Siri za wizi alizofichwa Mkaguzi Mkuu nje nje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri za wizi alizofichwa Mkaguzi Mkuu nje nje

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlalahoi, Apr 22, 2011.

 1. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2011
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Siri za wizi alizofichwa Mkaguzi Mkuu nje nje

  Mwandishi Wetu
  Aprili 20, 2011

  - Mabilioni yaligawanywa kama njugu kufidia hasara hewa
  - Ni kampuni 27 za vigogo, imo Al-Adawi iliyovuna mil 400/-

  WAKATI Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akiripoti kunyimwa orodha ya kampuni za ununuzi pamba zilizolipwa mabilioni wakati wa mtikisiko wa uchumi duniani, Raia Mwema, inayo orodha hiyo ya kampuni zaidi ya 26, ikiwamo kampuni inayoitwa Al-Adawi Limited.

  Al Adawi ni jina linalofanana na jina la mtu aliyejitambulisha kuwa ni mmiliki wa kampuni ya Dowans, akiitwa Brigedia Jenerali (mstaafu) Sulaiman Al-Adawi. Kampuni hiyo ilipendekezwa kuchotewa Sh milioni 405.6.

  Mbali na Al-Adawi, katika mchanganuo wa hesabu za kampuni husika, uliopendekezwa na baadhi ya benki nchini ambazo ni CRDB, Stanbic, Exim na Kenya Commercial, moja ya kampuni imebainika kulipwa hadi bilioni 1.4, wakati hasara iliyopata ni sh milioni 742, kampuni nyingine imefidiwa hasara ya Sh milioni 500, wakati ikibainika haikupata hasara yoyote.

  Katika toleo namba 129 (Aprili 14 hadi Aprili 20) mwaka jana, gazeti hili liliripoti orodha ya kampuni hizo, ambazo kabla ya kulipwa mabilioni hayo, michanganuo ya hesabu zake ili kubaini hasara walizopata kutokana na mtikisiko wa uchumi, ililazimika kurejewa baada ya michanganuo ya awali kugubikwa na taarifa za uongo.

  Lakini wakati Raia Mwema likiwa limepata orodha ya kampuni hizo kutokana njia zake za uchunguzi, CAG anaeleza kunyimwa orodha hiyo na kubainisha hayo katika ripoti yake kuhusu ukaguzi wa taarifa za fedha za Serikali Kuu kwa mwaka ulioishia Juni 30, 2010.

  Ingawa Bunge liliidhinisha Serikali kutumbukiza Sh trilioni 1.7 kwa ajili ya kudhibiti mtikisiko wa uchumi uliotajwa kuathiri zaidi kampuni za ununuzi wa pamba, CAG anaeleza kuwa kilichotolewa na Serikali ni Sh bilioni 48 na amenyimwa orodha ya kampuni zilizopewa mabilioni hayo.

  "Serikali kupitia Hazina ililipa kiasi cha Sh 48,000,270,000 katika Benki ya Tanzania kama mchango wake katika kuchochea ukuaji wa uchumi kutokana na mtikisiko wa uchumi ulioikumba dunia.

  "Hata hivyo, Hazina haikutoa orodha ya makampuni au watu binafsi walionufaika na fidia hiyo au malipo ya madeni yao kuahirishwa.

  "Utaratibu wa kurekodi malipo na marejesho ya fedha hizi haukuwekwa bayana na hivyo kushindwa kujiridhisha endapo yalikuwa ni malipo halali ya fedha za umma," anaeleza CAG, Ludovick Utouh.

  Hotuba ya Rais Kikwete

  Kutokana na mtikisiko wa uchumi duniani, ulioanzia Marekani, Rais Jakaya Kikwete alitangaza mpango wa serikali kudhibiti mtikisiko huo nchini.

  Mara baada ya hotuba yake, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, aliliomba Bunge kuidhinisha Sh trilioni 1.7 kwa ajili ya kudhibiti mtikisiko hasa kwa wanunuzi wa pamba, ili kutoathiri wakulima.

  Kwa wakati huo, wanunuzi wa pamba walitajwa kuathirika kutokana na bei ya zao hilo kwenye soko la dunia kuporomoka na wao kupata hasara kiasi cha kukosa fedha za kununua tena pamba kwa wakulima.

