Siri za Malasusa kumega kanisa zavuja

Matatizo makubwa kabisa ambayo nchi hii inayo, wala si ufisadi, umaskini, na hata madawa ya kulevya, bali ni ukosefu wa viongozi wa kiroho wenye kujisimamia wenyewe, kusimamia familia zao, kulisimamia kanisa na taifa. Kuwa na aina hii ya viongozi wa kiroho katika taifa ni majanga!

huyo jamaa ni kwel atakuwa anahusika, nachelea kumuita askofu, maana hana sifa yakuwa asikofu....

Hivi haiwezekani kung'atuka kwenye nafasi ya uongozi wa kiroho?!
Malasusa mbona unatia aibu hivi??!!

Kama kweli Malasusa ndo kaongea haya basi kanisa liko hatarini maana hakuna haja mtumishi wa Mungu kujibizana na watu huku ukisingizia wanasiasa

Huyo nilikua namheshimu sana kama askofu lakini kwa maelezo haya sipindishi maneno ni lazima katenda ila serikali inamlinda, akipelekwa mahakamani kesi wala haitachukua wiki
Why people are judging without any prove? Naona lengo la mleta habari limefanikiwa, huyu ni miongoni mwa mwa waandishi wanatumika.
 
hivi toka lini boss wako anakuja kukuona kwenye eneo lako la kazi halafu wewe unamzuia na unachukua jukumu la kutoka na mkeo kwenda mfuata hotelini? huyu ni jipu katika kanisa
 
Awahusisha maaskofu sakata lake la uzinifu Adai chanzo ni yeye kuwakataa kumrithi

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), ameshindwa kujisafisha dhidi ya tuhuma kuwa amezini na mchungaji wake, anaripoti Pendo Omary.

Askofu Dk. Alex Malasusa, anatuhumiwa anatuhumiwa kujihusisha kimapenzi na mchungaji wa kanisa hilo ambaye ni mke wa mtu, Leita Ngowi.

Akizungumza kwenye mkutano wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), mjini Dodoma, Alhamisi wiki hii, Askofu Dk. Malasusa ameishia kusema, “kuchafuliwa kwangu ni vita maalum ya watu wa Kaskazini wakiongozwa na maaskofu wao.”

Amesema, chanzo cha kuchafuliwa kwake kunatokana na hatua yake ya kukataa kumuunga mkono aliyekuwa mgombea wa urais UKAWA, waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa.

Alisema, “unajua wenzetu kule Kaskazini wote ni UKAWA. Sasa mimi nilikataa upuuzi huo wakanichukia.”

Mtoa taarifa wa gazeti hili amesema, kabla ya kwenda Dodoma, Askofu Dk. Malasusa alinukuliwa akisema, jitihada za kumchafua zinaendeshwa na baadhi ya viongozi serikalini na ndani ya kanisa.

Anasema, baadhi ya maaskofu wenzake wa kanisa hilo, hasa wale wanaotoka ukanda wa Kaskazini, walipomuona anaunga mkono John Pombe Magufuli, aliyekuwa mgombea urais kupitia CCM, waliamua kumshtaki kwa Reginald Mengi naLowassa.

Aidha, Askofu Dk. Malasusa alimtuhumu maaskofu wengine wa Kanda ya ziwa Victoria, akiwamo Askofu mmoja (jina linahifadhiwa), kuwa ndiye kinara wa yeye kuchafuliwa.

Anasema, Askofu huyo ambaye anaonekana kuwa na nguvu ndani ya kanisa hilo amekuwa na chuki binafsi dhidi yake.

Kuibuka kwa Askofu Dk. Malasusa, kutuhumu maaskofu na viongozi wengine wa kisiasa nchini, kumekuja wiki moja baada ya Mchungaji Leita kunusurika kifo.

Mchungaji huyo anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Askofu Malasusa, alinusurika kifo wiki mbili zilizopita, baada ya jaribio lake la kutaka kujiua kwa kutumia sumu kugonga mwamba.

na Leita Ngowi, mchungaji na mkurugenzi wa idara ya wanawake usharika wa Azania Front, jijini Dar es Salaam anadaiwa kutaka kujiua baada ya Askofu Malasusa kulazimisha uongozi wa kanisa lake kumpa likizo ya lazima mchungaji wake.

