Sishangai vigogo kukimbilia kwa babu loliondo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sishangai vigogo kukimbilia kwa babu loliondo!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kabindi, Apr 30, 2011.

 1. k

  kabindi JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 334
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Niliposikia vigogo wanasiasa kukimbilia loliondo kupata kikombe sikushtuka! Maana naelewa wengi huwa ni wepesi katika imani bila utafiti! mara ngapi tunasikia wakati wa uchaguzi wanakwenda mlingotini Bagamoyo, kulala Makaburini, viungo vya albino na Ushirikina chungu nzima??!! waulizeni waganga wa kienyeji wanajua siri zao!! Wameongoza misafara ya kuwapotosha wananchi badala ya kuimarisha miundombinu ya Hospitali zetu!?. Nilipoambiwa Kwamba Mkuu mwenyewe alikwenda kimyakimya, sikustaajabu maana nilijua huyo ana matatizo mengi! lakini na wewe Magufuli uliye na PhD ya KEMIA? nilidhani ungesubiri utafiti. Haya basi baada ya huo uchunguzi kutoka tunaona Report ya Ajabu kupata kutokea!! tunaona wataalamu wakitumia publications za watu kutoa Conclusion!!! How stupid you are!!! Tafadhali Maguli kama Mkemia Soma hiyo Report halafu tafakari!! Wambie
  watuonyeshe majibu ya Machine kutoka kwenye GC-MS (Gas chromatography–mass spectrometry) ili tuone chemicals Compounds zilizomo katika mmea huo! ni kweli hakuna alkaloids?!!? Maabara gani, imetumika na Sampuri ngapi zilikuwa analysed?! Wana hakika na Classification ya mmea huo?!! Haya! si huyo Babu anasema siku 7-21 Mgonjwa wa ukimwi atakuwa amepona?! hamjiulizi kwa nini wengine wanakufa na hakuna uthibitisho wa haliyepona Ukimwi?! Mtu akisema ameongea na Mungu na wewe si ni mtu wa Imani kwa nini usimuulize Mungu akujibu kama ni kweli?! ina maana Mungu hawezi kuongea na wewe?! Then kama ni Mkristo, Jesus alikuja kwa ajili ya nani?! na kama ni Muislamu, mahusiano yako na Mungu ndiyo hayo?! KWA WANASIASA SITASHANGAA SANA KWA MAANA WAMEJAWA NA IMANI ZA KISHIRIKINA!!!!! na ndiyo maana unaona hatupati maendeleo.! Kumbe na wewe??!! THINK TWICE!!
   
Loading...