  Bunge lilipitisha maombi hayo ya Waziri Mkulo, ingawa pia baadhi ya wabunge walitaka fungu hilo maalumu lililioitwa ‘stimulus package' liundiwe sheria maalumu ya Bunge ili kudhibiti matumizi yake na kuepusha nchi kutumbukia katika kile kilichotajwa kama EPA namba mbili.

  Hata hivyo, haikuridhiwa kuundwa kwa sheria mahsusi, na badala yake Serikali iliahidi bungeni kuwa CAG atakagua hesabu za mgawo huo.

  Benki zilizohusika na mgawo

  Serikali kupitia Hazina ilitoa fedha hizo kwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), ambayo iliweka fedha hizo katika baadhi ya benki ambazo zilipewa jukumu la kuwafidia wanunuzi husika wa pamba, baada ya kufanyika michanganuo ya hesabu na hasara walizopata.

  Benki zilizohusika ni CRDB, Tanzania Investment Bank (TIB), Exim Bank, Stanbic Bank na Kenya Commercial Bank.

  Kampuni na michanganuo tata

  Benki ya CRDB ilifanya michanganuo ya kampuni 26 na Benki ya TIB ikipitia mchanganuo wa kampuni ya Al-Adawi pekee na kupendekeza ilipwe Sh milioni 405.6.

  Benki ya Kenya Commercial, nayo pia ilipitia michanganuo ya kampuni kadhaa na kutaka zilipwe. Kampuni hizo ni Birchand Oil Mills Ltd, ambayo Kenya Commercial ilitaka kampuni hiyo ilipwe Sh bilioni 1.66.

  Hata hivyo, baada ya michanganuo hiyo kurejewa na watalaamu nje ya benki hiyo ilibainika kuwa kampuni hiyo ilistahili kulipwa Sh bilioni 4.642, kukiwa na ongezeko zaidi kulinganisha na mapendekezo ya awali.

  Benki ya Exim ilipendekeza kampuni ya Bio Sustain kufidiwa Sh milioni 597.7 hata hivyo, baada ya kufanyika upya kwa uhakiki kampuni hiyo ikapendekezwa ilipwe Sh milioni 458.1 pungufu zaidi ikilinganishwa na awali.

  Kwa upande wa benki ya Stanbic, ilipendekeza kampuni ya S & Ginning Co. Ltd kufidiwa Sh bilioni 5.69, na ulipofanyika uhakiki wa pili, ikabainika kuwa kampuni hiyo ilistahili kufidiwa Sh bilioni 2.86.

  Benki ya CRDB ilipendekeza kampuni ya Badugu Ginning ya Musoma, ilipwe fidia ya Sh bilioni 1.4, wakati hasara iliyopata ni ya Sh milioni 742.2. Hata hivyo, ulipofanyika ukaguzi upya kampuni hiyo ilifidiwa Sh milioni 742.2 hasara halisi iliyopata.

  Kampuni nyingine ni Chesano Cotton Ginning Ltd ya Bariadi, mkoani Shinyanga, katika mchanganuo wake kwa CRDB ilijieleza kuwa gharama za uendeshaji na ununuzi wake wa pamba ni Sh bilioni 2.6 na mapato yake ni Sh bilioni 1.99 (takriban bilioni 2).

  Kwa mujibu wa mchanganuo wa kampuni hiyo, mauzo iliyopata kutokana na kuuza mbegu za pamba ni Sh milioni 586 na mapato yake ya jumla ni bilioni 2.6.

  Utata unaoibuka hapo ni kwamba mchanganuo unabainisha ilipata faida ya Sh milioni 6.4 lakini CRDB ilipendekeza kampuni hiyo ifidiwe Sh milioni 580. Ukaguzi zaidi ulipofanyika kampuni hiyo ilipendekezwa ilipwe fidia yoyote kutokana na kutopata hasara.

  Uchunguzi pia umebaini kuwa katika orodha ya kampuni hizo, kampuni ya Gaki Investment Ltd ya Shinyanga, mchanganuo wake wa hesabu unaonyesha kuwa ilinunua kilo milioni 19.8 za pamba, ikitumia Sh bilioni 12.9, mapato yake baada ya biashara ya nyuzi za pamba ni Sh bilioni 12.15, mapato yaliyotokana na kuuza mbegu za pamba ni Sh bilioni 1.727.

