya kazi za uzalishaji za pamoja ni watoto wadogo, wazee na wagonjwa, wengine wote wanaobaki ni lazima kufanya kazi, ni haki na ni wajibu.

Na tafsiri ya watu wanaofanya kazi ni zaidi ya wafanyakazi wa maofisini na viwandani bali kila anayefanya kazi halali na inayomletea kipato au kumwezesha kuishi (hii yaweza kuwa kilimo, biashara, uvuvi, ufugaji n.k). Ni jukumu la jamii kuhakikisha inawezesha kila mwenye uwezo wa kufanya kazi kuipata fursa ya kuwa na mchango katika jamii hiyo kwa kufanya kazi. Ili kulifikia hili inapasa jamii ya kisoshalisti kujenga tabia na fikra sahihi kwa wanajamii husika kwamba changamoto yetu ni kubaini mahitaji yetu na kuyawianisha na fursa zilizopo katika jamii husika.

Msingi mwingine wa jamii ya kisoshalisti ni kutokuwepo kwa wanyonyaji na unyonyaji. Mwalimu Nyerere ameeleza bayana katika Kitabu chake cha Uhuru na Ujamaa kwamba haipasi mtu mmoja awe bwanyenye na asifanye kazi wakati wenzie wakifanya kazi katika mashamba na viwandani. Na aina nyingine ya unyonyaji Mwalimu anaeleza ni kukosa uaminifu na ubinafsi.

Sifa nyingine ya jamii ya kisoshalisti ni umiliki wa nyenzo za uzalishaji mali kuwa chini ya udhibiti na umiliki wa umma. Mwalimu Nyerere alifafanua umiliki na udhibiti wa umma kwa nyezo hizi za uzalishaji unaweza kuwa katika namna ya Serikali Kuu, au Serikali za Mitaa au Vyama vya Ushirika au taasisi na vikundi vingine katika jamii husika. Umiliki na udhibiti wa nyezo za uzalishaji mali haimaanishi kuzuia watu kushiriki katika uzalishaji, la hasha, bali kuhakikisha katika maeneo ya kimkakati Mamlaka ya Nchi nayo inakuwa na mkono.

Je ni ipi Misingi ya Itikadi ya Ujamaa au Ujamaa na Kujitegemea, "Ushoshalisti wa Kitanzania" - Tanzanian Socialism?

Baada ya kufafanua kwa sehemu kuhusu dhana na uhalisia wa Itikadi ya Ujamaa na namna kimisingi inashabihiana sana na Itikadi ya Usoshalisti, hapa Tanzania hali ni tofauti kidogo ukilinganisha na nchi nyingine.

Katika nchi yetu ya Tanzania tunayo Itikadi ya Taifa ambayo ni "Ujamaa na Kujitegemea au Ujamaa". Itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea pia ndio pia Itikadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Ujamaa au Ujamaa na Kujitegemea kama Itikadi ya Taifa imefafanuliwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Sura ya Kumi, Sura ya Tafsiri. Katiba ya Nchi inasema kwamba "Ujamaa au Ujamaa na Kujitegemea maana yake ni misingi ya maisha ya jamii ya kujenga Taifa linalozingatia demokrasia, kujitegemea, uhuru, haki, usawa, udugu na umoja wa wananchi wa Jamhuri ya Muungano".

Katika Itikadi ya Taifa iko misingi saba (7) ambayo ujumla wake kitaifa unapasa kutuelekeza kama Taifa la Tanzania, Chama Cha Mapinduzi na Serikali zake. Ujumla wa misingi hii unapasa kuzingatiwa katika kila jambo mojawapo tunalolitenda kama Taifa la Tanzania, kama Chama Cha Mapinduzi, Serikali, Taasisi za Umma, Taasisi Binafsi na watu mmoja mmoja ambao ni waumini wa Itikadi hii na kwa lugha nyingine tutawaita wajamaa.

Mtu yeyote ambaye anaamini au anajinasibu kama Mjamaa lazima wakati wote aiishi misingi ya jumla ya usoshalisti pamoja na misingi ya Ushoshalisti wa Tanzania (Ujamaa).

Katika Awamu ya Pili ya Makala hii nitaelezea kwa ushahidi namna ambavyo Mjamaa Ndugu John Pombe Joseph Magufuli ameishi na kuitekeleza itikadi ya Ujamaa au Ujamaa na Kujitegemea kwa vitendo tangu aingie madarakani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Ujamaa ni Mapambano, na nitaeleza vita iliyoko mbele yetu ambayo ni lazima wajamaa wote tusimame na Ndugu Magufuli ili kufikia Malengo ya pamoja ya kutuletea Maendeleo watanzania.

Mwandishi ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwenye dhamana ya Itikadi na Uenezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kwanini meseji za mawaziri zinadukuliwa? au huo pia ni ujamaa..!

Zile nchi zilizokuwa za kijamaa Russia, China, Cuba na ambao walitufundisha ujamaa siku hizi ni mapepari hata kushinda Uk na Marekani! Kama unabisha tupe sababu! China imekuwa nchi ya kibepari kwa kiwango cha hali ya juu saaaaaana, Russia usiseme, China kuna mabilionea wengi kuliko Marekani!!!!!
 
ndio maana serikali haina uelekeo, kuna watu wanaota ujamaa hii leo?
 
Upuuzi mtupu. Polepole unapoteza muda wako kukesha ukisoma (na kukariri kama mtoto wa form one) matango pori ya miaka ya sabini huko ofisini Lumumba. Mtafute Zitto akupe vitabu vya kusoma vinavyoendana na ulimwengu wa leo.

Vitabu vya Nyerere vya ujamaa ni "OBSOLETE". Ukivisoma angalau uwe na akili ya kutafakari kilichomo ndani na kulinganisha na mazingira ya sasa ya dunia. Kwa nafasi yako ya uenezi ukisoma kwa kukariri kama mtoto wa form one A, ni hasara kwa chama chako na taifa kwa ujumla.

Kwa andiko hili, unapaswa kuondolewa kwenye hiyo nafasi uliyokalia.
 
Fikra za kimasikini hizi, eti wajamaa wanachota hela hazina wanawanunua wapinzani
 
Back
Top Bottom