Sishauri Forker 50 na Forker 28 ziwe 'Branded' kama Ndege za Kibiashara za ATCL

Ni bwege sana huyu Genta, nilidhani ana hoja kubwa na mbadala kumbe eti moja iuzwe. Hopeless kabisa!
Huyu jamaa anajifanya ana akili sana na mjuzi wa mambo, na Mimi mwanzoni nilikuwa namchukulia hivyo lakini hili andiko, let me reserve my comments! Unajua kitendo alichofanya JPM ni cha kipongezwa cha kutoa hizi ndege zizalishe! Niliumia sana siku moja wakati mtoto wa (yule waziri wa ndani alofukuzwa kwa ulevi na Magufuli ) alipofariki ndege ya serikali ilikuwa imepaki mwanza airport ikiksubiri mama salma (enzi za JK) tangu asubuhi hadi jioni. Ni bora ibaki moja na nyingine zizalishe. After all kwa vile ni ndogo ATCL waweza kuwa wanasitumia kwa route ambazo zina abiria wachache. Aidha alinikosha aliposema ndege hizi zinaweza kukodishwa nikafikiria Dreamliner ni bora ikakodishwa kwa mtano Ethiopian airlines au mashirika mengine zizalishe
 
Waliobeza hoja ben saa nane juu ya PhD ya jiwe,kimoyomoyo mnaumia.

Jamaa yeye kila panapo hadhira yete hachagui maneno ya kuongea.na hata anapo umbuliwa bado hajifunzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mh. Rais kwa hili inabidi ashauriwe upya... Nina sbb za msingi mno mnoo..!!

1: Fokker 28, kwa kubebea abiria hailipi kabisaa kabisaa.. Sijui nisemeje mnielewe, yaani was not meant for paxs business.. Ni ndege inayokula mafuta sana, pia vifaa vyake vya matengenezo ni ngumu kuvipata sbb ni ndege mzee sana..!! Sbb hizo ndege F28 zilisha achwa kutengenezwa miaka mingi hivyo spares ni ngumu mno kupata, biashara haitaweza na ni fuel guzzler yaani..!! Yaani ni sawa na VX V8 upaki na dala dala upakie abiria utegemee profit..!! It doesn't work.. Hili tutapenyeza ushauri kwa mh Rais ili ajue ukweli halisi, mh Rais ni mtu mwelewa sana hana shida..!!

2: Fokker 50, hii biashara ya kubeba abiria inaweza na inalipa, ulaji wa mafuta ni mzuri, vifaa vya spares vinapatikana, hili halina tatizo..

Tatizo la kupeleka F50 ATCL ni hili hapa:
Fokker 50 ndio ndege pekee imebaki kama moyo na roho ya serikali kwa domestic flights zote za viongozi wa juu, ikiwemo Mh. Rais mwenyewe, Makamu, Rais wa Znz, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais wa Znz na National events zote za kitaifa za ndani.. G550 mostly ni kwa international flights..!! Sasa ingawa Mh. Rais haruki mara kwa mara, hawa viongozi wengine wote, wasaidizi wake hapo juu, huruka mara nyingi, karibu kila siku, nchi nzima, serikali hutegemea hiyo F-50 kwa asilimia 100% kusafirisha hao viongozi.. Sasa sielewi viongozi hao watasafiri vipi ikiwa F-50 itaenda ATCL..!! Nchi ni kubwa mno kusafiri kwa gari..!! Pia ndege ikiwa inatumia na abiria mara kwa mara itachoka haraka, sijui kama hilo wameliona, na ndege za viongozi zinatakiwa salama mno mnoo, sasa sielewi itakuaje, ugumu mkubwa itakuwa kwa wasaidizi wake Mh. Rais, sbb watapata shida sana kusafiri ikiwa F-50 itaenda ATCL.. Ujue ukishapanga ndege kwenye schedule ya abiria, na inaruka, tayari ushaingiza hasara ikiwa utaitoa kwenye schedule na abiria watakuwa na usumbufu, sbb mfano imeruka asubuhi, mchana F-50 inatakiwa kuruka na kiongozi, na kuna route ya abiria na hakuna ndege nyingine ya kuwachukua hao abiria mchana huo labda, tayari ni mvurugano kweli kweli..!!

