HAYA NI MAONI YANGU MIAKA MIWILI ILIYOPITA, LEO 29 JANUARI 2023 NDO YAMETEKELEZWA NA NECTA.
NAOMBA LIKES ZENU KWA WALE AMBAO MULIONA VINGINE.
_____________________________________________________
Nimeangalia matokeo ya kidato cha 4. Kwa ujumla wake wanafunzi wameshindwa hesabu. Je, Baarza limeleza sababu yake? Hapana! Wako bize kutueleza shule fulani imeongoza.
Baraza hili linalojiita NECTA ni shemu ya wizara ya Elimu. Miaka nenda rudi limeheshimika kwa kusimamia ubora wa mitihani na matokeo yake. Kwa maana nyingine, wanakagua kuona kama wizara mama, imetimiza wajibu wake wa kuwaelimisha watoto wetu. Tunachotaka ni elimu na siyo division 1,2,3,4. Hizo divisions ziwepo lakini kweli tunapozungumza na mtu wa division tuone hiyo division.
Hali haiko hivyo. Hao wote unaowaona division 1, baada ya miaka miwili ya form 5 na 6 unawakuta division 3, 4 na wengine sifuri! Inakuwaje? Hii ni kwa sababu NECTA wameweka sana suala la division kama kipimo cha ufahamu. Hata shule bora sasa ni ile yenye division 1 nyingi jambo ambalo naliona ni upuuzi tu!
Mtendaji mkuu wa NECTA tunaamini kisha sikia maoni kama haya, kwamba aache mtindo wa kututangazia shule ya kwanza, ya pili, nk. Kwa sababu haina maana yoyote zaidi ya kutangaza bishara za watu. Biashara hizi zinakuzwa na NECTA kwa kuzifanya divisions ndo elimu.
Imefikia hatua waalimi wanaiba mitihani ili tu wapate division 1 nyingi. Ubunifu umekuwa ni kujibu maswali madarasani ili wanafunzi wapate division 1. Huu ni upuuzi tuachieni hata division 4 ambaye anaonesha ukomavu na uwezo wa sekondari kuliko division 1 asiyeweza hata kuzungumza mbele za watu.