Siri za madereva taxi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri za madereva taxi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Nov 21, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Nov 21, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  SIRI ZA MADEREVA TAXI
  Bwana juma alikuwa anatafuta taxi ya kumpeleka mbezi beach ghafla akapata gari moja taxi iliyokuwa inaelekea mbezi beach , bwana juma alikuwa na haraka sana akamwambia Yule dereva wa taxi aendeshe gari kwa mwendo wa kasi ili wawahi kufika , walipofika lugalo wakakuta foleni kubwa dereva wa taxi ikabidi apitie njia ya kawe kuepuka foleni .

  Alipopita njia hiyo kwenye kipori kidogo ulikuwa ni usiku hakuna watu kule na magari ni machache – dereva wa taxi akasimamisha gari akamtolea juma silaha akamwambia atoe vyote alivyokuwa navyo na ashuke kwenye gari , bwana juma alifanya hivyo akatoa kila kitu , pesa simu na vingine kwa kushikiwa silaha – dereva wa taxi huyoo akaenda zake mbio .

  SOMO LA KWANZA LINATUFUNDISHA KUPANDA TAXI KWENYE VITUO VINAVYOTAMBULIKA AU KAMA UNACHUKUWA TOKA SEHEMU ZINGINE HAKIKISHA UNAMJUA MTU HUYO .

  Siku nyingine tena bwana juma alichelewa kutoka kazini kama kawaida akaamua kuchukuwa taxi sasa sehemu ambayo anaijua pamoja na kujuana na watu kadhaa pale siku hiyo alichukuliwa na dai waka , kufika mbele ya safari akabadilishiwa kibao akachukuliwa tena pesa na mali zake .
  Bwana juma akafikisha suala hili kwenye vyombo vya usalama , askari akafika pale bwana juma akaonyesha gari ambalo lilimpakia usiku huo , lakini Yule daiwaka hakwepo - mwenye gari akasema usiku huo gari yake ilikuwa imeshalazwa , wakaamua kwenda sehemu ambayo gari hiyo hulazwa .
  Kufanya ukaguzi ikaonekana kweli gari ile iliandikishwa kwa ajili ya kulazwa kwenye kituo hicho ilikuwa balaa wale wenye gari nusu wamtoe juma ngeu na kudhalilisha kwa tabia yake hiyo .

  WATU WENGI WANAOLAZA MAGARI HUWA WANALIPWA KUANDIKISHA MAGARI YANAYOFANYA UHALIFU USIKU – KWAHIYO GARI ILE ILIANDIKISHWA KAMA IMELALA ILA UKWELI HAIKULALA PALE NI MLINZI ALIHONGWA PESA AANDIKA GARI IMELALA KUMBE ILIENDA KUFANYA UHALIFU .

  Siku nyingine bwana juma akapanda tena taxi , aliyekuwa anaendesha taxi akawaambia wenzake kwa njia ya sms kwamba amepata ngombe ( wanaoibiwa wanaitwa ngombe ) kwahiyo vijana wenzake wakae mkao wa kula .
  Kweli bwana Yule dereva wa taxi akaendesha taxi mpaka kwa jamaa zake kufika pale akabadilika akawa mbogo mara akasema Yule aliyepakiwa yaani juma alikuwa anamtishia kwenye gari lake ndio maana akaamua apaki pale
  Wenzake wakamsapoti wakampa kibano kidogo juma wengine wakamsachi mali na vitu vyake wakamchukulia -- kisha wakamwambia aondoke au watampeleka polisi .
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  eeeh sasa mbona hata hawa ma dreva Tax tutaanza kuwaogopa kama tabia zao ndo hizi
   
 3. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Tunashukuru kwa elimu uliyo itoa. Mimi nawashauri abiria wanapochukua taxi, kama hawamfahamu driver,basi wawe makini sana, na wawe ndo wanaotoa maamuzi waelekee wapi na si driver awaelekeze wapite njia gani.

  Pili wasikubali kuingia kwenye taxi ambayo tayari kuna mtu mwingine bali na dreva hatakama driver atajitahidi kumtambulisha mtu huyo.

  Tatu wasiwe na mazoea ya kukaa seat ya mbele karibu na driver, bali wakae seat za nyuma, kwani ukikaa seat ya mbele, driver anaweza kupunguza mwendo sehemu fulani na watu wengine ambao si wema wakaingia seats za nyuma na kukudhuru
   
 4. Sugar wa Ukweli

  Sugar wa Ukweli JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna rafiki yangu mmoja msichana alichukua taxi posta usiku akaambiwa tsh 1000 kwa kwenda Ubungo hivyo ni ya kuchangia,wakaja abiria wengine wanaume wawili,safari ikaanza.kufika magomeni kukawa na Traffick jam dreva Taxi akashauri wapitie njia za panya,huko vichochoroni wakamkaba wakamyanganya kila kitu na kumtupa!!!
   