  Kwa kuzingatia mchanganuo huo, mapato yake ya jumla kwa msimu husika ni Sh bilioni 13.9, ikiwa imepata faida ya Sh bilioni 1. Hata hivyo, licha ya kampuni hiyo kupata faida ya Sh bilioni moja wakati huo wa mtikisiko wa uchumi, benki ya CRDB ilionyesha imepata hasara ya Sh milioni 146 na ikipendekeza ifidiwe kiasi hicho cha fedha lakini ukaguzi ulipofanyika tena, kampuni ilitakiwa isilipwe.

  Kampuni nyingine ni Igunga Cotton Ltd, ambayo kwenye nyaraka inatajwa kuwa na makao yake makuu Dar es Salaam, mchanganuo wa hesabu zake CRDB ulibainisha kuwa mapato yake ni Sh bilioni 1.7 na kwamba imepata hasara ya Sh milioni 205, lakini ikipendekezwa ifidiwe Sh milioni 839 na uhakiki uliporejewa ikatakiwa ilipwe fidia ya awali Sh milioni 205.

  Orodha ya kampuni hizo iliyofichwa dhidi ya CAG inataja kampuni nyingine kuwa ni Ipililo AMCOs Ltd, ambayo mchanganuo uliokuwapo CRDB ulibainisha kuwa mapato yake ya jumla ni Sh milioni 65.35 ikiwa imepata hasara ya Sh milioni 16.7, hata hivyo, katika hali ya utata zaidi, CRDB ilipendekeza kampuni hiyo ilipwe fidia ya hasara Sh bilioni 51, marejeo ya uhakiki yalipofanyika ikaamriwa ilipwe Sh milioni 16.7 tu.

  Kampuni ya Jambo Oil & Ginneries Ltd ya Shinyanga, ambayo nyaraka zinaonyesha kuwa katika msimu husika (wa mtikisiko) mapato yake ya jumla yalikuwa Sh bilioni 14.9, ikipata faida ya Sh milioni 927.1, katika hali ya kushangaza, ilipendekezwa ilipwe fidia ya Sh bilioni 1.06.

  Kahama Oil Mill Ltd ya Kahama, Shinyanga, mapato yake ya jumla ni Sh bilioni 17 kwa wakati huo wa mtikisiko wa uchumi, mchaganuo ukibainisha ilipata hasara ya Sh bilioni 2.3, lakini cha kushangaza ililipwa fidia ya hasara ya Sh bilioni 4.4.

  Kampuni ya Kisumwa Machinery Ltd, ambayo haikuwasilisha nyaraka za mchanganuo benki katika nyaraka za kampuni zilizolipwa inaonekana kufidiwa Sh milioni 377, kama kampuni ya Canvas Mills (1998) Ltd ya Morogoro ambayo nayo haikuwasilisha mchanganuo lakini imetajwa kwamba imelipwa fidia ya Sh bilioni 1.612.

  CHANZO: Raia Mwema
   
 2. A

  August JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  huu ni wizi, mbona watu wengi tu tannzania wanapata hasara awe mfanyakazi au mkulima lakini hawasaidiwi
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mataifa kama marekani stimulus package ilitumika kwa ajili ya unemployment, lakini darisalama wanagawana vizito kwa visingizio vya kunusuru makampuni binafsi kumbe janja ni asilimia kadhaa zilienda kwa wakaongozi wa sirikali na makampuni kuambulia kidogo.
  Matokeo yake ni kuwanunulia magari ya kifahari wabunge ili kuwaziba midomo, ndio maana wapinzani tu ndio wenye uchungu na mali ya umma.

  Riziwani Kikwete amepata wapi utajiri huu alio nao mara tu baada ya kutoka chuoni kama si pesa hizo ndizo zilizoingizwa kwake na babake kwa kivuli cha kulindwa na cheo cha Urais?
   
 4. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hizo pesa ilikuwa changa la macho tu, Chama cha Magamba kililenga kuzitumia kwenye kampeni. Ufisadi mwingine wa kutisha huo. Hapo sijui ni nani atajivua gamba tena?
   
 5. Elinasi

  Elinasi Member

  #5
  Apr 22, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 64
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Iko siku zitarudishwa.i guess not far from now..
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Apr 22, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kama hukumu ya fisadi katika nchi ni kuvuliwa gamba na kuachwa uendelee na mali zako ulizopata kifisadi basi bora nami niwe fisadi tu!! Alaaaa mbona tunapigwa mbele, nyuma, kushoto na kulia!!
   
