Sirro: Lissu atahakikishiwa usalama wake atakaporejea nyumbani

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,982
144,308
Amesemei kurejea kwake kutakasaidia kukamilisha upelelezi na kufahahamu waliohusika na shambuli lake.

Kamanda Sirro amesema kurejea kwa Lissu kutasaidia kukamilisha uchunguzi na kufahamu waliohusika na shambulio lake.

Akizungumza na Nipashe jana, Sirro alisema kama raia wengine wa Tanzania, anahakikishiwa usalama wake kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

“Kwanza tunashukuru kuwa amepona na sasa anarejea… tutaweza kufahamu zaidi waliohusika na shambulio dhidi yake, lakini pili usalama wake ni jambo la muhimu kama raia mwingine yeyote wa nchi hii,” alisema na kuongeza: “Ndio maana hata wewe upo salama, kwa hiyo tutahakikisha anakuwa salama.”

Jumatano, mbunge huyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alitaja tarehe rasmi ya kurejea nchini kuwa ni Septemba 7, mwaka huu.

Lissu ambaye kwa sasa anatembea kwa msaada wa gongo moja, amepanga kurejea siku hiyo tarehe ambayo mwaka 2017, alishambuliwa kwa kupigwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana.

Septemba 7, mwaka juzi, Lissu alishambuliwa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya gari nyumbani kwake Area ‘D’ jijini Dodoma na watu hao wakati akitoka bungeni.

Akizungumza na gazeti hili Jumatano, Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Patrick Ole Sosopi, alisema Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, aliwapa taarifa kuwa Lissu amemwambia kuwa atawasili nchini tarehe hiyo.

“Tuliambiwa na mwenyekiti wetu kuwa Lissu amesema atarejea Tanzania Septemba 7, mwaka huu na atakuwapo kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,” alisema.

Katika ukurasa wa Bavicha Instagram, waliandika: “Lissu atawasili nchini Septemba 7, mwaka huu na mapokezi yake yatatangazwa kitaifa.”

Awali taarifa za kurudi kwa mbunge huyo zilianza kusambaa kupitia video fupi ikumuonyesha Mbowe akiwataarifu wanachama wa chama hicho kuhusu kurejea kwa Lissu.

Baada ya shambulio hilo la risasi, Lissu ambaye ni Mnadhimu Mkuu wa Upinzani Tanzania alipelekwa Hospitali ya Rufani ya Dodoma kwa matibabu ya awali na siku hiyo hiyo usiku alihamishiwa katika hospitali moja mjini Nairobi, Kenya.

Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, alikaa siku 121 hospitali ya Kenya hadi Januari 6, mwaka jana, alipohamishiwa hospitali nyingine nchini Ubelgiji ambako Desemba 31, alimaliza matibabu yake ya awali na kuanza ziara nchi mbalimbali.

Januari 19, mwaka huu, Lissu alihojiwa katika kipindi cha Dira ya Dunia cha Idhaa ya Kiswahili ya BBC na kuonyesha nia ya kugombea urais mwaka 2020 kama wanachama na viongozi wenzake wa Chadema watampa ridhaa hiyo.

Januari 21, Lissu alihojiwa kwenye kipindi cha HardTalk kwenye Televisheni ya BBC na mtangazaji maarufu Stephen Sackur, kipindi ambacho kilizua mjadala mkubwa kutokana na namna alivyojibu maswali.

Februari 20, mwaka huu, Lissu alifanyiwa upasuaji wa 23 wa mwisho kwenye goti la mguu wa kulia katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, Gasthuisberg nchini Ubelgiji, na alisema baada ya hapo atarejea Tanzania.


 
Habari nzuri
Rudi nyumbani kumenoga tu na dereva wake nae arudi.

Si wana kuhojiwa au hawataki tena waliompiga risasi wapatikane?
 
Tunataka kulindwa wote sio mumlinde Lissu peke aKE maana hata sisi ni watanzania tunahitaji ulinzi na kuhakikishiwa usalama wetu.

Mkijipendekeza kumpa ulinzi extra itakua nikutukosea heshima wananchi wa kawaida.

Akitaka uLinzi zaidi ana uwezo wa kuajiri Ma bodyguards binafsi hata 7 watembee nae kila mahali.\

Ila kumpa ulinzi wa jeshi la TAIFA lissu peke ake kama vile yeye ndio Rais wa hii nchi huo ni udhaifu wa Jeshi na kuonyesha fika kuwa sisi wananchi tusio na kitu ni BURE kabisa.
 
Tunasubiri zile "SIKU TATU" ziishe ili kesho yake tupate waliomteka MO
- KumbukiziMTAFUTANO.jpg
 
Siro kumbuka ulisoma seminary, Mungu anakuona ujue! Hujui kweli Lisu alishambuliwa na akina nani?

Hakuna unayemhisi? Kwanini mlkataza watu wasivae T shirt, wasimwombee kwanini mlisema akifa aende kuzikwa immeadiately bila taratibu za mazishi ya kiserikali.

SIRO UTAHUKUMIWA
 
Amesemei kurejea kwake kutakasaidia kukamilisha upelelezi na kufahahamu waliohusika na shambuli lake.

Vigumu sana kuamini hawa watu
Ushauri kwa Lissu ' watasema wanayotaka watu wasikie but they don't mean it'
Private security ni salama yako
Ngoja jiwe aondoke madarakani lakini kwa sasa don't buy their stories
 
Habari nzuri
Rudi nyumbani kumenoga tu na dereva wake nae arudi.

Si wana kuhojiwa au hawataki tena waliompiga risasi wapatikane?
Mwanamke kuwa na roho la hivi ni hatari kwa uzao wako!!huwez dumu ndoani na utaitwa mchawi mtaani...anyways
Karibu sana nyumbani Tundu Lissu,jihadhari na siasa unazofanya,jilinde vizuri na uendelee kuitetea haki yawale wanaokandamizwa...
 
Amesemei kurejea kwake kutakasaidia kukamilisha upelelezi na kufahahamu waliohusika na shambuli lake.

Siyo kusema tu atahakikisha kuwa Tundu Lissu atakaporejea atakuwa salama, bali atuhakikishie kuwa wale watu wasiojulikana waliomshambulia kwa risasi Mheshimiwa Tundu Lissu wanajulikana
 
Ningekuwa na mamlaka, ningelivunja kabisa hili Jeshi au kubadili uongozi wote wa juu wa Jeshi hili.
Hakuna sababu ya kuwa na Jeshi la Polisi nchini, wakati huo huo wamewabatiza majina, baadhi ya watu nchini kuwa ni watu wasiojulikana...........

Jeshi la Polisi wajibu wake no 1 ni kulinda raia na mali zao

Inapotokea nchini kuwa watu wanatekwa, wanauawa na viroba vya maiti vinaokotwa bila kutolewa Maelezo ni kina nani, basi Jeshi la Polisi la aina hiyo halipaswi KUWEPO nchini
 
Back
Top Bottom