 5. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tunakushukuru sana kwa reminder hii, uzoefu wangu unanionyesha kwamba tatizo letu watanzania tunaaminiana sana. Cha kuzingatia ni kwamba ukichukua Tax huu ni usafiri wa kukodi hivyo kwa tafsiri wewe ndiye kiongozi wa roote hiyo, hivyo basi isijekutokea unaingia kwenye tax dereva anakwambia huyu (mtu uliyemkuta kwenye gari) ni jamaa yangu ukikubali ki usalama una bahatisha.

  kwa kuwa gari/tax uliyochukua wewe ndiye unajua mnakwenda wapi, dereva asikupangie uende na nani au mpite njia gani hili ni suala ambalo unatakiwa kupanga wewe, kwani cha kuzingatia hapa ni USALAMA KWANZA.

  Ingawa kwa vyovyote vile kuchukua tax ni risk kwa sababu mara nyingi suala la kuchukua tax huwa ni dharura na ndio maana sio rahisi usubiri hadi umpate mtu mnaye fahamiana naye. Hivyo pamoja na kubahatisha usalama ni kitu cha msingi sana kwani wa weza kupoteza maisha kwa kuwahi deal, lipi bora, uwahi deal ukihatarisha maisha au KAWIA UFIKE? Naamini jibu unalo.
   
 6. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #6
  Nov 22, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nilidhani hii tabia imekomeshwa na mhe Kova! iliwahi kunitokea zamani kidogo pale posta mpya nadhani ndio makao makuu ya huu upuuzi...bahati nzuri nilishtuka mapema vinginevyo ingekuwa balaa maana nilikuwa na "makaratasi" yangu yote muhimu!
   
 7. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #7
  Nov 22, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  bongo uodho mtupu!
   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Nov 22, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  unastuka leo? mbona haya yapo tangu miaka ya 1990? sema siku hizi yameongezeka sana. Mimi huwa siku hizi nikiwa nimechelewa na nahitaji tax huwa lazima nimpigie simu dereva ninaye mjua.
   
 9. M

  Magezi JF-Expert Member

  #9
  Nov 22, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  mkuu unasema bongo......nenda south uone cha moto
   
 10. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #10
  Nov 23, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Muhimu!
  Si vyema kubadili-badili dereva kila unapochukua taxi.

  Wakati mwingine dereva taxi hana nia mbaya ila akawa mzembe. Usimtegemee yeye afanye - ni vyema uka-lock milango yote (huwa nakaa siti ya nyuma).
  Kuna matukio watu wameporwa mali zao kwa kusahau ku-lock milango.

  Ukiwa umebeba mzigo mdogo wenye vitu vya thamani, ni vyema kuingia na mzigo pamoja. Ukitanguliza mzigo kwenye gari halafu labda umezunguka ili uingie mlango wa upande wa pili....
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  Nov 23, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Mi walitaka kunifanya kitu kibaya sasa hivi nawaangalia kwa umakini sana
   
 12. s

  shabanimzungu Senior Member

  #12
  Nov 23, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tanzanians are all thieves bwana no safety anywhere?
   
 13. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #13
  Nov 24, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,289
  Likes Received: 22,055
  Trophy Points: 280

  hadithi zote hizi zinatufundisha tununue magari yetu binafsi au tutumie usafiri wa daladala kwa usalama wetu na mali zetu
   
 14. GP

  GP JF-Expert Member

  #14
  Nov 24, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mkuu hata daladala nazo ni hatari sana hasa za usiku wa manane, za buguruni na mwananyamala, usiombee!, inafika kituo fulani ghafla dreva anajifanya gari imeharibika hamadi mnaanza kukabwa na kuporwa kila kitu, huwa wanaotea sana.
  kama ni tax kwa ushauri wangu uwe na tax maalum kwa baadhi ya maeneo unayopenda kutembelea mara kwa mara
   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Nov 24, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hoja zako haziondoi umuhimu wa huduma za teksi.

  Mosi, Sio kila mtu anapenda kumiliki gari au kuwa na uwezo wa kununua gari.

  Pili, usafiri wa daladala ni usafiri wa umma na kuna routes kwa ajili ya huduma hiyo, unapokuwa na hitaji la kwenda sehemu maalum kwa ratiba maalum, usafiri wa umma unakuwa sio muafaka.
   
Loading...