 7. V

  Vumbi Senior Member

  #7
  Apr 22, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 191
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  CCM walitumia hizi fedha kufanyia kampenzi zao, hizo kampuni ni mali ya vigogo wa CCm na serikali. Nimeamini ufisadi ccm upo kwenye damu na dawa ya nyoka ni ku-muua na siyo kujivua gamba. 2015 ccm lazima watoke madaraka hata kama ni mapambano kama Libya.
   
 8. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Orodha ya kampuni hizo iliyofichwa dhidi ya CAG inataja kampuni nyingine kuwa ni Ipililo AMCOs Ltd, ambayo mchanganuo uliokuwapo CRDB ulibainisha kuwa mapato yake ya jumla ni Sh milioni 65.35 ikiwa imepata hasara ya Sh milioni 16.7, hata hivyo, katika hali ya utata zaidi, CRDB ilipendekeza kampuni hiyo ilipwe fidia ya hasara Sh bilioni 51, marejeo ya uhakiki yalipofanyika ikaamriwa ilipwe Sh milioni 16.7 tu.

  Nimechukua tu sehemu ndogo ya ufisadi unaofanywa na CRDB.Hii bank sielewi kwanini imekuwa mstari wa mbele kuidhinisha malipo mbali mbali yenye utata mkubwa.Angalia kuanzia jinsi walivyohusika na malipo ya EPA, walivyohusika na Richmond n.k.Kwa kweli hii bank inabidi iangaliwe upya kwani imehusika kwa kiwango kikubwa sana kuitia hasara serikali yetu.
   
 9. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2011
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hizi hela zilitumika kwenye kampeni za CCM wakati wa uchaguzi mkuu?
   
 10. Wed

  Wed JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 298
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60

  Nani haju kwamba hii ilikuwa janja ya CCM kupata fetha za kugarimia uchaguzi mkuu ?? Hii ni EPA nyingine kwa mafisadi nchini !:A S 465:
   
 11. Quinty

  Quinty JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 463
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mwandishi Wetu
  Aprili 20, 2011
  Mabilioni yaligawanywa kama njugu kufidia hasara hewa
  Ni kampuni 27 za vigogo, imo Al-Adawi iliyovuna mil 400/-
  WAKATI Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akiripoti kunyimwa orodha ya kampuni za ununuzi pamba zilizolipwa mabilioni wakati wa mtikisiko wa uchumi duniani, Raia Mwema, inayo orodha hiyo ya kampuni zaidi ya 26, ikiwamo kampuni inayoitwa Al-Adawi Limited.

  Al Adawi ni jina linalofanana na jina la mtu aliyejitambulisha kuwa ni mmiliki wa kampuni ya Dowans, akiitwa Brigedia Jenerali (mstaafu) Sulaiman Al-Adawi. Kampuni hiyo ilipendekezwa kuchotewa Sh milioni 405.6.

  Mbali na Al-Adawi, katika mchanganuo wa hesabu za kampuni husika, uliopendekezwa na baadhi ya benki nchini ambazo ni CRDB, Stanbic, Exim na Kenya Commercial, moja ya kampuni imebainika kulipwa hadi bilioni 1.4, wakati hasara iliyopata ni sh milioni 742, kampuni nyingine imefidiwa hasara ya Sh milioni 500, wakati ikibainika haikupata hasara yoyote.

  Katika toleo namba 129 (Aprili 14 hadi Aprili 20) mwaka jana, gazeti hili liliripoti orodha ya kampuni hizo, ambazo kabla ya kulipwa mabilioni hayo, michanganuo ya hesabu zake ili kubaini hasara walizopata kutokana na mtikisiko wa uchumi, ililazimika kurejewa baada ya michanganuo ya awali kugubikwa na taarifa za uongo.

  Lakini wakati Raia Mwema likiwa limepata orodha ya kampuni hizo kutokana njia zake za uchunguzi, CAG anaeleza kunyimwa orodha hiyo na kubainisha hayo katika ripoti yake kuhusu ukaguzi wa taarifa za fedha za Serikali Kuu kwa mwaka ulioishia Juni 30, 2010.

  Ingawa Bunge liliidhinisha Serikali kutumbukiza Sh trilioni 1.7 kwa ajili ya kudhibiti mtikisiko wa uchumi uliotajwa kuathiri zaidi kampuni za ununuzi wa pamba, CAG anaeleza kuwa kilichotolewa na Serikali ni Sh bilioni 48 na amenyimwa orodha ya kampuni zilizopewa mabilioni hayo.