Anyway, Mh. Rais ndio muamuzi wa mwisho, pamoja na nia njema sana aliyonayo, ila hili ni ngumu mno, ataja ona katika utekelezaji..!! Siku njema sana niwatakie..!!
 
Nashukuru Mungu kuwa kupitia tu ' Uzi ' wangu huu nimeweza sasa kuwajua wale ' Waliobarikiwa ' kwa ' Upumbavu ' hadi Milele. Nimeweka wazi sana Hoja yangu kuwa sishauri hizo Ndege za Rais ziwe ' branded ' hivyo na zibebe ' Abiria ' kwa Hoja ya Rais kama alivyosema na kama nia ni Kuiongezea Mapato ATCL na Kuimarisha Sekta ya Anga nchini basi hizo Ndege kama ziko Tatu mbili zibebe Abiria ila Ndege moja ibaki vile vile kuwa ni ' Maalum ' tu kwa Kumbeba Mheshimiwa Rais au Makamu wake au Waziri Mkuu wake lakini zote zisifanywe zikawa za Abiria. Na kama haitoshi katika Maelezo yangu nisema vyema tu kuwa kama ikiwezekana basi ni bora hizo Ndege ziuzwe na Hela inayopatikana hapo ielekezwe katika Sekta muhimu ya Kilimo ambayo Kwangu Mimi bado inahihati nguvu kubwa lakini bado ' Mifungulu Ngenge ' fulani isiyojua Kufikiri na inayojua tu Kujipendekeza kama siyo Kujikomba inatetea.

Ngoja niendelee ' Kuwadharau ' hapa.

Cc: Saguda47 , heavyload, narumuk , retweeted , jogoo_dume , idawa , sonaderm , Rogojin The Idiot , Elly official , kakolaki , Lokissa , MWALLA
Hizo ndege zote zinamaana yake, Fokker 50 ni ndege maalumu kutua mahali popote hata kwenye nyasi,hivyo itasaidia hata kuconnect watalii mbugani au viwanja ambavyo Q400 au jet engines hazitatua hivyo kwa maamuzi hayo zitasaidia kuongeza routes na mtandao, hiyo F 28, ni jet engine na very fast itasaidia pia, kwanza ilikuwa na tatizo la engine na ikawa imepaki tu hivyo bora ifanye kazi, Makamu au WM wakihitaji zitakuwepo tu, kwani mbona wamekuwa wakikodi, Beechcraft (safari), PW etc. kwa matumizi ya Rais Gulfsteam inabaki kwanza interior configuration yake haifai kuwa commercial aircraft, labda ikodiwe kwa executives na VIPs, ila kwa usalama ni bora hiyo ibaki mahususi kwa viongozi wetu wakuu.na ni long range.kwa ufupi uamuzi husika ni sahihi, kwanza TGFA sasa watakuwa kipato kikubwa zaidi maana ukiacha ndege za serikali hata hizi zote za ATCL kimsingi ni za TGFA.
 
Aliyekuambia kuwa Mimi nina shida ya Vyeo au labda wakati nampamba na nampigia Kampeni Rais Dkt. Magufuli hapa Jamvini mwaka 2015 nilikuwa natafuta ' Uteuzi / Cheo ' Serikalini nani? Unadhani kila mwana CCM anashida na hizo ' Teuzi ' zenu? Kwani ambao hawajateuliwa huko CCM na Serikalini hawaendeshi maisha yao? Hawana maisha mazuri? Na aliyekuambia kuwa ili Mtanzania ufanikiwe unatakiwa ujiingize katika Siasa ni nani? Eti na Wewe kwa ' Uharo ' huu ni ' Kada ' wa CCM. Kweli CCM ya sasa imevamiwa na inahitaji Damu ya Yesu Kuikomboa.
Tangu Lini ukawa mtanzania, wewe si raia wa Rwanda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe na wenzio, mlioumia na system ya uongozi wa JPM, tunajua mko wengi sana,na kwa ujumla mmebanwa na kushikwa pabaya sana.
Ingawa unaongea kwa kuzidi kujaa sumu, mimi nitaendelea kukueleza ukweli.