Leita Ngowi, ni mke wa Venance Mwakilima, mkazi wa eneo Vikawe, Bagamoyo, ambaye ni mfanyakazi wa Shule ya Msingi Dunda.

Akizungumza katika mkutano huo wa viongozi wa kiroho, Askofu Dk. Malasusa ametaja maaskofu wawili kutoka ukanda wa Kaskazini, kuwa ndiyo wanaoendesha kampeni za kumchafua.

Anasema, sababu ya maaskofu hao kumchafua inatokana na kukasirishwa na hatua yake ya kuwakatalia kuwa warithi wa nafasi yake ya ukuu wa kanisa.

Amesema, “tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa kanisa letu, maaskofu hao wa Kaskazini wamekuwa wakinichukia; na nilipoona huu uchafu magazetini nilijua kuwa watakuwa ni wahusika wakuu, kwa sababu kila mmoja alitaka kuwa mkuu wa kanisa. Nimekataa.”

Mtoa taarifa anasema, taarifa kuwa Askofu Malasusa anatuhumu watu wa Kaskazini kumchafua, tayari zimetinga kwa mkuu wa sasa wa kanisa hilo, Askofu Dk. Fredrick Shoo; ambapo alilazimika kufanya safari hadi jijini Dar es Salaam kwa lengi la kukutana na Malasusa.

Hata hivyo, Askofu Malasusa aligoma kukutana na mkuu wake, Dk. Shoo kwa madai kuwa hata yeye ni mtuhumiwa kwa sababu ni rafiki wa karibu wa “wabaya” wake.

“Kwa kweli ndugu yangu, Baba Askofu Shoo amelazimika kusafiri hadi Dar es Salaam kukutana na Malasusa ili kuzungumza mambo haya. Lakini ameshindwa kumuona.

“Askofu Malasusa amekataa Dk. Shoo kufika ofisini kwake Luther House; badala ya majadiliano mengi na baadhi ya watu kuingilia, ndipo Askofu Malasusa aliamua kumfuata Askofu Shoo hotelini akiwa ameambatana na mkewe,” ameeleza.

Naye Dk. Shoo ananukuliwa na mtoa taarifa akisema, “…ni kweli nilitaka kuonana na Baba Askofu Malasusa. Lakini alipofika na mkewe hotelini kwangu, nimeshindwa namna ya kusema naye. Nimeishia kumpa pole na akaondoka kwa manunguniko makubwa.” Hakufafanua.
Ndugu una nini na huyo askofu mbona umemuandama kiasi hicho???
 
Malasusa anaandamwa kwa kuwa alimkaribisha Dr. Magufuli Azania Front kwny Misa ya Pasaka kabla ya hapo alikuwa akisifiwa mno na wanaomkashifu leo.
Kurudi kwake CCM kutoka Ukawa baada ya kustaafu Jakaya Kikwete isifanywe ni kuliasi Kanisa.
Fanya research kabla ya ku post humu, Askofu amekua akiandamwa na haya mambo kabla ata ccm hawajafikiria kumpitisha magu, aliwahi kutuhumiwa kununua makahaba nje ya nchi, fuatilia yawezekana ikawa ana tabia hiyo kwani nae ni mwanadamu.
 
Kama kweli haya maelezo ni ya dr malasusa basi huu u dr hauna maana.
Hata mswaga ngombe porini hawezi kujitetea kama hivi.
Dr maelezo yake kachanganya kila kitu chumvi sukari pilipili tangawizi.
Du dr askofu yuko aina hii hao waumini watakuwaje au anaharibikia uzeeni kama mungunye?
 
Hah.... Kazi ipo...
Kama kweli Malasusa kajitetea hivyo, hakika amekwisha. Tena atakuwa mzinifu kweli. Leita Ngowi Mchaga, Mumewe Mnyakyusa(Mwakilima) ambaye kwa Uzi wa nyuma ndiye alimtuhumu. Askofu kama ni kweli TUBU acha kushutumu watu kwa Uzinzi wako. Hii dhambi utatubu lini naona inakutafuna hadi unasema Uongo Na ionaonekana una dhambi ya Chuki kwa Viongozi wenzako wa Kiroho
Farisayo aka Sadukayo
 