  “Serikali kupitia Hazina ililipa kiasi cha Sh 48,000,270,000 katika Benki ya Tanzania kama mchango wake katika kuchochea ukuaji wa uchumi kutokana na mtikisiko wa uchumi ulioikumba dunia.

  “Hata hivyo, Hazina haikutoa orodha ya makampuni au watu binafsi walionufaika na fidia hiyo au malipo ya madeni yao kuahirishwa.

  “Utaratibu wa kurekodi malipo na marejesho ya fedha hizi haukuwekwa bayana na hivyo kushindwa kujiridhisha endapo yalikuwa ni malipo halali ya fedha za umma,” anaeleza CAG, Ludovick Utouh.

  Hotuba ya Rais Kikwete

  Kutokana na mtikisiko wa uchumi duniani, ulioanzia Marekani, Rais Jakaya Kikwete alitangaza mpango wa serikali kudhibiti mtikisiko huo nchini.

  Mara baada ya hotuba yake, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, aliliomba Bunge kuidhinisha Sh trilioni 1.7 kwa ajili ya kudhibiti mtikisiko hasa kwa wanunuzi wa pamba, ili kutoathiri wakulima.

  Kwa wakati huo, wanunuzi wa pamba walitajwa kuathirika kutokana na bei ya zao hilo kwenye soko la dunia kuporomoka na wao kupata hasara kiasi cha kukosa fedha za kununua tena pamba kwa wakulima.

  Bunge lilipitisha maombi hayo ya Waziri Mkulo, ingawa pia baadhi ya wabunge walitaka fungu hilo maalumu lililioitwa ‘stimulus package’ liundiwe sheria maalumu ya Bunge ili kudhibiti matumizi yake na kuepusha nchi kutumbukia katika kile kilichotajwa kama EPA namba mbili.

  Hata hivyo, haikuridhiwa kuundwa kwa sheria mahsusi, na badala yake Serikali iliahidi bungeni kuwa CAG atakagua hesabu za mgawo huo.

  Benki zilizohusika na mgawo

  Serikali kupitia Hazina ilitoa fedha hizo kwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), ambayo iliweka fedha hizo katika baadhi ya benki ambazo zilipewa jukumu la kuwafidia wanunuzi husika wa pamba, baada ya kufanyika michanganuo ya hesabu na hasara walizopata.

  Benki zilizohusika ni CRDB, Tanzania Investment Bank (TIB), Exim Bank, Stanbic Bank na Kenya Commercial Bank.

  Kampuni na michanganuo tata

  Benki ya CRDB ilifanya michanganuo ya kampuni 26 na Benki ya TIB ikipitia mchanganuo wa kampuni ya Al-Adawi pekee na kupendekeza ilipwe Sh milioni 405.6.

  Benki ya Kenya Commercial, nayo pia ilipitia michanganuo ya kampuni kadhaa na kutaka zilipwe. Kampuni hizo ni Birchand Oil Mills Ltd, ambayo Kenya Commercial ilitaka kampuni hiyo ilipwe Sh bilioni 1.66.

  Hata hivyo, baada ya michanganuo hiyo kurejewa na watalaamu nje ya benki hiyo ilibainika kuwa kampuni hiyo ilistahili kulipwa Sh bilioni 4.642, kukiwa na ongezeko zaidi kulinganisha na mapendekezo ya awali.

  Benki ya Exim ilipendekeza kampuni ya Bio Sustain kufidiwa Sh milioni 597.7 hata hivyo, baada ya kufanyika upya kwa uhakiki kampuni hiyo ikapendekezwa ilipwe Sh milioni 458.1 pungufu zaidi ikilinganishwa na awali.

  Kwa upande wa benki ya Stanbic, ilipendekeza kampuni ya S & Ginning Co. Ltd kufidiwa Sh bilioni 5.69, na ulipofanyika uhakiki wa pili, ikabainika kuwa kampuni hiyo ilistahili kufidiwa Sh bilioni 2.86.

  Benki ya CRDB ilipendekeza kampuni ya Badugu Ginning ya Musoma, ilipwe fidia ya Sh bilioni 1.4, wakati hasara iliyopata ni ya Sh milioni 742.2. Hata hivyo, ulipofanyika ukaguzi upya kampuni hiyo ilifidiwa Sh milioni 742.2 hasara halisi iliyopata.

