Sisali katika makanisa yao, ila naeshimu imani zao, watendewe haki

4 7mbatizaji

JF-Expert Member
Dec 8, 2019
5,974
6,775
WanaJF Mungu mwema siku zote na niwasalim kila mmoja KWa imani yake popote mlipo nje na ndani nchi.

Sitakuwa na maneno mengi,ila kichwa Cha habari chajieleza.

Leo Tanzania tupo na dini nyingi ambazo zimebeba imani za watu mbalimbali, na sio mbaya Kama hakuna hukiukwaji wa SHERIA za nchi maana lengo kila mtu anapigana KWa njia yake kuiona pepo, japo WENDA hata hao wenye dhamana ya kuchunga kondoo katika imani zao wanapigana fitina za kutosha Kama vile CCM na CHADEMA au Simba na Yanga wakati wao ni tofauti Sana na siasa au club za mpira tajwa hapo juu

Nakuja kwa huyu mama ZUMARIDI, Kama walivyo wengine nae ni mtumishi katika imani yake na wafuasi wake,

Siungi mkono hata kidogo linapokuja suala la jinai maana hakuna aliye juu ya SHERIA Kama imedhibitika bila shaka yoyote lakini lazima uchunguzi wa kina ufanyike Ili thibitisha Hili.

Nasema haya kwa sababu nahisi kwa Jambo la huyu mama ,hajaanza kutana na vikwazo leo mpaka kufikia hatua ya kufunga kanisa, na juzi kwa mujipu wa picha za mtandaoni amekamatwa bado kapigwa, hii inaonesha kwamba bado viko visirani vitokavyo nyuma ya jeshi la police.

NITUMIE FURSA HII KUWAOMBENI SERIKALI KUUNDA TUME HURU YA KUCHUNGUZA TUHUMA ZA HUYU MAMA, KAMA KWELI AFUNGWE TU, NAOMBA MFANYE KAMA MLIVYO FANYA MTWARA NA WATU LEO WAPO MBELE YA SHERIA,

NIONAVYO HUYU MAMA ANAWEZA FUNGWA HATA MAISHA KWA HAKI AU BILA HAKI ,

SASA SERIKALI UNDA TUME HURU MTAMSAIDIA NA KUSAIDIA WENGINE WAJAO KWA KUJUA KOSA ,AU KUJUA UONEVU ,

Mwisho tusicheze na imani za watu ,sio afya KWa taifa Ili Hali akuna vunjaji wa taratibu za nchi ,lakini isiwepo watu fitiana na kuingiza nchi kwenye majaribu,

Amani ya BWANA iwe juu yenu
 
Back
Top Bottom