Kwanza kauli zako ni ushahidi wazi tukuelewe, ya kwamba wewe unaweza kabisa kuwa wale wafanya matukio, halafu yakatupiwa lawama upande usiohusika.

Lakini pia usijipe" brand" kwamba wewe humu ni think tank.nasema wazi kila member humu ana haki sawa na mwingine yeyote ambaye amekidhi vigezo vya kumridhisha moderator kumuachia kuchangia bila kuvunja masharti na vigezo vya JF. (Ingawa siku zinavyosonga, kejeli na matusi yanazidi kuongezeka kwa baadhi ya wachangiaji).

Nashangaa unajiita mahiri, lakini unalipuka kwa vipande vidogo tu vya ukweli.
Je ungefanikiwa kuukwaa ukubwa wewe na unayemkosoa mna tofauti gani???.

Ungekuwa msomi lazima ungekuwa mstaarabu pia, na usingetoa vitisho vya maisha humu JF.hili ni jukwaa huru

na hupaswi kuligeuza kama jamvi la watu wa mlengo fulani na kujigeuza VIP wa JF ambaye ni untouchable.
Lakini pia ungekuwa smart usingetiririka humu hadi kufikia kutishia member maisha. Hii inaweza kuja kutumika kama• water tight evidence •

Jaribu kuacha mihemuko isiyo ya lazima na ukubali kuambiwa ukweli. Hata kama huupendi.

Nchi hii kabla ya JPM kushika madaraka ya urais, tayari tulikuwa tunaelekea kwenye mgawanyiko mkubwa kitabaka. Na enzi hizo kauli na vitisho kama hivi ulivyovitoa leo humu ndiyo ilikuwa lugha ya mtaani.

Kila aliyewahi kubahatika kuwa aidha na rafiki au ndugu mwenye madaraka,

itokeapo aidha katika hali ya kawaida iwe bar,kijiweni au hata mmepata ajali ya magari yenu kukwaruzana kidogo na hata bila kujali nani mkosefu.
Ilikuwa anapiga simu na dakika mbili kufumba na kufumbua zitatokea zitakako tokea iwe defender au whatever ,na kukusomba bila kutaka kujua nani mkosefu.

Na utasindikizwa na kauli kali kama NITAKUPOTEZA MIMI au NITAKUFICHA! nk.

Sasa hayo matabaka niliyoyatolea mfano hayapo tena. .

Acha JPM atujengee nchi na acha hizi zipakwe rangi. VIVA MAGUFULI.

.
View attachment 992205View attachment 992204

Sent using Jamii Forums mobile app
Naomba usubili hizi zipakwe rangi

Mbona maelezo yako ya sasa hivi umendika ' Kiuhuruma ' sana? Nimeiva kwa mbinu zote baadhi za Kitanzania na nyingi za Kiuganda na Kinyarwanda hivyo kuwa makini mno na Mimi tafadhali. Halafu unasema kuwa Mimi ndiyo nimekutisha wakati Kimsingi Wewe ndiyo uliyeanza Kunitishia au umeyasahau maelezo yako ya awali katika ' post ' yako ile? Nakupa tena ONYO KALI najua unajivunia ' Mafunzo ' yako ila nikuhakikishie tu kuwa bado hujafuzu na kuwa makini sana. Maelezo mengi halafu yote ni ' Garbage In Garbage Out ' na ' Trash In Trash Out ' ( GIGO na TITO ) tupu!
 
