Siri zaidi migodi ya dhahabu zafichuka; Wawekezaji wajifungulia kampuni za udalali

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=1][/h]
Mwandishi Wetu


anglogold.jpg




Majimbo ya kampuni ya Anglo Gold Tanzania




Wawekezaji wajifungulia kampuni za udalali




MIGODI ya dhahabu nchini imekuwa ikikwepa kulipa kodi kwa kutengeneza mikopo ‘bandia’ iliyoombwa kama mtaji wa kuendesha shughuli na ambayo ndiyo inayodaiwa kula mapato ya mauzo kupitia katika ulipaji wake na riba, Raia Mwema imeelezwa.

Mbali na migodi hiyo kujitengenezea mikopo hiyo zipo pia taarifa ya kuwa baadhi ya migodi huuza dhahabu kwa kampuni tanzu zilizoanzishwa kwa nia ya ukwepaji kodi.


Kampuni hizo ndizo huuziwa dhahabu kwa bei nafuu ambayo ni tofauti na ile ya soko la dunia na zenyewe baadaye huuza dhahabu hiyo kwenye soko la dunia ambako bei ni kubwa, hiyo ikisaidia kuipotezea mapato Serikali kwa sababu hesabu za mauzo zinazowasilishwa serikalini ili kukokotoa takwimu na kujua kiasi cha fedha kinachopatikana ni zile za kiwango cha chini kinachohusisha mauzo kati ya migodi iliyowekeza nchini kwa kampuni za za kati.

Kiwango cha bei ya awali ambayo dhahabu imekuwa ikiuzwa kwa kampuni hizo za kati ndicho hesabu zake zimekuwa zikiwakilishwa serikalini. Kwa hiyo, takwimu halisi za mauzo ya dhahabu zimekuwa za ‘kuchakachua.’


Taarifa hizo zimefichuliwa na Kampuni ya Kimataifa ya CRA-International, iliyotafiti kinachoendelea katika migodi ya dhahabu nchini Tanzania, ikijikita zaidi katika migodi ya North Mara, mkoani Mara na Geita, mkoani Mwanza (sasa Geita).


Hali hiyo ya hujuma zinazotajwa kudumu kwa miaka kadhaa inaanza kufichuka katika wakati ambao migodi hiyo sasa imekubali kulipa kodi serikalini, makubaliano yaliyowekwa bayana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Anglo-Gold Ashanti, Mark Cutifani, mbele ya Rais Jakaya Kikwete, walipokutana Perth, Australia, hivi karibuni.


Hata hivyo, katika hali inayothibitisha kuwa migodi ya dhahabu imekuwa hailipi kodi, taarifa ya Ikulu ilieleza kuwa Anglo-Gold Ashanti sasa italipa kodi.


“Sera nzuri za Serikali za kuyataka makampuni ya madini nchini kuanza kulipa kodi ya mapato zimeanza kuzaa matunda baada ya Kampuni ya Anglo-Gold Ashanti kutangaza kuwa italipa kodi ya sh bilioni 86 (sawa na dola za Marekani milioni 50) mwaka huu.


Taraifa ya Ikulu inathibitisha kwa kueleza kuwa ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kulipa kodi ya mapato tangu mwaka 1999.


“Hii ni mara ya kwanza kwa kampuni ya Anglo-Gold Ashanti kulipa kodi ya mapato kutokana na mapato yake tokea kuingia katika soko la Tanzania mwaka 1999,” inaeleza taarifa ya Ikulu.


Hata hivyo, katika kile kinachoweza kuthibitishwa kuwa ni makosa ya awali ya Serikali kuwapa uhuru mpana wachimbaji wakubwa wa dhahabu nchini kujiamulia kulipa kodi wanapomaliza kurejesha fedha za mtaji wao, taarifa hiyo ya Ikulu imeeleza, “hatua hiyo inatokana na sera ya Serikali ya kuyataka makampuni ya madini nchini kuanza kulipa kodi ya mapato baada ya kurudisha fedha zake za uwekezaji katika uchimbaji wa madini nchini”.


Taarifa ya CRA-International iliyotafiti migodi ya Geita na North Mara inaeleza kuwa migodi hiyo imekuwa na sifa inayofanana ambayo ni kuuza dhahabu kwa kampuni zenye uhusiano nayo kwa lengo la kula njama ili kutoa takwimu zinazoweza kuikosesha mapato halisi Serikali.


Kwa upande mwingine Kampuni hiyo imeweka bayana kuwa migodi hiyo yote miwili haijawahi kulipa kodi tangu kuanzishwa kwake nchini, hali ambayo inathibitishwa na taarifa ya Ikulu kwamba kama ilivyo kwa kampuni mama ya Anglo Gold Ashanti, nayo haijawahi kulipa kodi tangu mwaka 1999.










 
Unadhani wako peke yao watakuwa wanakula sahani moja na Mh Jakaya Kikwete ,Mh Mkapa,na Magamba wenzao, Kunguni wanyonyaji wakubwa haiwezekani kwa miaka kumi yote wasijue hao madalali
 
Hapa ndipo tunapojiuliza weledi wa wazee wa intelijensia! mbona mambo kama haya hawayaoni maana toka 1999 - 2011= 12 years ambayo hawa jamaa hawakugundua wizi huu mkubwa! Ikidhibitika wanasheria wetu wawashtaki hawa jamaa walipe fidia na kulipa kodi yote waliyokwepa.
 
Hapa ndipo tunapojiuliza weledi wa wazee wa intelijensia! mbona mambo kama haya hawayaoni maana toka 1999 - 2011= 12 years ambayo hawa jamaa hawakugundua wizi huu mkubwa! Ikidhibitika wanasheria wetu wawashtaki hawa jamaa walipe fidia na kulipa kodi yote waliyokwepa.
Kinachosikitisha ni kwamba dhahabu ni depletable goods. Wameshachimba miaka 12 kwa bure kabsia. Huenda hiyo dhahabu ikamalizika katika miaka 12 mingine ijayo. Ile mikataba ambayo wanadai kuwa ni siri kati ya serikali na wawekezaji bunge lazima liishupalie iwekwe wazi tujue mchawi wetu ni nani.
 
Vice President wa hiyo North Mara ni Mtanzania tena Kijana.

Haya maujanja hayafanywi na wazungu, "miafrika ndivyo tulivyo"
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom