Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,265
- 21,443
Niseme ukweli, pamoja na kuteuliwa kuwa IGP, mie sikuheshimu sana kutokana na utendaji na kauli zako za huko nyuma, kitu kilichonifanya nijiulize kama kweli una busara za kukufanya uwe kiongozi wa juu wa jeshi la Polisi. Raisi Magufuli alisema tuwaogope nyie Polisi - ukweli ni kwamba wala sikuogopi.
Labda unaweza kuji-redeem.
Swali ninalojiuliza hadi sasa ni kwamba kuteuliwa kwako kuwa IGP kutatusaidia nini Watanzania katika suala zima la utendaji wenye ufanisi wa jeshi la Polisi. Uhalifu utapungua? Usalama wetu utaongezeka? Au bado tutaona unaongoza jeshi lenye mtazamo wa kuwatumikia walio wachache na lenye kuona kazi yao ni kupiga, kutoza faini, kuwaweka ndani au hata kuua yeyote anaedhaniwa jambazi? Kwa sasa hivi ndivyo Watanzania, watoto kwa wakubwa, wanavyowaona Polisi. Kushangaa kwangu wewe kukubali kuwa IGP ni katika kukubali kuwa Mkuu wa Jeshi lenye huu muonekano. Labda utaurekebisha.
Nina machache ya kukushauri.
Unapaswa kujua kwamba karibu 70% ya Watanzania wanawachukia sana askari wako. Wengi wamefikia hatua ya kufurahia wakisikia askari polisi kauwawa. Watanzania wengi hawawaoni polisi kama wapo kwa ajili yao. Hivyo jambo kubwa kuliko yote unayotakiwa kufanya, ni kwamba huna budi kuligeuza jeshi la Polisi lisiwe tu jeshi la Polisi la serikali ya Tanzania, bali Jeshi la Wananchi la Polisi (JWP).
Ili ufanikiwe katika jambo la msingi la kulifanya jeshi la polisi liwe la wananchi na lenye ufanisi mkubwa si tu Tanzania bali pia Afrika na duniani kwa ujumla (fanya iwe mission statement mpya ya Polisi), ulipaswa, au unapaswa umweleze ukweli Raisi Magufuli kwamba ikiwa kweli ana nia ya kutaka ukomeshe uhalifu na kukuza usalama, basi yeye na watendaji wake na chama chake waliache jeshi la Polisi liwe huru na kamwe lisitumike kisiasa au kitabaka, asilani. Ukifanikiwa kumshawishi juu ya hili na kulifanya jeshi la polisi liwe neutral na kuwatumikia Watanzania wote kwa usawa bila kujali tabaka au itikadi zao za kisiasa, basi utakuwa umeweka msingi (prerequisite) ya kupata ushirikiano wa juu wa wananchi utakaofanya iwe rahisi sana kukomesha uhalifu la kukuza hali ya usalama nchini.
Hakuna jeshi la polisi duniani lisilo na uhusiano mzuri na wananchi litakalofanikiwa kulinda usalama na kukomesha uhalifu. Haijatokea na haitaanza kutokea Tanzania.
Sehemu rahisi sana kuanza kujenga uhusiano mzuri na raia ni kitengo cha usalama wa barabarani. Usikubali kitengo hiki kitumiwe na serikali kama chanzo cha mapato ya fedha kuisaidia serikali katika ukata wake.
Waagize askari wako wa trafiki kuanza kujenga uhusiano mwema na raia. Kwa mfano, si lazima kila gari wanalolismamisha watafute kwa udi na uvumba losa la kutoza faini. Wanaweza kumsimamisha mtu, kuwasalimu vizuri watu walio kwenye gari, na kutoa ushauri tu juu ya makosa madogo madogo na kuwatakia safari njema. Unaweza kukuta ni indiketa moja imekufa - mwambie tu dereva unajua indiketa yako moja haifanyi kazi - ukifika nyumbani jitahidi uibadilishe isije ikakuletea madhara. Utashangaa impact itakayoletwa na approach hili ikiwa wataitekeleza.
Nilishawahi kutozwa faini ya speeding nikiwa 56km/hr badala ya 50km/hr, nikaambiwa kwa kiburi ukiweza tumia hata 30km/hr. Nilichukia sana - nikawachukia trafiki wote!.
Na pia wanapokuta mtu amekwama na gari njiani, angalau wasimame kuuliza kulikoni, na kama wakiweza watoe msaada angalau wa kumsaidia kusukuma gari lake pembeni, au kumuuliza tu kama ameshawasiliana na mtu ili kupata msaada. Kama ni eneo la hatari wasubiri nae apate msaada au hata ikibidi kusimamisha gari nyingine na kuliomba limvute hadi sehemu iliyo sala - hivyo ndivyo jeshi la wananchi la polisi linavyofanya kazi kukuza usalama, sio kumfokea aliyepata tatizo na gari lake kwa kusema "toa gari yako hapa haraka!"
Jambo la msingi ni unalopaswa kukumbuka ni kwamba, si kila kosa linapofanywa na raia linarekebishwa kwa fimbo - na fimbo zikizidi zinazaa kiburi na chuki - iwe barabarani au mitaani.
Ukizingatia haya utafanikiwa na kuheshimiwa sana na Watanzania - labda hata na Raisi Magufuli. La sivyo subiri tu tushangilie zamu yako ya kutumbuliwa ikifika.