Sisi marofa na mawazo yetu juu ya corona

Papi Chulo

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
6,260
7,389
Hapa nipo na marofa wenzangu tumeshashiba ugali wa mama ntilie, ghafla stori za corona zikaanza na ubishani mkubwa ukatokea,

Hivi serikali kwa nini isitangaze uvaaji wa barakoa kila mtu pindi anapotoka nyumbani kwake hasa katika haya majiji yaliyoathirika zaidi, mmoja kati ya marofa akasema "haiwezekani" kwani dunia nzima inalalamika kutotosheleza kwa hizo barakoa, mwingine akasema"inawezekana"

Tukamuuliza "inawezekana vipi"

Akaanza kueleza

Serikali ifadhili vile viwanda vinavyozalisha hii mifuko tunayotumia kununulia bidhaa sokoni badala yake izalishe barakoa kwa wingi sana usiku na mchana...hahaaaa aaah ha marofa tukacheka sana, pia akaongeza

Au kama hiyo ni ngumu, basi serikali itumie kiwango fulani cha fedha itangaze tenda kwa mafundi vyerehani zaidi ya 1000 Dar es Salaam nzima, kisha iwatafutie uwanja mkuuuubwa sana kama ule wa taifa, iwaweke hao mafundi vyerehani washone hizo barakoa kwa wingi wastani wa barakoa 200 kwa kila fundi usiku na mchana, kisha serikali iwauzie wananchi kwa gharama nafuu kabisa za ki-uwananchi ili kila mmoja wetu avae barakoa kila anapotoka nje ya hausi yake.. ..

Eti nyie wadau mnaonaje haya mawazo ya marofa hawa, eti inawezekana au haiwezekani
🤣🤣🤣🤣🤣🤣😂😂😂
 
Kwani rofa mwenzao wasemaje?
Yaani rofa mimi ndo sielewi kama inawezekana au haiwezekani!..ila nashangaa tu inakuwaje tunashindwa kutengeneza ventilators,hata hizi barakoa nazo tushindwe?
 
Yaani rofa mimi ndo sielewi kama inawezekana au haiwezekani!..ila nashangaa tu inakuwaje tunashindwa kutengeneza ventilators,hata hizi barakoa nazo tushindwe?
Mkuu ventilator haina ugumu was kutengeneza ila hamasa /hamu ya kutengeneza haipo kulingana na wabasiasa waliopo.Nano atafadhili hip ventilator.Kuna blue print za ventilator rahisi from MIT zimewekwa mtandaoni ili wanasayansi mbalimbali wajiundie wenyewe nchini mwao.Kinachohitzjika no kununua vifaa rahisi vinavyopafikana ktk mazingira na kuunganisha.
Document hii hapa
 

Attachments

  • DMD_2010_Al_Husseini.pdf
    684.4 KB · Views: 1
Mkikusanya hawo mafundi 1000 mkawaweka uwanjani...italeta msongamano mkubwa ambalo bado ni tatizo
 
Hapa mnataka wananchi wageuzwe fursa tu.
Barakoa moja bora yenye dawa sasa ni 2000.
Massa 9 ya kazini mtu atapaswa kuvaa barakoa 2-3 = 4000-6000 per day.
Hapo mkate wa wana mtaupeleka nyie nyumbani kwa mvaa hiyo barakoa?
 
Back
Top Bottom