  Kampuni nyingine ni Chesano Cotton Ginning Ltd ya Bariadi, mkoani Shinyanga, katika mchanganuo wake kwa CRDB ilijieleza kuwa gharama za uendeshaji na ununuzi wake wa pamba ni Sh bilioni 2.6 na mapato yake ni Sh bilioni 1.99 (takriban bilioni 2).

  Kwa mujibu wa mchanganuo wa kampuni hiyo, mauzo iliyopata kutokana na kuuza mbegu za pamba ni Sh milioni 586 na mapato yake ya jumla ni bilioni 2.6.

  Utata unaoibuka hapo ni kwamba mchanganuo unabainisha ilipata faida ya Sh milioni 6.4 lakini CRDB ilipendekeza kampuni hiyo ifidiwe Sh milioni 580. Ukaguzi zaidi ulipofanyika kampuni hiyo ilipendekezwa ilipwe fidia yoyote kutokana na kutopata hasara.

  Uchunguzi pia umebaini kuwa katika orodha ya kampuni hizo, kampuni ya Gaki Investment Ltd ya Shinyanga, mchanganuo wake wa hesabu unaonyesha kuwa ilinunua kilo milioni 19.8 za pamba, ikitumia Sh bilioni 12.9, mapato yake baada ya biashara ya nyuzi za pamba ni Sh bilioni 12.15, mapato yaliyotokana na kuuza mbegu za pamba ni Sh bilioni 1.727.

  Kwa kuzingatia mchanganuo huo, mapato yake ya jumla kwa msimu husika ni Sh bilioni 13.9, ikiwa imepata faida ya Sh bilioni 1. Hata hivyo, licha ya kampuni hiyo kupata faida ya Sh bilioni moja wakati huo wa mtikisiko wa uchumi, benki ya CRDB ilionyesha imepata hasara ya Sh milioni 146 na ikipendekeza ifidiwe kiasi hicho cha fedha lakini ukaguzi ulipofanyika tena, kampuni ilitakiwa isilipwe.

  Kampuni nyingine ni Igunga Cotton Ltd, ambayo kwenye nyaraka inatajwa kuwa na makao yake makuu Dar es Salaam, mchanganuo wa hesabu zake CRDB ulibainisha kuwa mapato yake ni Sh bilioni 1.7 na kwamba imepata hasara ya Sh milioni 205, lakini ikipendekezwa ifidiwe Sh milioni 839 na uhakiki uliporejewa ikatakiwa ilipwe fidia ya awali Sh milioni 205.

  Orodha ya kampuni hizo iliyofichwa dhidi ya CAG inataja kampuni nyingine kuwa ni Ipililo AMCOs Ltd, ambayo mchanganuo uliokuwapo CRDB ulibainisha kuwa mapato yake ya jumla ni Sh milioni 65.35 ikiwa imepata hasara ya Sh milioni 16.7, hata hivyo, katika hali ya utata zaidi, CRDB ilipendekeza kampuni hiyo ilipwe fidia ya hasara Sh bilioni 51, marejeo ya uhakiki yalipofanyika ikaamriwa ilipwe Sh milioni 16.7 tu.

  Kampuni ya Jambo Oil & Ginneries Ltd ya Shinyanga, ambayo nyaraka zinaonyesha kuwa katika msimu husika (wa mtikisiko) mapato yake ya jumla yalikuwa Sh bilioni 14.9, ikipata faida ya Sh milioni 927.1, katika hali ya kushangaza, ilipendekezwa ilipwe fidia ya Sh bilioni 1.06.

  Kahama Oil Mill Ltd ya Kahama, Shinyanga, mapato yake ya jumla ni Sh bilioni 17 kwa wakati huo wa mtikisiko wa uchumi, mchaganuo ukibainisha ilipata hasara ya Sh bilioni 2.3, lakini cha kushangaza ililipwa fidia ya hasara ya Sh bilioni 4.4.

  Kampuni ya Kisumwa Machinery Ltd, ambayo haikuwasilisha nyaraka za mchanganuo benki katika nyaraka za kampuni zilizolipwa inaonekana kufidiwa Sh milioni 377, kama kampuni ya Canvas Mills (1998) Ltd ya Morogoro ambayo nayo haikuwasilisha mchanganuo lakini imetajwa kwamba imelipwa fidia ya Sh bilioni 1.612.
   