Mbona haeleweki? Daktari gani hana maelezo ya kina na yenye unyofu zaidi ya haya ya kupinda pinda?
Mara ooh vita imetokana na kutomuunga mkono Lowassa ktk mbio za urais hapa anamdanganya nani? Anatafuta mbeleko ya Magufuli? Nani hajui Malasusa alikua baba wa familia ya Lowassa? Nani hajui Malasusa ndiye mshauri muhimu na mshirika binafsi wa lowassa wa siku nyingi? Lini alimuunga mkono Magufuli? Haha anatafuta kuatamiwa si bure!!
Haya huyo huyo tena analeta kisingizio kingine kuwa alikataa kuwapa uaskofu mkuu maaskofu wawili wa kaskazini hivi tangu lini yeye akawa mtoaji wa madaraka hayo?

Mara kiongozi wa kanda ya ziwa Mara viongozi serikalini!!!

Malasusa anatia aibu na anaaibisha wasomi kwa kuwaya waya kwake.
KAMA KAJIPIGIA KUNA UBAYA GANI JAMANI
 
Kama kweli Malasusa kajitetea hivyo, hakika amekwisha. Tena atakuwa mzinifu kweli. Leita Ngowi Mchaga, Mumewe Mnyakyusa(Mwakilima) ambaye kwa Uzi wa nyuma ndiye alimtuhumu. Askofu kama ni kweli TUBU acha kushutumu watu kwa Uzinzi wako. Hii dhambi utatubu lini naona inakutafuna hadi unasema Uongo Na ionaonekana una dhambi ya Chuki kwa Viongozi wenzako wa Kiroho
Farisayo aka Sadukayo
Fanya research kidogo. Mch. Leita Ngoi (siyo Ngowi), ana asili ya DRC na si Mchagga.
 
  1. Ni watu gani waliokp serikalini wanampiga vita
  2. Kwa mini huyo mama a take kujiua? Kama hakudinywa kwa mini afanye jaribio hill?
  3. Kwa nini amzuie mchungajo kwenda likizo?
  4. Kama hana kosa na kujihesabia haki kwa nini akatae kukutana na askofu shoo?? Suluhu ya tatozo hill nani wa kulitatua?
  5. Kwa mini anapindisha maelezo anaruka ruka?
Huyu malasusa na mwenzake wa iringa watalihirikisha kanisa lao...wanapenda ngono sana
 
Biblia inatamka wazi kuwa uasherati usitajwe kwenu kamwe. Je, ni kweli hujawahi kufanya uzinzi na huyo mwanamke anayetajwa? Malasusa, kwa nini unatajwa wewe wakati kuna maaskofu wengi tu? Malasusa wakati wote kumbuka Mungu anakuona na hata unapopanga uongo ukidhani utajiokoa anakuona. Ninakushauri usijihesabie haki ambayo huna. Tubu uovu huu. Mungu ni mwaminifu. Kama utatubu kweli atakusamehe. Lakini kama utaendelea kutafuta kiki kwa wanadamu na utetezi wa uongo utazidi kwenda mbali na Mungu. Kumbuka hapa hatuna mji udumuo na wala hakuna mwanadamu mwenye mbingu.
 
Hivi haiwezekani kung'atuka kwenye nafasi ya uongozi wa kiroho?!
Malasusa mbona unatia aibu hivi??!!
Ang'atuke kwa HOJA zipi mkuu au porojo za hapa JF, huu ni upepo kama upepo mwingine ulivyowahi kutokea, utapita tu. Just the matter of TIME
 
hivi toka lini boss wako anakuja kukuona kwenye eneo lako la kazi halafu wewe unamzuia na unachukua jukumu la kutoka na mkeo kwenda mfuata hotelini? huyu ni jipu katika kanisa
Hawajala kiapo cha utii....Ukihudhuria ibada ya Upadrisho Kanisa Katoliki utaelewa nini maana ya kiapo cha utii...

System ya utii kwa viongozi wa kanisa Katoliki imeigwa na majeshi mengi...
 
Ndio shida ya watumishi wa mishahara! kanisa limechafuka! Malasusa utubu yaishe! mnatuaibisha washarika wenu! wapo na wengine huku moro. siku zao zinahesabika, nitaweka mambo yao hadharani wasipoacha.
 
Back
Top Bottom