Sirro: Sakata la kina Roma kutekwa ni jambo la kawaida, awashangaa wasanii na Makonda kuingilia

Good People

JF-Expert Member
Aug 6, 2016
945
1,819
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro amesema kupotea (kutekwa) kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake ni jambo la kawaida huku akisitiza kuwa hayajaanza kutokea leo kwani ni tukio kama matukio mengine.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro

Kamanda Sirro amesema hayo baada ya kelele za watu kwenye mitandao ya kijamii ndani ya siku tatu, huku wasanii, wanasiasa pamoja na wadau mbalimbali wa muziki kuja juu juu ya suala la kupotea vijana hao katika mazingira ya kutatanisha huku wengine wakihusisha tukio hilo na masuala ya kisiasa yanayoendelea nchini.

“Matukio ya utekaji hayajaanza leo, hili la kina Roma na wenzake ni tukio kama matukio mengine yaliyokuwa ya ujambazi kwa hiyo tupeni muda tupeleleze, tukifika mahali pazuri tutawaita tuwape taarifa lakini nimeona mitandao mingi inazungumza, jana nikaona wasanii wamekutana lakini nikajiuliza hivi yangekuwa haya matukio yanatokea ya uhalifu yanapotokea watu wanakutana ingekuwaje ?,

Jamani kazi hii tumepewa kwa mujibu wa Katiba na ni lazima tutimize wajibu wetu kwa hiyo tupeni muda tutakuwa na majibu mazuri katika hili”. Alisema Kamishna Sirro pindi alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari ofisni kwake Jijini Dar es Salaam

Aidha Kamanda huyo amesema mpaka sasa wameshaunda timu ya uchunguzi na inaendelea vizuri katika upelelezi huku akiwataka wananchi kuwa na subra kwa kuwa upelelezi ndiyo utasema kila kitu.

Kwa upande mwingine amewataka watu waache tabia ya kujifanya wao ndiyo ‘Kamishna Sirro’ na kutaka kuzungumzia habari za upelelezi hivyo amewataka watu kuliamini jeshi la Polisi kwa kuwa hawapendi vitendo hivyo viwepo na viendelee kutokea.

Pia Soma: Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara
 
Makonda amesema hadi Jumapili watakua wamepatikana

Huyu naye anasema siyo jambo la kubwa

Kesho ndo Jumapili ngoja tusubiri
Kweli aliyeturoga amekufa, yani kwa akili yako unasubili ifike kesho!!!! kwa hiyo swala la Roma limebaki ni la mkuu wa mkoa pekee hadi kesho??? Hili swala ni letu sote mana leo kwake kesho kwangu na wewe.
 
Maneno aliyoyatumia ni ya KIDHALIMU SANA, he is so rude hajatumia maneno ya kibinadamu yapaswa atambue hii mbegu ya chuki wanayoipandikiza kwenye jamii sasa inamea na kustawi vizuri tu.
Mavuno yake yatakuwa machungu sana na ni lazima kuvuna hata yeye atavuna tu.
Atambue pia haya maneno na matendo yao iko siku vitapimwa kwenye mizani ya haki.
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro amesema kupotea (kutekwa) kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake ni jambo la kawaida huku akisitiza kuwa hayajaanza kutokea leo kwani ni tukio kama matukio mengine.

sirro%20lai..jpg

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro

Kamanda Sirro amesema hayo baada ya kelele za watu kwenye mitandao ya kijamii ndani ya siku tatu, huku wasanii, wanasiasa pamoja na wadau mbalimbali wa muziki kuja juu juu ya suala la kupotea vijana hao katika mazingira ya kutatanisha huku wengine wakihusisha tukio hilo na masuala ya kisiasa yanayoendelea nchini.

“Matukio ya utekaji hayajaanza leo, hili la kina Roma na wenzake ni tukio kama matukio mengine yaliyokuwa ya ujambazi kwa hiyo tupeni muda tupeleleze, tukifika mahali pazuri tutawaita tuwape taarifa lakini nimeona mitandao mingi inazungumza, jana nikaona wasanii wamekutana lakini nikajiuliza hivi yangekuwa haya matukio yanatokea ya uhalifu yanapotokea watu wanakutana ingekuwaje ?,

Jamani kazi hii tumepewa kwa mujibu wa Katiba na ni lazima tutimize wajibu wetu kwa hiyo tupeni muda tutakuwa na majibu mazuri katika hili”. Alisema Kamishna Sirro pindi alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari ofisni kwake Jijini Dar es Salaam

Aidha Kamanda huyo amesema mpaka sasa wameshaunda timu ya uchunguzi na inaendelea vizuri katika upelelezi huku akiwataka wananchi kuwa na subra kwa kuwa upelelezi ndiyo utasema kila kitu.

Kwa upande mwingine amewataka watu waache tabia ya kujifanya wao ndiyo ‘Kamishna Sirro’ na kutaka kuzungumzia habari za upelelezi hivyo amewataka watu kuliamini jeshi la Polisi kwa kuwa hawapendi vitendo hivyo viwepo na viendelee kutokea.
Basi sawa!
Ni kawaida kutekwa na watu wasiojulikana.
Haijaanza leo na wala haitaisha leo.
Ingekuwa imeanza leo Ben Saanane ingekuwaje?

Aliyeturoga bado anaishi, anaturoga tena na tena.
 
Kweli aliyeturoga amekufa, yani kwa akili yako unasubili ifike kesho!!!! kwa hiyo swala la Roma limebaki ni la mkuu wa mkoa pekee hadi kesho??? Hili swala ni letu sote mana leo kwake kesho kwangu na wewe.
Kama huafuatilii habari basi uliza kwanza kabla ya kumjibu mtu. Aliyesema mpaka kesho Si ni makonda (Bashte) mwenyewe!
 
Back
Top Bottom