Hii ni ' dharau ' kubwa kwa Marais waliopita kuanzia Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Mzee Kikwete kwa Mtu mmoja leo kuamua kwa ' Kukurupuka ' tu kuwa Ndege za Rais Forker 50 na Forker 28 ziwe ' Branded ' kama ' Commercial Planes ' za ATCL.

Hili halipo na halijawahi kutokea nchi yoyote ile duniani na naamini hata tungekuwa Mbinguni Kwake Mwenyezi Mungu hata Yeye pia asingefanya hiki ' Kituko ' ambacho GENTAMYCINE nakiita ni cha Kufungulia mwaka huu ambao bado ni mbichi kabisa wa 2019.

Hoja kwamba zipakwe rangi kisha zichuke Abiria kwakuwa huwa zinakuwa ' grounded ' tu na kwamba hata mwenye Kuhusika nazo huwa hazitumii kwakuwa hasafiri mara kwa mara kutolewa na ' PhD Holder ' kidogo ni kutaka Kuwadhalilisha ' Intellectuals ' wote nchini Tanzania.

Wasaidizi wa Rais hebu fanyeni Kazi zenu vyema Kwake kwa Kumshauri mnaogopa nini? Hivi Sekta ya Anga ya leo au ATCL ya leo inahitaji kweli hadi hata Ndege za Marais nazo ziwe ' branded ' na zijumuishwe kama Ndege za Biashara na Kubeba Abiria? Je kuna hilo hitaji kweli?

Ningeambiwa au ningesikia Hoja kwamba labda Ndege hizo ziuzwe na ibaki moja kisha hizo Hela zitumike Kuimarisha Sekta ya Kilimo ambayo inahitaji msaada na ungalizi mkubwa ningemwelewa Mheshimiwa Rais na ningekubaliana nae kwa 100% ila kwa hii Hoja yake ya leo nampinga na naona ni kama vile ' Tusi ' kwa Watangulizi wake.

Wengine tumeumbwa kuwa wakweli na wawazi hivi hivyo mtusamehe tu na tuvumiliane. Tuache Kukurupuka na kuwa na ' Mihemko ' isiyo na Tija wala Mantiki. Halafu akina Donald Trump ' wakitutukana ' Waafrika huwa tunalalamika na kuona labda anatuonea wakati kumbe huwa yuko sahihi tena kwa 100% zote kutokana na ' Madhaifu ' yetu ya asili.

Nimesikitika!

Nawasilisha.

Umesahau baba la baba alishasema hata akihamia Idodomya anauza majengo yote jijini!
Jengo jeupe najua atanunua mwenyewe kama kipindi ile ya NHC.
Jamaa hataki kuchosha ubongo, kila anachofanya kinaweza kufanywa na mtu yeyote bila kushauriwa.
 
Hapana ushauri wa kiuchumi nikuwa kwa vile tuna ndege za kutosha sasa kwa safari za ndani na pia kwenda nchi za jirani na pia kwavile hizo ndege mbili za serikali hazina matumizi ni bora hizo ndege mbili zikauzwa na pesa itakayopatikana itumike kwenye maendeleo ya nchi! It will be a rational decision.

Na hiki ndicho ambacho ' nimekikazia ' mno Mkuu ila nashangaa kuna Watu ni ' Wapumbavu ' hapa hadi nashangaa hata huko Vyuoni walienda Kusomea nini. Bado narudia Hoja ya Ndege za Rais kuwa ' Branded ' kisha zibebe Abiria naikataa kabisa na naiita ni ya ' Kukurupuka ' ila nikisikia kuwa Ndege hizo ziuzwe ili Hela itakayopatikana itumike Kuimarisha Sekta zingine nchini kama Kilimo, Elimu na Kupunguzia baadhi ya Madeni ambayo Tanzania tunadaiwa na Mataifa makubwa nitakubalina nayo tena kwa 100%.

Cc: commonmwananchi , narumuk
 
Back
Top Bottom