 12. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nchi hii ni kama shamba la bibi au mwembe ulio upenuni mwa kibanda cha bibi. Watu wanafika na kutikisa na maembe yanadondoka. Wanakula maembe kirahisi bila 'chenga'. Kinachosikitisha ni kwamba nchi yetu inaliwa ikiwa katikati ya matatizo tena makubwa.

  Ebu rejea suala la Richmond. Tulikuwa na crisis ya umeme nchi nzima, wakaja wazee wenye matumbo makubwa wakacheza na raketi zao, nchi ikatafunwa na kuliwa zaidi. Mabilioni ya shilingi yalikwapuliwa mara moja na mengine yaliendelea kukwapuliwa kila mwezi. Likaja suala la mdororo wa uchumi ulioikumba takriban Dunia nzima, wenye matumbo wakapata kisingizo, wakaja na mwamvuli wa 'stimulus package'. Mabilioni ya shilingi yakamwagwa na hatima yake ndiyo hii, kumbe fedha zililiwa na wenye matumbo makubwa huku watanzania wa kawaida wakiendelea kuwa mafukara zaidi. Ndiyo maana wengi wetu tunaichukulia Tanzania kama shamba la bibi. Hata mpita njia anaweza kuchepuka akapata maembe kadhaa bila bugudha!
   
 13. Quinty

  Quinty JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 463
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Duh mkuu hata shamba la bibi lina afadhali muda mwingine nikifikiria hii nchi yetu na uongozi nasikitika sana maana ufisadi uko nje nje na bado hawachukuliwi hatua yeyote....!
   
 14. k

  kakini Senior Member

  #14
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  unajua watu wengi bado wamelala na wengine bado wana ild inaitwa nidhamu ya woga,

  Raisi wa burundi aliwahi kusema watanzania hawana amani bali hawajui mambo yanayoendelea, kama wangejua tu mambo yanayoendelea pasingekalika, jamani tuamkeni
   
 15. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,402
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  1. Stimulus package for Tanzania? Mtikisiko upi huo tuliupata hata tupate mmapesa yetu yote hayo yatolewe; kwanza international trade yetu ni negligible. Sis tunategemea subsidy kwenye badget kutoka kwa wfandhili (at least 50%)
  2. Haya makampuni yaliyopewa stimulus yanafanya backbone ya economy?
  3. For this I believe we have a coward president, a president who doesn't think

  About 1.7 trillion unaccountable; a stimulus pckage, hawa wabunge wetu inabidi wawekwe lupango wote, they are good for nothing! Overall sielewi stimulus package for what?

  Kwa nini was-invest kwenye infrastructure? wizi wizi? Hata kama President ni mwizi; basi nimekata tamaa; otherwise a mass action is needded, you can't prostitute us this way, we need respect!
   
 16. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ****** alijitapa kuwa ni ya kihistoria, sasa ndo muone sasa kuwa huwa utakuwa ufisadi wa waziwazi wa kihistoria. I hate jk go hel
   
 17. FuturePresident

  FuturePresident JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 322
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa Mwendo huu hata tufanyeje yaliyotokea Tunisia ,Misri Libya na kwengineko yatatokea tuu hapa kwetu......You can fool some people some times but you can`t fool all people all of the time......Tanzanians one days will see the light and they will stand for their rights........ .....Chota chota mabilions, cku inakuja mtasimama kizimbani kama Mubarak na watoto wake hata kama wakati huo mnamiaka zaidi ya 80...na Mungu awape maisha marefu ili tuje kuwahukumu katika uzeee wenu
   
 18. Bob

  Bob JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2011
  Joined: Sep 10, 2007
  Messages: 277
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hii ngoma bado mbichi sana.
  Hakuna marefu yasio na ncha.
  Time will tell, yetu macho, masikio, ubongo wa kuchanganua mambo, ........
   
 19. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Yaani hizi taarifa zinauma mbaya. Tunaviongozi wabinafsi, walafi, wanyonyadamu sijapata kusikia popote. Na chaajabu zaidi hakuna hatua zozote zitakazo chukuliwa dhidi yao. Jamani mimi mwenzenu nimechoka na mambo haya, pls ni lazima tufanye kitu hapa.
   
 20. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Mtapiga kelele sana(wananchi)lakini Kama hamtachukua vitendo sambamba na kelele zenu basi itakuwa ni bure.Wapo watu bado ni waoga kiasi JK aliposema Chadema inaleta vita waliogopa.Arusha tupo tayari kwa lolote lile tatizo lipo ktk mikoa mingine wamelala usingizi wa pono.
   
Loading...