"Sirudishi Hata Senti Moja, Kiyama Sasa ni Oktoba 21 - Camping" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Sirudishi Hata Senti Moja, Kiyama Sasa ni Oktoba 21 - Camping"

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mjunguonline, May 25, 2011.

 1. mjunguonline

  mjunguonline Member

  #1
  May 25, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Harold Camping, amegoma kuzungumzia mustakabali wa michango aliyokusanya ili kuwezesha radio yake anayomiliki, kutangaza habari za mwisho wa dunia ambao ulitakiwa kujiri siku ya Jumamosi iliyopita, japo siku yenyewe ilikuja na kupita.
  Camping mwenye miaka 89 sasa ni milionea anayemiliki stesheni za radio zipatazo 66 , aliibuka mbele ya mlango wa makazi yake akiviambia vyombo vya habari kwamba "Mwisho wa juma lililopita ulikuwa mgumu kupindukia.

  " Kwa mujibu wa wavuti ya www.myfoxdc.com kwamba 'mtume' huyu amegoma moja kwa moja kuzungumzia suala la urejeshaji wa makusanyo ya sadaka alizopata toka kwa waumini wake aliwaingiza mkenge, akidai hakumtuma yeyote kwenda kukwangua fedha kwenye akaunti zao za benki.


  Huko Marekani makanisa yamekuwa yakijineemesha kwa kuweka mitego wa waumini wao ambao wako tayari kulifia kanisa na si Mungu kama wanavyodahani. Makanisa haya yanaendeshwa na watu waliojibatiza jina la ' wainjilisti' au 'watumishi wa mungu'.

  Viongozi hawa ndio wenye usemi wa mwisho kuhusu mustakabali wa kanisa, hakuna anayeruhusiwa kusema chochote kwani kiongozi ndio sauti teule ya mungu.


  Camping ni mmoja wao, anachosema yeye ndicho alichosema Mungu. Unaweza kudhani hata baada ya kutabiri na kupoteza utabiri wake mara mbili, wamba dunia ilikuwa ikikutana na kiyama, jamaa amekuja na nyingine akisema sasa kiyama ni mwezi Oktoba,

  We had all of our dates correct,” Camping insisted, clarifying that he now understands that Christ’s May 21 arrival “a spiritual coming” ushering in the last five months before the final judgment and destruction.
  “It wont be spiritual on October 21 st,” Camping said, adding, “the world is going to be destroyed all together, but it will be very quick.”


  Tafadhali, wateule wa Camping, safari hii akiomba sadaka/akiba zenu, mpatieni zote, hata zile zilizoko mchagoni. LOL! Kuna dada mmoja alikuwa ananambia jana kwamba Tanzania kuna kina-Campings wengi sana, tuendelee
  kuwasikilizia.


  Wale wanaopenda kukaa pembeni na kuendelea kutazama filamu hii, tegesha macho na masikio vizuri

  http://www. washingtonpost.com/ local/harold-camping- reaffirms-octobe...
   
Loading...